KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, November 2, 2009

Homa ya mapafu yatishia vifo kwa watoto


Homa ya mapafu yatishia vifo kwa watoto

Umoja wa Mataifa umeomba dola za kimarekani bilioni thelathini na tisa kwa miaka sita ijayo ili kuzuia vifo vya mamilioni ya watoto kutokana na homa ya mapafu.
Shirika la afya duniani, WHO, na shirika la watoto duniani, UNICEF, yamesema homa ya mapafu huua takriban watoto milioni mbili chini ya umri wa miaka mitano kila mwaka.


Kiwango hicho ni zaidi ya wanaofariki dunia kwa malaria, surua na ukimwi yakichanganywa pamoja.

Hata hivyo, umoja huo unasema ni gharama ndogo na ni rahisi kuzuia homa hiyo, na tangu mwaka 2000 kuna chanjo imetengenezwa maalum ya kuwalinda watoto na maradhi hayo.

No comments:

Post a Comment