KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, July 27, 2010

Marekani yazidi kusikitishwa na kuvuja kwa siri za kijeshi


Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema madhara yaliyosababishwa na kuvuja kwa nyaraka za siri za kijeshi zaidi ya elfu tisini kuhusu vita nchini Afghanistan itachukua wiki kadha kupima.

Nyaraka hizo zilizotumwa kwenye internet na shirika la Wikileaks, zimejaa shutuma , ikiwa ni pamoja na kuvishutumu vyombo vya ujasusi vya Pakistan kuwasaidia wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan.

Mwanzilishi wa mtandao huo wa Wikileaks amesema nyaraka hizo zimeonekana kufichua uhalifu wa kivita.

Mnamo Jumatatu mashirika makubwa matatu ya habari duniani yalichapisha kile yalichosema ni habari za kina zilizovuja za maelfu ya nyaraka za jeshi la Marekani katika vita vinavyoendelea nchini Afghanistan.

Magazeti haya, The Guardian, New York Times, na jarida la Ujerumani, Der Spiegel, yalisema, taarifa hizo za kina za kijeshi zinaelezea kuuawa kwa maelfu ya raia wa Afghanistan na majeshi ya NATO, na wasiwasi wa NATO kwamba Pakistan na Iran zinawasaidia wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan.

No comments:

Post a Comment