KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, October 26, 2009

Mawaziri wa afya wakutana Ethiopia


Mawaziri wa afya kutoka kote ulimwenguni wako mjini Addis Ababa, Ethiopia, kujadili ni vipi wataweza kuzuia maelfu ya vifo vya kina mama wakati wa uzazi kila mwaka.
Mkutano umedhaminiwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya idadi ya watu ulimwenguni, UNPF.

Nia ni kuzihimiza serikali kufanya juhudi zaidi za kisiasa na kuwekeza zaidi katika kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia ya kupunguza vifo vya kina mama wakati wa uzazi kwa thuluthi mbili, kufikia mwaka 2015.

Dr Yves Bergevin, mratibu wa masuala ya afya ya uzazi kwa kina mama katika shirika hilo, amesema tofauti za jinsia ni chanzo cha tatizo hilo.

No comments:

Post a Comment