KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, November 18, 2009

Tunisia yafukuza kocha wa soka


Mwalimu wa timu ya soka ya taifa ya Tunisia Humberto Coelho raia wa Ureno, ametimuliwa baada ya nchi hiyo kutofuzu Kombe la dunia mwaka 2010 Afrika Kusini.
Faouzi Benzarti, mwalimu wa vigogo wa soka wa Tunisia Esperance, ndiye atachukua hatamu za kuionoa timu ya taifa ya nchi hiyo kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2010 Angola.

Kumekuwa na kelele nyingi za vyombo vya habari vya nchi hiyo pamoja na raia wa Tunisia dhidi ya Coelho tangu walipofungwa bao 1-0 na Msumbiji mjini Maputo siku ya Jumamosi.

Matokeo hayo yaliifanya Nigeria waliowafunga Kenya mabao 3-2 kufuzu Kombe la Dunia kutoka kundi la B.

Coelho alitoa lawama kwamba nyasi za bandia katika uwanja wa Maputo pamoja na joto kali vilisababisha kufungwa kwao.

Lakini lawama hizo hazikupenya masikioni mwa waziri wa michezo pamoja na maafisa wakuu wa Shirikisho la Soka la Tunisia wakati wa mkutano wao uliofanyika usiku wa Jumanne.


No comments:

Post a Comment