KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, July 20, 2010

Kongamano laanza kujadili Afghanistan


Wajumbe kutoka nchi mbali mbali duniani wanakusanyika hii leo mjini Kabul kwa kongamano la kwanza la kimataifa nchini Afghanistan.

Mkutano huo utajadili harakati za mpito hasa hatua zinazohitaji kuchukuliwa kuwawezesha raia wa Afghanistan kusimamia ukarabati wa nchi yao.

Rais Hamid Karzai anatarajiwa kuwa shawishi wafadhili kuwa amepanga mikakati mizuri ya kuhakikisha kuwa shughuli hiyo itafanyika kwa uwazi. Wakati ambapo ufisadi ukithiri serikalini

Huu ndio mkutano mkubwa kabisa wa kimataifa kuwahi kufanyika mjini Kabul baada ya kipindi cha miaka 30.

Wanajeshi na polisi wanashika doria katika maeneo mengi mjini humo hii inafuatia mashambulizi ya hivi karibuni yaliotekelezwa na kundi la taliban.

Maada kuu kwenye mkutano huo ni juhudi za raia wa afghanistan kuchukua mamlaka ya kusimamia ujenzi mpya wa nchi yao baada ya muda mrefu wa vita.

Wafadhili wa nchi hiyo wakiwemo marekani wanaunga mkono juhudi hizo ila nao wanataka serikali iwajibike na ikomeshe ufisadi.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon amemtaka rais Hamid Karzai aelezee mipango yake madhubuti ya kusimamia mkakati huu wa ujenzi wa nchi yake huku akiangazia hatua atakazochukua kuwapa imani wafadhili.

Rais Karzai anatarajia kuelezea mikakati kuhusu utawala bora, mpango wa kuendesha maendeleo, na matumizi bora ya pesa kutoka kwa wafadhili.

Waziri wa mambo ya nje wa marekani Bi hilary clinton ni mmoja wa viongozi muhimu wanaohudhuria mkutano huo.

Alipowasili walipokewa kwenye uwanja wa ndege na balozi wa marekani nchini humo Karl Eikenberry na kiongozi wa kikosi cha NATO jenerali David Petraeus.

Watu hawa wawili wanawakilisha mbinu mbili ambazo marekani na Nato wanatumia kujaribu kutuliza hali nchini Afghanistan, ikiwa ni zile za kijeshi na diplomasia.

Marekani kama washirika wengine inataka raia wa afghanistan waweze kusimamia ujenzi wa nchi yao na Bi clinton akizungumza na Rais Karzai alisema vita vinavyoendelea nchini afghanistan ni muhimu sana na akawaomba walio na tashwishi kuhusu juhudi zao nchini Afghanistan wawe na subira.

Hata hivyo wanaokosoa mikakati hiyo wanahofu na uwezo wa rais Karzai kusimamia kikamilifu juhudi za kuikarabati nchi hiyo kutoka na viwango vya juu vya ufisadi.

Tangu mwaka wa 2001 nchini hiyo imepokea dola bilioni 36 lakini haieleweki zimetumika vipi. Nayo benki ya dunia mara kadhaa imelalamika kuwa dola za kimataifa zinayoisaidia afghanistan hazi fanyi chochote kukuza uwezo wake wa kusimamia fedha hizo.

No comments:

Post a Comment