KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, May 17, 2010

Milipuko ya gruneti yatokea nchini Rwanda

Milipuko miwili ya gruneti imetokea mjini Kigali, Rwanda na kuwaua watu wawili na wengine 27 kujeruhiwa.Hii ni mara ya nne kwa mashambulio haya kutokea mjini humo katika miezi minne.
Mwa mujibu wa msemaji wa polisi Eric Kayiranga,mlipuko wa kwanza ilitokea katika eneo la kibiashara kati kati mwa jini la Kigali na karibu na kituo cha mabasi eneo la Nyabugogo.

Eneo hilo lililengwa tena na shambulizi la gruneti hapo mwezi Februari mwaka huu ambapo mtu mmoja alikufa na zaidi ya 10 kujeruhia.
Mashambulizi hayo yanatokea wakati Rwanza ikijianddaa kufanya uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu. Watawala wa Kigali wamewalaumu wanajeshi wa zamani Faustin Kayumba na Kanali Patrick Karegeya kwa kuhusika na shambulizi la mwezi Februari.

Maafisa hao wamekimbilia uhamishoni Afrika Kusini.Aidha mwanasiasa anayepinga serikali, Deo Mushahidi amelaumiwa kuhusika na matukio yanayoendelea.

Mwanasiasa huyo anazuiliwa nchi jirani ya Burundi. Polisi wamesema uchunguzi unaendelea na kuahidi kwamba wanaohusika na mashambulizi hayo watachukuliwa hatua za kisheria.

No comments:

Post a Comment