KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, June 5, 2010

Mke wa Rais Zuma Ala Uroda na Mlinzi Wake

Familia ya mke wa pili wa rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma imelazimika kumlipa Zuma fidia ya mbuzi mmoja mweupe baada ya kugundulika kuwa mke huyo wa rais Zuma aliisaliti ndoa yake na kula uroda na mlinzi wake. Utata upo kwenye ujauzito alio nao hivi sasa mke huyo wa rais.
Imegundulika kuwa mke wa pili wa rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Nompumelelo Ntuli alifukuzwa toka nyumbani kwa Zuma siku chache kabla ya krismasi baada ya kugundulika alimsaliti Zuma na kutembea nje ya ndoa.

Ntuli alimpa uroda mlinzi wake, Phinda Thomo mkazi wa Dobsonville, Soweto. Mlinzi huyo alijiua mwenyewe baada ya siri kufichuka kuwa ametembea na mke wa rais.

Ntuli ambaye hivi sasa yuko pamoja na Zuma katika safari ya kiserikali nchini India, ana mimba ya mtoto anayetarajiwa kuwa mtoto wa 21 wa Zuma. Hata hivyo maswali mengi yamezuka kuhusiana na ukweli wa baba wa mtoto huyo aliye tumboni mwake.

Taarifa zinasema kuwa Ntuli mwenye umri wa miaka 35 aliamua kufanya hivyo baada ya kukasirishwa na hatua ya Zuma kutangaza kuoa mke wa tatu.Taarifa zaidi zinasema kwamba Ntuli alimtukana mke wa tatu wa Zuma Tobeka Madiba na pia alitishia kutohudhuria harusi yake iliyofanyika mwezi januari mwaka huu, hata hivyo alibadilisha uamuzi wake na kuhudhuria harusi hiyo lakini alifukuzwa na kurudishwa kwao wakati wa sherehe za kitamaduni za harusi hiyo.

Ntuli alisindikizwa na wazee wa kijadi hadi kwenye nyumba ya familia yake ambapo alikabidhiwa kwa wazazi wake.

Ntuli aliambiwa kuwa kitendo chake cha kuisaliti ndoa yake kimeikasirisha familia ya Zuma na mizimu ya mababu.

Ili kuweka mambo sawa mwezi aprili mwaka huu, familia ya Ntuli ilienda kwa mzee Zuma na kumlipa fidia ya mbuzi mmoja mweupe ambaye alichinjwa siku hiyo hiyo.

Habari za Ntuli kumsaliti Zuma zimeigawanya Afrika Kusini ambapo watu wengi wanampongeza Ntuli wakisema kuwa kama Zuma anazisaliti ndoa zake kwanini wake zake nao wasimsaliti.

Mmoja wa watu waliopiga simu redioni kujadili suala hilo alisema kuwa Zuma ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 68 hayawezi tena mambo ndio maana mke wake ametembea nje.

No comments:

Post a Comment