KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, January 30, 2010

CUF yataka serikali ya kitaifa, Zanzibar


CUF yataka serikali ya kitaifa, Zanzibar

Chama cha upinzani CUF visiwani Zanzibar, kimewasilisha hoja binafsi kwa baraza la wawakilishi kikipendekeza kuundwe serikali ya umoja wa kitaifa.
Hoja hiyo imewasilishwa na Abubakar Khamis wa chama cha CUF.

Miongoni mwa mambo mengine yaliyopendekezwa ni pamoja na kufanyika kwa kura ya maoni mwezi Mei mwaka huu.Vilevile kimependekeza baraza litoe agizo kwa serikali kukabidhi rasimu ya mabadiliko ya katiba ndani ya wiki moja.

Bw Khamis pia amependekeza marekebisho katika maeneo manne, mkiwemo nafasi ya waziri kiongozi kuchukuliwa na mshindi wa pili wa uchaguzi.

No comments:

Post a Comment