KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, October 14, 2009

Muswada wa afya sasa wapita Marekani


Kamati ya Senate imeidhinisha muswada wa mageuzi ya afya wa Marekani, ikiwa ni hatua muhimu kwa jaribio la Rais Barack Obama kuurekebisha mfumo mzima wa afya.
Maseneta waliunga mkono muswada huo kwa kura 14 dhidi ya tisa zilizopinga, huku mjumbe mmoja wa Republican akiungana na upande wa Democrats katika Kamati ya Senate ya Fedha kwa kura ya kuafiki.

Senator Olympia Snowe amekuwa mjumbe wa kwanza kutoka chama cha Republican kuunga mkono mapendekezo ya muswada huo.

Mageuzi hayo yanakusudia kupunguza gharama na kufanya watu wamudu bima ya afya, ikiwa ni kipaumbele cha juu cha Bw Obama kwa mambo ya ndani ya nchi.

Akiafiki uamuzi huo wa kamati ya Senate, Rais Obama amesema hiyo ni hatua muhimu.

Ameendelea kusema" Tunakaribia kuufanyia mageuzi mfumo wetu wa afya, lakini bado hatujafika tunapopataka. Sasa sio wakati wa kurudi nyuma, ni wakati wa kwenda mbele zaidi ili mageuzi haya yafanikiwe."

No comments:

Post a Comment