KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, October 20, 2009

Afghanistan itafanya uchaguzi wa marudio tarehe 7 mwezi wa Novemba


Afghanistan itafanya uchaguzi wa marudio tarehe 7 mwezi wa Novemba utakaoamua nani atakuwa rais kati ya Hamid Karzai na Abdullah Abdullah.
Taarifa za kufanyika duru ya pili ya uchaguzi zinafuatia chagizo kutoka jumuia ya kimataifa.

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya jopo linaloungwa mkono na Umoja wa Mataifa kusema linaushahidi wa kutosha wa kufanyika udanganyifu katika uchaguzi wa mwezi wa Agosti na kuziporomosha kura za Bw Karzai hadi chini ya asilimia 50.

Bw Karzai ameuambia mkutano wa waandishi wa habari, anakubali matokeo ya uchunguzi huo na akaongeza hiyo ni hatua muhimu kwa demokrasia.

Matokeo ya awali yameonesha Bw Karzai, alipata asilimia 55 ya kura na waziri wake wa zamani wa mambo ya nje Bw Abdullah alipata asilimia 28.

Lakini tume ya uchaguzi inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, iliamuru masanduku kutoka vituo 210 uchaguzi, kura zake zake ni batili.

No comments:

Post a Comment