KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, February 1, 2010

13 wakamatwa Burundi, kwa jaribio la mapinduzi

Nchini Burundi msako mkali unaendelea baada ya wanajeshi 13 kutiwa nguvuni kwa madai ya kupanga njama za kuipindua serikali ya Rais Pierre Nkurunziza.

Madai hayo yameibuka wakati Burundi inajiandaa kufanya uchaguzi wa pili baada ya muda mrefu wa vita. Na Rais Nkurunziza amepongeza vyombo vya usalama kwa kuzima jaribio hilo.

Rais huyo ametamka hayo kabla ya kunondoka Bujumbura kuelekea Mjini Addis Ababa ,Ethiopia kuhudhuria kikao cha 14 cha Umoja wa Afrika. Lakini vyama vya upinzani vinadai kuwa hizo ni hila za serikali kwa kuhofia kushindwa kwenye uchaguzi.

No comments:

Post a Comment