KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, May 11, 2010

Serikali na Tucta hawajafikia muafaka


HATIMAYE mazungumzo yaliyokuwa yakisuburiwa na wengi kati ya Serikali na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA yaliyofanyika Mei 8 mwaka huu hayakutoa matunda wka wafanyakazi baada ya kutofikia muafaka kati yao.
Katika mazungumzo hayo hapakuwa na muafaka baina ya wajumbe wa tucta na serikali na hakuna jambo lolote waliloafikiana na hatimaye kila pande kuondoka bila muafka wowote kupatikana katika mazungumzo hayo.

Kufuatia kukwama kwa mazungumzo hayo viongozi wa Tucta wameamua kumpa siku 21 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia atoe tamko la serikali kuhusu mapendekezo ya wafanyakazi hao.

Hivyo waziri huyo mwenye dhamana hiyo anatakwias afanyie kazi hoja hiyo na atoe tamko ndani ya iku hizo alizopew na wfanyakazi na dyeye ndiye atakuwa na maamuzi ya kutatua suala hilo.

Na endapo atashindwa kujibu hoja hizo shirikisho hilo walidai warudishwe tena mezani katika mazungumzo kati yao

No comments:

Post a Comment