KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, November 17, 2009

Mwandishi Zambia hakutuma picha chafu


Mwandishi mmoja wa habari nchini Zambia aliachiliwa huru na mahakama siku ya Jumatatu baada ya kupatikana hana hatia dhidi ya mashtaka ya kuwatumia maafisa wa serikali picha zinazodaiwa kuwa za "ngono".
Ilidaiwa kuwa mwandishi huyo, Chansa Kabwela, aliwatumia maafisa wa serikali picha za mwanamke aliyekuwa akijifungua katika maegesho ya magari kwenye hospitali moja nchini humo.

Mkasa huo ulitokea wakati wa mgomo wa wauguzi na bahati mbaya mtoto aliyezaliwa alikufa. Rais Rupiah Banda wa Zambia alizielezea picha hizo kuwa pichangono.

Chansa Kabwela alisema aliwatumia viongozi hao picha husika kulalamikia athari za mgomo ulioathiri hospitali za nchi hiyo. Bi Kabwela angeweza kukabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela endapo angepatikana na hatia

No comments:

Post a Comment