KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 11, 2009

Maharamia wafikishwa mahakamani Kenya


Watu saba wamefikishwa mahakamani nchini Kenya kwa madai ya kujaribu kuteka nyara meli moja ya uvuvi katika Ghuba ya Uajemi.
Raia hao saba wa Somalia wamekabidhiwa katika mamlaka husika mjini Mombasa na mawanamaji wa Ujerumani ili kujibu mashitaka ya uharamia.

Hadi sasa zaidi ya Wasomali 100 wanaodhaniwa kuwa maharamia wamepelekwa nchini Kenya kushitakiwa kwa makosa ya uharamia.

Mwandishi wa BBC mjini Mombasa, Odhiambo Joseph anasema hata hivyo juhudi hizo zinaonekana kuwapa ujasiri zaidi maharamia hao, kuliko kuwakatisha tamaa.

No comments:

Post a Comment