KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, July 31, 2010

Uchina "ya pili" yenye uchumi bora duniani


Uchina imesema imeipiku Japan na kuwa nchi ya pili yenye uchumi mkubwa duniani kote.

Hatua nyingine ya kihistoria inashuhudiwa katika juhudi za Uchina za kujiipatia hadhi ya kuwa taifa lenye uchumi mkubwa. Kwa ujumla wengi wanakubaliana kuwa Uchina karibu iweze kuipiku Japan na kuwa taifa la pili lenye uchumi bora duniani mwaka uliopita.


Kwa hivyo wanauchumi wachache wataweza kubisha kuhusiana na madai yaliyotolewa na mratibu wa sarafu za nje wa Uchina, kuwa nchi yake tayari imeshafikia hadhi hiyo ya kuwa taifa la pili lenye uchumi mkubwa ulimwenguni.

Lakini hakuna takwimu mpya zinazounga mkono madai hayo wala kuthibitishwa na bodi za kimataifa kama vile Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, IMF.
Kuaga ufukara

Baado maelezo ya Uchina kupiga hatua katika kukua kwa uchumi wake ni muhimu. Uchumi wake umekuwa ukikua kwa takriban asilimia kumi kwa mwaka katika miongo mitatu iliyopita, na kuweza kuitoa nchi katika ufukara.

Ilipiga hatua za kuzipiku Uingereza na Ufaransa na kuwa nchi ya nne bora kiuchumi mwaka wa 2005.

Mwaka wa 2007 ikaipokonya Ujerumani nafasi ya tatu ya kuwa taifa lenye uchumi mkubwa duniani.

Kulingana na Benki ya Dunia na taasisi nyingine, Uchina itaipuku Marekanu na kuwa taifa lenye uchumi bora zaidi duniani mwaka wa 2025.

No comments:

Post a Comment