KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, June 24, 2010

Obama amfuta kazi generali McChrystal
Rais wa Marekani, Barack Obama, amemteua mmoja wa maafisa wake wakuu jeshini Generali David Petraeus, kama kamanda mkuu wa majeshi yote ya kigeni nchini Afghanistan.

Hii ni kufuatia kuachishwa kazi ghafla kwa ,Generali Stanley McChrystal kuhusu matamshi yake ya kuhujumu serikali ya Obama.

Kulingana na rais Obama matamshi ya McChristal yameonyesha hana imani na serikali na pia ni ya kuhujumu jeshi analolihudumia.

Jenerali McChrystal aliitwa kutoka Afghanistan kwenda Washington kujieleza kutokana na kauli aliyoitoa dhidi ya utawala wa Marekani.

Matamshi aliyotatoa bwana McChrystal yamechapishwa kwenye jarida la Rolling Stone.

Mwandishi wa BBC wa maswala ya usalama alisema kuwa generali Petraeus alikuwa miongoni mwa watu waliopelekwa vitani Iraq na kubuni sera ambazo sasa zinatumika kutafuta usalama na kumaliza vita nchini humo.

No comments:

Post a Comment