KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, May 11, 2010

Wanajeshi 2,000 wa UN kuondoka Congo


Balozi wa Ufaransa katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Pierre Jacquemot, amesema kuwa Umoja wa Mataifa umependekeza kuondoa vikosi vya kulinda amani 2,000 kufikia mwishoni mwa mwezi ujao.

Wanajeshi wengine 20,000 wataendelea kubaki hadi hali ya usalama itakapo imarika.

Katika mahojiano na shirika la habari la Reuters,Bw Jacquemot amesema Umoja wa Mataifa utafanya kama serikali ya Congo ilivyotaka ya kuondoa wanajeshi wa kulinda amani hatua kwa hatua,ikiwa hii ni idadi kubwa ya vikosi vya kulinda duniani kote.

Alisema maelezo kamili ya mapendekezo yatawasilishwa kwa serikali ya rais Joseph Kabila na ujumbe utakaongozwa na Ufaransa wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa baadaye mwezi huu.

No comments:

Post a Comment