KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 30, 2010

Waasi Nigeria wavunja mkataba




Kundi kubwa la waasi katika jimbo la Delta linalozalisha mafuta nchini Nigeria limesema kuwa halitoheshimu tena muafaka wa kusitisha mapigano ambapo kundi hilo lilitangaza mwezi October mwaka uliopita.
Katika taarifa yake, kundi la the Movement for the Emancipation of the Delta ( MEND), lilisema haliamini kuwa serikali ya Nigeria itatimiza matakwa ya kundi hilo, ikiwa ni pamoja na kurejesha udhibiti wa rasilimali za mafuta na ardhi kwa watu wa jimbo la Delta.



Kundi la MEND lilisema uamuzi huo ulifikiwa kwa uangalifu na mashauriano ya kina.

Kundi hili lilitoa onyo kwa makampuni ya mafuta na kuyafahamisha yajiandae kwa mashambulizi ya mitambo yao pamoja na wafanyakazi.

Wanamgambo wamekuwa wakishambulia mitambo ya mafuta na kuisababisha Nigeria hasara ya mamilioni ya fedha.

No comments:

Post a Comment