KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Monday, August 31, 2009
YATIMA KATIKA MSINGI WA NJIA PANDA
YATIMA NI MTU GANI?
YATIMA NI MTU MWENYE UPUNGUFU WA MZAZI AU WAZAZI MAISHANI MWAKE.
ILI BINADAMU AWEZE KUWEPO NA KUTAMBULIKA KATIKA JAMII, LAZIMA AWE NA MAMA NA BABA KATIKA MSINGI WA KUZALIWA NA UKUTA WA MALEZI.
KUNA BAADHI YA WATU AMBAO WALIISHI BILA YA BABA WALA MAMA, NAO NI ADAMU NA HAWA. ADAMU NDIO BINAADAMU WA KWANZA KUUMBWA NA MWENYEZI MUNGU HAPA DUNIANI, NAFSI YAKE MWENYEZI MUNGU ALIIPA ZAWADI YA JINSIA YA KIUME NA HAWA AKAPEWA NAFASI YA PILI KATIKA UMBO LA
BINAADAMU, NAYE MWENYEZI MUNGU AKAMZAWADIA
JINSIA YA KIKE. HUO NDIO ULIOKUWA MWANZO WA MKE NA MME KUISHI NA KUPATA MTOTO AU WATOTO, KUPITIA NJIA YA MBEGU YA UHAI KATIKA MSINGI WA SHERIA YA NDOA NA UKUTA WA TENDO LA NDOA.
BINADAMU MWINGINE AMBAE ALIZALIWA BILA NDOA, TENDO LA NDOA, BABA, SHANGAZI, BAMDOGO AU
BAMKUBWA AU BABU KWA UPANDE WA BABA NI YESU
(NABII ISA).
UKIWATOA ADAMU, HAWA NA YESU, HAKUNA BINADAMU MWINGINE MWENYE UPUNGUFU WA MZAZI, KATIKA MSINGI WA CHANZO (KUZALIWA KUPITIA NJIA YA TENDO LA NDOA) CHAKE CHA MAISHA, WOTE WALIBAKI TUMETOKANA NA
TUNAZIDI KUTOKANA NA NASABA YA BABA NA MAMA.
BIBLIA KATIKA NJIA YA DINI FASI NA KUJALI YATIMA NA WAJANE
DINI SAFI NI IPI ?
DINI ILIYO SAFI, ISIYO NA TAKA MBELE ZA MUNGU BABA NI HII, KWENDA KUWATAZAMA YATIMA NA WAJANE KATIKA DHIKI PASIPO MAWAA.
( WARAKA WA YAKOBO 1 :27)
KWA MUJIBU WA BIBLIA, TUNAONA KWAMBA KILA NJIA INA JINA LAKE. KWAMFANO NJIA YA KUMJUA MWENYEZI MUNGU, INAITWA DINI. NA TUNAONA DINI KUWA NI NJIA YA WATU WENYE IMANI YA KUWEPO KWA MWENYEZI MUNGU, NA HUFANYA MATENDO YAO KATIKA MSINGI WA KUWAPENDA NA KUWA HURUMIA YATIMA. NA NDIO MAANA KATIKA RATIBA YA MAISHANI MWAO(WACHA MUNGU) JAMBO LA KWANZA NI KUMTAMBUA MWENYEZI MUNGU NA KUHAKIKISHA UPENDO WAO JUU YA MWENYEZI MUNGU, KWA KUTENDA MAPENZI YA MUNGU, KAMA KUWATEMBELEA MAYATIMA NA WAJANE.
KUWATEMBELEA YATIMA NA WAJANE, HAKUMANISHI KWAMBA LAZIMA UWE NAHELA AU MALI YA KUWAPA, LA MARANYINGINE WANAHITAJI KUKUONA NA KUZUNGUMZA NAWEWE MAZUNGUMZO YENYE MFUMO WA FARAJA NA MSINGI WA AMANI NA UKUTA WA UTULIVU BAINA YENU.
KILA MWANAMKE MWENYE MSINGI WA NDOA ,ANAWEZA KUWA MJANE BILA KUTEGEMEA NA KILA MTOTO MWENYE WAZAZI ANAWEZA KUWA YATIMA BILA KUTEGEMEA. NDIO MAANA NI JUKUMU LA KILA MWANAUME NA MWANAMKE WENYE MSINGI WA NDOA, WANATAKIWA WATOWE AU WAONESHE NAFASI YAO YA KWANZA KATIKA HARAKATI YA KUWASAIDIA WAJANE.
KWASABABU HAKUNA FAMILIA YENYE MKATABA WA KUEPUKA UJANE AU UYATIMA NDANI YAKE.
IKIWA HUTAKI KUWASAIDIA WATOTO WA YATIMA, KUMBUKA KWAMBA KESHO NA KESHO KUTWA UNAWEZA KUONDOKA (KUFA) NA UKAACHA MJANE AU WAJANE NA MZIGO WA WATOTO WA YATIMA DUNIANI.
IKIWA MLIKUWA BABA NA MAMA WENYE KUWAPENDA MAYATIMA NA KUWAJALI KATIKA MSINGI WA HISIA ZAO, MWENYEZI MUNGU ATAFANYA WAJANE AU MJANE WAKO KUNUSURIKA NA MATESO YA WANAWAKE NA WANAUME WASIO WAJALI WAJANE, HAPA DUNIANI.
