KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, May 24, 2010

TBL yapigwa faini kuvuruga ushindani wa kibiashara


KAMPUNI ya bia ya Tanzania Breweries Limited [TBL] imepigwa faini ya shilingi bilioni 518 kwa kukiuka na kuvuruga ushindani wa kibiashara nchini
Hatua hiyo imechukuliwa na Tume ya Ushindani ya biashara [FCC] baada ya Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries [SBL] kulalamikia vitendo vinavyochukuliwa na kampuni hiyo shindani.

Hayo yamekuja baada ya TBL kukiuka misingi ya kibiashara kwa kungo’a mabango ya biashara ya kampuni ya SBL katika baa mbalimbali yaliyowekwa na kampuni hiyo kitendo ambacho si halali kwa kanuni za kibiashara nchini.


Mbali na hilo pia TBL imekuwa ikizuia kabisa bia za kampuni hiyo zisiuzwe na kuwaagiza wamiliki wa baa wasiuze bia za kampuni hiyo ya Serengeti.

Hivyo kutokana na vitendo hivyo adhabu kali imechukuliwa didi yao na tume hiyo imetoa adhabu ya kuwakata asilimia tano ya mapato ya mwaka mzima kutoka katika kampouni hiyo.

No comments:

Post a Comment