KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, July 28, 2010

10 wafa ajalini papohapo -Tanga


WATU 10 wamefariki dunia papohapo baada ya basi walilokuwa wakisafiria kiugongwa uso kwa uso na lori huko Segera mkoani Tanga.
Inadaiwa kuwa abiria hao walikuwa wakisafiria na basi dogo aina ya Hiace na kugongwa na lori hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa waTanga, Bw. Liberatus Sabas, alithibitisha na kusema ajali hiyo ilitokea majira ya usiku jana kati ya Hale na Segera.

Amesema kuwa basi hilo lilikuwa likitokea Hale kuelekea Segera na lori hilo lilikuwa likitokea Segera kwenda wilayani Muheza.

No comments:

Post a Comment