KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, May 3, 2010

Vitu 10 tulivyojifunza kuhusu Afrika


Vitu 10 tulivyojifunza kuhusu Afrika

Kituo cha utafiti cha Pew kimezindua uchunguzi wao juu ya namna watu wanavyochukulia dini na maadili barani Africa, ambayo imeibua masuala muhimu.

Ifuatayo ni orodha ya mambo 10 tuliyojua kutokana na utafiti huo, uliyowahoji watu 25,000 kutoka nchi 19.

1.Asilimia 75 ya raia wa Afrika Kusini wana fikra kuwa ndoa ya mke zaidi ya mmoja ni ‘makosa kimaadili’- taarifa ambazo hazitamridhisha rais wao, Jacob Zuma aliyeoa mke wa tatu mapema mwaka huu na ameshamchumbia mwengine wa nne. Hata hivyo, utafiti huo umeonyesha utofauti wa maoni katika suala hilo. Wakati asilimia saba ya raia wa Rwanda wamekubaliana na ndoa za wake wengi (ambapo pia iliridhiwa na wanawake), idadi kubwa ya wanaume kwa asilimia 17 wamesema wana mke zaidi ya mmoja.

2. Idadi kubwa ya waliohojiwa wamepinga vikali mapenzi ya jinsia moja. Katika nchi tatu za Zambia, Kenya na Cameroon, mapenzi hayo yamepingwa kwa asilimia 98. Nchi moja yenye idadi kubwa ya watu- asilimia 11- wanaokubaliana na mapenzi ya jinsia moja ni Uganda, ambapo mbunge mmoja anajaribu kulishawishi bunge la nchi hiyo kupitisha sheria ya kutoa adahbu kwa vitendo kama hivyo kwa kifungo cha maisha na hata kifo kwa baadhi ya makosa.

3. Afrika huenda likawa ndilo bara lenye watu wenye imani sana ya dini, ambapo zaidi ya asilimia 80 wanamwamini Mungu. Takriban nusu ya wakristo waliohojiwa wanatarajia Yesu Kristo kurejea duniani wakiwa bado wahai. Nchini Ethiopia, asilimia 74 ya Wakristo wamesema wameshuhudia shetani au pepo mbaya kutolewa kwenye mwili wa mtu au hata wao wenyewe na asilimia 40 ya Wakristo wa Ghana wamesema wamepata wahai moja kwa moja kutoka kwa Mungu. Karibu nusu ya waislamu wote wana matumaini ya kushuhudia muungano wa kiislamu chini ya kiongozi mmoja ingali wakiwa hai.

4. Zimbabwe, ambapo watu wa Lemba wanasema asili yao ni kutoka kabila la Israel, halikuwa miongoni mwa nchi zilizofanyiwa utafiti. Lakini asilimia 26 ya wakristo wa Nigeria wanasema katika utafiti wao wamegundua asili yao inatokea Israel na Palestina.

5. Imani za kichawi ni kubwa sana Tanzania kwa asilimia 93- hii ni nchi ambayo waganga wa kienyeji wanadai viungo vya miili ya watu ni bora zaidi kutumika hasa vya albino. Ethiopia ilikuwa na kiwango cha chini cha watu wenye imani za kichawi kwa asilimia 17. Imani kuwa juju au viungo vinaweza kuzuia vitu vibaya kumtokea mtu ilikuwa ndogo sana- baina ya asilimia 20-30. Hata hivyo, asilimia 75 ya raia wa Senegal wanaamini jambo hilo linawezekana, kiwango kilichozidi hata wale wenye imani hiyo Tanzania (asilimia 49). Inaweza ikawashangaza wengi kuwa Afrika Kusini ilikuwa na idadi kubwa ya watu-aslimia 52- wakisema kuwa wanashiriki katika sherehe za kiutamaduni au kutambika kwa mizimu.

6. Kulikuwa na mgawanyiko katika dini hizo juu ya utumiaji wa pombe, unaokatazwa na dini ya kiislamu. Hata hivyo, Waislamu wengi zaidi Chad, asilimia 23, wanawafiki unywaji wa pombe, ukilinganisha na wakristo wa Ethiopia, asilimia 5.

7.Maoni juu ya talaka umeonyesha tofauti kubwa kati ya dini hizo nchini Nigeria. Idadi kubwa ya wakristo, asilimia 79, wameona kimaadili ni makosa, wakati miongoni mwa Waislamu, kwa asilimia 46-41 wamekubaliana na suala hilo.

8. Katika miaka ya hivi karibuni, Waislamu wenye msimamo mkali Somalia na Nigeria wameanza kutoa adhabu kali, kama vile kuwakata viungo wezi na hata kuwapiga mawe mpaka kufa kwa wazinifu. Wengi hawajakubaliana na adhabu hizo. Nchini Nigeria, iliungwa mkono na takriban asilimia 40 ya Waislamu na chini ya aslimia 10 ya Wakristo. Hata hivyo, wengi wameridhia na hatua ya kuwachapa na kuwakata viungo katika nchi za Senegal na Mali. Katika nchi jirani ya Guinea-Bissau, hata asilima 50 ya Wakristo wameunga mkono adhabu hiyo. Idadi hiyo ni mara mbili ya Waislamu Ethiopia (asilimia 25)- huenda kwao ikawa sawa kwa kuwa wanapakana na Somalia na Waislamu wengi wa Ethiopia kwa asili ni Wasomali.

9. Utafiti huo pia uliuliza juu ya bidhaa katika bara lililo maskini kuliko lote. Si muda mrefu sana, katika utafiti mwengine Cameroon ilionekana kuwa nafasi ya juu katika nchi zinazokunywa pombe sana ‘champagne’. Hata hivyo, la kushangaza asilimia 71 ya raia hao waliohojiwa wamesema kuna wakati mwaka jana walikosa hata fedha za kununulia chakula. Nchini Ethiopia, ambapo huonekana nchi inayohangaika kujilisha, takwimu zake zilikuwa ndogo, asilimia 30- idadi ndogo kabisa ukilinganisha na nchi zote zilizofanyiwa utafiti.

10.Hata hivyo, Ethiopia, ni nchi yenye idadi ndogo ya watu –asilimia saba- wanaotumia wavuti mara kwa mara. Rais Paul Kagame wa Rwanda yupo katika jitihada za kuimarisha uwezo wa wavuti nchini mwake. Atapata matumaini zaidi baada ya kufahamu kuwa asilimia 30 ya watu wake hutumia wavuti mara kwa mara. Simu za mkononi zinatumika zaidi, huku asilmia 81 ya waliohojiwa Botswana hutumia simu hizo. Nchi nyingi zilizofanyiwa utafiti hutumia simu za mkononi, lakini Rwanda kidogo iko nyuma kwa watumiaji wachache kwa asilimia 35 tu.

1 comment: