KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, June 18, 2010

Sanamu la Yesu Lapigwa na Radi, Lateketea Kwa Moto


Sanamu kubwa sana la Yesu lilikowa likijulikana kama 'Mfalme wa Wafalme' ambalo lilikuwa kivutio kikubwa cha watalii mjini Ohio nchini Marekani limepigwa na radi na kuteketea kwa moto.
Sanamu hilo maarufu lenye urefu wa mita 19 na upana wa mita 12 liliteketea kwa moto baada ya kupigwa na radi jumatatu usiku, taarifa ya polisi ilisema.

Sanamu hilo lililokuwa likijulikana kama "King of Kings" lilikuwa ni miongoni mwa vivutio vya watalii kusini magharibi mwa Ohio kuanzia mwaka 2004 lilipowekwa pembeni ya barabara ya kuu inayokatiza mbele ya kanisa la Kianglikana Monroe.

Taarifa ya polisi ilisema kuwa sanamu hilo liliteketea kwa moto jumatatu usiku kabla ya moto huo kudhibitiwa na maafisa wa zimamoto. Hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo.

Sanamu hilo liligharimu dola 250,000 kulitengeneza na kutokana na ukubwa wake watu wengi wanaopita kwenye barabara ya Interstate 75 walikuwa wakisimama kwa muda mbele ya kanisa ili kupata taswira za sanamu hilo

No comments:

Post a Comment