KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, July 1, 2010

11 wanusurika kifo wakiwa kwenye jahazi Dar


WATU 11 wamenusurika kufa maji Dar es Salaam, baada ya jahazi walilokuwa wakisafiria kugongana na boti ya Kampuni ya Sea Gull iliyokuwa ikienda Zanzibar.

Ajali hiyo ilitokea jana, majira ya mchana wa saa 7, katika eneo la feri wakati jahazi hilo lilipogongana na boti hiyo ubavuni na kuingizwa majini umbali wa mita 200 ndani ya bahari.

Jahazi hilo linajishughulisha na usafirishaji wa vinywaji aina ya bia kati ya Dar es Salaam na Zanzibar.


Jahazi hilo kwa muda huo lilikuwa linatokea Zanzibar likiwa na limebeba kreti tupu zipatazo 1400 na linakuja Dar es Salaam kubeba bia na kuzipeleka tena Zanzibar.

Watu hao waliokolewa kwa kuonyesha ishara ya kitambaa na kuja kuokolewa wakiwa karibu na kutua nanga.

Walionusurika katika ajali hiyo ni Nahodha mkuu wa jahazi hilo, Musa Machano (35), Kaimu Amri (50), Musa Machano (35), Hamis Abdalah (18), Hamis Makame(14) Nasoro Muhamed(15).

Wengine ni Rashid Fumo (15), Hamis Shauri(24), Haji Shabani (22) na Mati(32)..

No comments:

Post a Comment