KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, May 12, 2010

Wanafunzi SUA wasakwa kwa mauaji

JESHI la POLISI Mkoani Morogoro linawasaka wanafunzi sita wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mlinzi wa anayelinda chuoni hapo Jafari Thabiti [38] wa Kampuni ya Moku.
Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Thobias Andengenye alisema wanafunzi hao walifanya shambulio hilo Mei 8, mwaka huu, majira ya saa 12:00 jioni chuoni hapo.

Alisema mlinzi huyo alishambuliwa na wanachuo hao na alipata majeraha sehemu ya kichwani na sehemu nyingine za mwili baada ya kumtuhumu kusababisha upotevu wa simu ya mkononi katika bweni la wanafunzi wa kike wa chuo hicho.


Kamanda aliendelea kusema kuwa, mlinzi huyo alifariki siku mbili baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

Wanafunzi wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo ni sita na wanasakwa na jeshi hilo kwa uhalifu huo

No comments:

Post a Comment