KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, October 16, 2009

Ufaransa imewasihi raia wake kuondoka Guinea huku kukiwa na ongezeko la ukosoaji wa namna jeshi la nchi hiyo lilivyoyadhibiti maandamano.

Ufaransa imewasihi raia wake kuondoka Guinea huku kukiwa na ongezeko la ukosoaji wa namna jeshi la nchi hiyo lilivyoyadhibiti maandamano.
Inaaminiwa kuna raia 2,500 wa kifaransa nchini Guinea, wengi wakiwa wafanyakazi wa kutoa misaada, wafanyabiashara wakiwa na familia zao.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamesema takriban watu 157 walifariki dunia baada ya majeshi kufyatua risasi kwa waandamanaji walioipinga serikali ya nchi hiyo mwezi uliopita.

Umoja wa Afrika umemwambia kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo aachie madaraka ifikapo siku ya Jumamosi, la sivyo atafunguliwa mashitaka.

No comments:

Post a Comment