KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, April 27, 2010

Shindano la filamu fupi


Baada ya mpambano mkali ulioshirikisha filamu kutoka sehemu mbali mbali duniani, hatimaye mshindi amepatikana, naye ni Frederico Teixeira de Sampayo kutoka Hispania.

Filamu yake "Wash, Rinse and Spin", imeibuka mshindi kati ya filamu 500 zilizoandaliwa na watu wa kila aina kutoka mabara yote duniani.

Filamu iliyoshinda

Kuanzia mwezi Februari, BBC World News, katika mfululizo wa vipindi maalum vya televisheni na radio, vile vile online, walifanya shindano la kuandaa makala fupi ya video - kwa digital camera au mobile phone camera, ruksa!

Kwa upande wa Afrika, filamu iliyowika ni "Somewhere in Northern Tanzania", iliyoandaliwa na Ibrahim Matukuta mkazi wa Zanzibar.

Angalia Somewhere in Northern Tanzania

Zawadi
Video au filamu tano bora zaidi kutoka kila bara - Afrika, Amerika ya Kusini + Amerika ya Kaskazini, Ulaya, Asia na Oceania, ziliingia katika fainali ambayo inarushwa kupitia matangazo ya televisheni ya BBC World vile vile zitaonyeshwa kwenye tovuti ya BBC.

Mshindi wa jumla amepatikana na atapewa zawadi ya semi-professional HD mini DV camcorder

No comments:

Post a Comment