KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, May 26, 2010

Wanajeshi wa UN kuondolewa Chad na CAR

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura kuidhinisha kuondolewa kwa wanajeshi wa Umoja huo kutoka nchi za Chad na Jamuhuri ya Afrika ya Kati.Shirika la kutetea haki za Binadamu Human Rights Watch limepiga hatua hiyo likisema Chad haijathihirisha uwezo wake kulinda usalama wa Raia.

Baraza hilo lilipiga kura kuondolewa kwa wanajeshi 3,000 ifikapo mwisho wa mwaka huu. Thuluthi ya wanajeshi hao wataanza kuondoka mwezu Julai na kikosi cha mwisho kikiaga mwezi oktoba. Kikosi cha Umoja wa Mataifa kilikuwa na jukumu la kuwalinda wakimbizi nusu milioni kutoka Chad wana wengine ambao wamekimbia vita nchi jirani ya Sudan.

Chad na Jamuhuri ya Afrika ya Kati zimekumbwa na machafuko mashariki mwa maeneo yao. Hata hivyo mamlaka ya Chad imesisitiza kwamba ina uwezo wa kuthibiti maasi yeyote licha ya uwezo huo kutiliwa shaka na baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Wakati huo huo mashirika ya kibinadamu yameonya dhidi ya kuondolewa kwa wanajeshi wa kulinda amani yakisema hali huenda ikahatarisha maisha ya wakimbizi na juhudi za kutoa misaada.

Lakini rais Idriss Deby amesema kikosi cha Umoja wa Mataifa hakijafanikiwa kubadilisa hali nchini humo.

No comments:

Post a Comment