KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, May 5, 2010

Kongamano la uchumi laanza Tanzania


Kongamano la uchumi duniani litakaloangazia bara Afrika limeanza mjini Dar Es Salaam, Tanzania.

Jumla ya marais kumi na wajumbe kutoka nchi 85 wanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo la siku tatu.

Mada ya mkutano ni athari za msukosuko wa uchumi duniani na jinsi ya kuimarisha ushirikiano barani Afrika katika nyanja za uchukuzi na mawasiliano.

Wakati huohuo wanaharakati wa maswala ya Ukimwi, wametishia kufanya maandamano kunakofanyika mkutano huo kushinikiza viongozi hao kutoa msaada zaidi kwa harakati dhidi ya ugonjwa huo.

No comments:

Post a Comment