KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, July 28, 2010

Kuelekea uchaguzi mkuu CCM kwanuka rushwa TAKUKURU kuwachunguza vigogo


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni inawachunguza vigogo kadhaa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa vitendo vya kutoa rushwa ili waweze kupitishwa kuwania ngazi mbalimbali ikiwemo Ubunge na Udiwani.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni inawachunguza vigogo kadhaa wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kwa vitendo vya kutoa rushwa ili waweze kupitishwa kuwania ngazi mbalimbali ikiwemo Ubunge na Udiwani.

Akizungumza na waandishi wa habari. jana ofisini kwake Mkurugenzi wa TAKUKURU, John Kabale alisema kuwa ofisi yake imejiandaa kukabiliana na vitendo vya rushwa ususa ni kwa kipindi chote cha kuelekea uchaguzi ambapo wanachama wa CCM kadhaa wameweza kuwanasa.

“Mpaka sasa tunawachunguza viongozi wa CCM kwa madai ya kutoa na kupokea rushwa, uchunguzi ukikamilika tunawafikisha mikononi mwa dola” alisema Kabale.

Kabale alisema kuwa ofisi yake inafanya kazi usiku na mchana kubaini vitendo vya rushwa vinavyofanywa na wagombea wa nafasi mbalimbali kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi kati ya kazi hizo ni kukusanya ushahidi na kupata taarifa ambazo zitasaidia kuwafikisha katika chombo cha dola.

Hata hivyo Kabale hakuwa tayari kutaja majina ya vigogo hao wa CCM, ambapo alidai kuwa kwa sasa ni mapema mno. “ Tumewabaini wengi kwa tuhuma za kutoa rushwa karibu majimbo yote ya Mkoa wa Kinondoni, hivyo tukikamilisha tutawahoji pamoja na kupandishwa mahakamani’ alisema Kabale.

Mbali na hilo ofisi hiyo ya Kinondoni iliweza kutibua dili katika uchaguzi wa UWT wa CCM uliofanyika ukumbi wa Urafiki jijini Dar e Salaam baada ya kupokea taarifa ambapo walitega mitego licha akina mama wa UWT kuishtukia, ambapo bado wanaendelea kuchunguza huku akiwataka wananchi kutoa taarifa za vitendo vya rushwa ilikudhibiti tatizo hilo.

Taarifa za kuaminika kutoka vyanzo mbalimbali ziliiambia nifahamishe kuwa maafisa wa TAKUKURU ilimshikiria aliyekua diwani wa Kata ya Magomeni Julian Bujugo na kumuhoji kwa madai ya kutoa rushwa ambapo walimuachia muda mfupi hivi karibuni.

Chanzo kingine kiliiambia nifahamishe kuwa baadhi ya vigogo wapo katika ‘danger zone’ ya TAKUKURU; ambapo jimbo la Kinondoni wapo wawili,Ubungo wawili huku Kawe ikiendelea na uchunguzi kubaini vitendo hivyo.

No comments:

Post a Comment