KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 18, 2009

Polisi huko Ujerumani wamewakamata viongozi wawili wa kundi la waasi wa Rwanda


Ignace Murwanashyaka
Polisi huko Ujerumani wamewakamata viongozi wawili wa kundi la waasi wa Rwanda kwa tuhuma za uhalifu wa kivita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Ignace Murwanashyaka, kiongozi wa kundi la FDLR, na msaidizi wake Straton Musoni walikamatwa Ujerumani ambako wamekuwa wakiishi kwa miaka kadhaa, kukabiliwa na madai ya kuhusika na uhalifu dhidi ya uanadamu na makosa ya kivita.

Viongozi wa FDLR walikimbilia Kongo baada ya mauaji yaliyotokea Rwanda mwaka 1994 ambako watu zaidi ya 800,000 waliuawa.














Kukamatwa kwao kumetokea wakati walinda amani wa Umoja wa Mataifa wakiendelea kusaidia jeshi la Kongo kupambana na waasi hao wa FDLR

No comments:

Post a Comment