KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 18, 2009

A. Kusini ilipeleka mamluki Guinea?


Serikali ya Afrika Kusini imesema inafanya uchunguzi juu ya ripoti kwamba mamluki wa nchi hiyo wanawapa mafunzo wafuasi wa utawala wa kijeshi wa Guinea .

Kumekuwa na ripoti katika vyombo vya habari vya Ufaransa kuwa askari kutoka Afrika Kusini wanatoa mafunzo hayo katika kambi kusini mwa mji wa Conakry.

Jeshi hilo la Guinea limekuwa likishutumiwa vikali kwa mauaji ya waliounga upinzani mwezi Septemba.


Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamesema zaidi ya watu 150 waliuawa wakati jeshi la Guinea lilipowafyatulia risasi waandamanaji wanaopinga serikali na wanawake wengi kubakwa.



No comments:

Post a Comment