KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, January 22, 2010

Obasanjo apendekeza rais YarÁdua anayeugua ajiuzulu

sana kubakia madarakani.
Matamshi hayo ya Bw Obasanjo ni ya kwanza tangu mzozo wa kisiasa nchini Nigeria uanze wakati rais Yar'Adua aliondoka nchini humo kuenda kupata matibabu nchini Saudia Arabia, takriban miezi miwili iliyopita.

Bw Obasanjo ndiye aliyemchagua Umaru Yar'Adua kuwania kiti cha rais mwaka wa 2007. Hii ilikuwa baada ya yeye kujaribu kuwania kiti hicho kwa muhula wa tatu lakini akashindwa. Kwa hivyo, matamshi haya ya Bw Obasanjo yatazidisha shinikizo za kumtaka ajiuzulu.

Akijibu maswali wakati alipokuwa akitoa hotuba nchini Nigeria, Bw Obasanjo alisema kuwa ni uamuzi wa heshima kwa mtu anayechukua wadhifa na baadaye kushindwa kufanya kazi hiyo kwa sababu ya matatizo ya kiafya.

Wakosoaji wa rais Yar'Adua wanasema kuwa, kuwa mgonjwa kwa muda mrefu, na kukosa kupata habari kamili kuhusu afya yake, kumewacha pengo kubwa katika uongozi na kusimamisha shughuli za serikali.

No comments:

Post a Comment