KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, July 30, 2010

Mahakama yapinga sheria ya uhamiaji Arizona

Jaji wa mahakama moja katika jimbo la Arizona nchini Marekani, amezuia kutekelezwa kwa vipengele tata vya sheria kuhusiana na uhamiaji ambavyo vilitarajiwa kuanza kutekelezwa leo.

Serikali kuu ya Marekani na makundi ya kutetea haki za binadamu wamepinga sheria hiyo ya uhamiaji ambayo ingesababisha watu kuchunguzwa zaidi.

Makundi kutoka Hispania yametaja sheria hiyo kama yenye ubaguzi.

Gavana wa jimbo hilo ambaye alipendekeza vipengele hivyo amesema kuwa atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama.

Miongoni mwa vipengele hivyo ambavyo kwa sasa vinatakiwa kuondolewa katika sheria hiyo ni kile ambacho kiliwataka maafisa wa polisi kuwahoji watu kuhusu hadhi yao ya uhamiaji watakaposimamishwa kihalali, hatua ambayo Rais Obama ameielezea kuwa ni ya upotoshaji na ubaguzi dhidi ya raia wa kigeni, hususan wa makundi ya kutoka Amerika ya Kusini.

No comments:

Post a Comment