KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, October 16, 2009

Waziri mkuu wa Zimbabwe amesema chama chake kitajiengua kutoka serikali ya muungano


Waziri mkuu wa Zimbabwe amesema chama chake kitajiengua kutoka serikali ya muungano mpaka masuala waliyokubaliana kuhusu kugawana madaraka yatimizwe.
Morgan Tsvangirai amesema si kwamba MDC inajitoa rasmi lakini haitoendelea kushirikiana na chama cha Rais Robert Mugabe cha ZANU-PF.

Amesema hatua hiyo imeshinikizwa na kutiwa kizuizini kwa kiongozi mwandamizi wa MDC, Roy Bennet kwa shutuma za kuhusika na ugaidi.

Shirika la habari la AFP limemnukuu Tsvangirai akisema kuwa Zanu-PF si washirika wanaoaminika.

No comments:

Post a Comment