NA IKIWA UMEACHA AU MMEACHA WATOTO WA YATIMA KATIKA MFUMO MZURI WA KUPENDA NA KUPENDWA KATIKA JAMII YA MAYATIMA, BASI ULINZI WA WATOTO WAKO, UTAKUWA NI MZURI NA WENYE ULINZI KATIKA JAMII.
NA MWENYEZI MUNGU ATAWANUSURU WATOTO WENU AU WAKO, KWASABABU NA WEWE AU NYINYI (BABA NA MAMA ) MLIWEZA KULINDA NA KUTETEA MASLAHI YA WATOTO YATIMA, BINDI MLIPOKUWA HAI.
TENDA MEMA NENDA ZAKO WENGI HUONA KAMA MANENO HAYO NI HADITHI, LAKINI MATENDO HAYO NI NUSRA JUU YA MTENDAJI NA NI AFYA YENYE MSINGI WA KUMBUKUMBU BORA KWA MPOKEAJI.
KUMBUKA YA KWAMBA KISASI KINALIPWA KWA MABAYA NA WEMA HULIPWA JUU YA MAZURI. IKIWA ULIMTENDEA MTU JAMBO ZURI, ATAKUOMBEA KWA MUNGU AKUPE BARAKA NA UTENDEWE MAZURI. HATA KAMA ULIMSAIDIA MTOTO YATIMA, ATAKUOMBEA BARAKA NA MAZURI KWA MWENYEZI MUNGU, KISHA UTAPATA ULINZI WA MUNGU, NA SIKU AMBAYO UTAKUWA NA MZIGO WA YATIMA KATIKA FAMILIA YAKO, BASI MWENYEZI MUNGU ATAKULIPA KUTOKANA NA ULE MSINGI BORA WA KUTENDEA MAZURI YATIMA , KWA HIVYO NAWE YATIMA WAKO WATALIPWA JUU YAYALE ULIYOYATANGULIZA MIKONO YAKO
(WEMA JUU YA YATIMA).
QURANI INASEMAJE ! KUHUSU YATIMA ?
MWENYEZI MUNGU ANASEMA HIVI » WALA MSIKARIBIE (MSIYAGUSE) MALI YA YATIMA, ISIPOKUWA KWA NJIA ILIYOBORA (KWA HAO MAYATIMA) MPAKA AFIKE BALEGHE YAKE(HUYO YATIMA AKABIDHIWE MWENYEWE). NA TIMIZENI AHADI, KWA HAKIKA AHADI ITAULIZWA «
(SIKU YA KIAMA)
(17 : 34)
KWA MUJIBU WA QURANI, TUNAONA KWAMBA KUNA WATU WENYE KUTUMIA MALI ZA WATOTO YATIMA, NA NDIO MAANA MWENYEZI MUNGU ALITOA TAHADHARI, JUU YAMATUMIZI MABAYA YA MALI ZA WATOTO YATIMA. KUNA WATU WENYE KUTUMIA VIFO AU KIFO CHA MZAZI KAMA MTAJI(DILI). BABA ANAPOKUFA, NDUGU AU WAZAZI WA MAREHEMU, HUANZA VIKAO VYA KUMNYANYASA MJANE ALIOACHWA NA MAREHEMU NA MARANYINGINE KUMDHULUMU HAKI YAKE YA MSINGI KATIKA MALI YA MUMEWE. KINACHOTOKEA NI UKOO HUSIKA KUMTIMUA MJANE YULE NA KUMNYANGANYA WATOTO, KATIKA MSINGI WA KUBAKI NA UTETEZI WA DHULMA YA MALI YA BABA YAO. KITENDO HICHO NI KITENDO AMBACHO NI KIBAYA NA HUTENGENEZA UHASABA BAINA YA MKE NA BABA, MAMA MKWE, MASHEMEJI, MAWIFI, WAJOMBA NA KUTENGANISHA UHUSIANO WA NDOA
(MKATABA WA MUUNGANO WA KOO MBILI).
MWANAMKE ANAPOTIMLIWA NA NDUGU WA MMEWE ATAJIKUTA AKIHANGAIKIA MAISHA YAKE NA AKIHANGAIKA KATIKA MSINGI WA KUKOSA MME, NA KUHANGAIKA KATIKA UKUTA WAKUKOSA MALEZI YA WANAE NA KUHANGAIKA KATIKA MLANGO WA KUDHULUMIWA MALI YAKE.
SI RAHISI KWA MWANAMKE HUYO, KUWA NA AKILI TIMAMU KATIKA JAMII. HUJIKUTA KATIKA HALI YA KUCHANGANYWA NA MZONGO WA MAWAZO NA KWA UPANDE MWINGINE MZIGO WA MATENDO YA KUTAFUTA RIZIKI. HALI HII, IMETENGENEZWA NA WATU AMBAO TAYARI WALIUNGANISHA NDOA (MUUNGANO WA KOO) HUSIKA, KATIKA MSINGI WA KICHEKO NA FURAHA, NA WAMEVUNJA MKATABA HUSIKA KATIKA CHUKI NA MAUMIVU YA KILA UPANDE, NA MWISHO WAKE WAKIPORA HAKI YA VIUNGO KATIKA VIUNGO VYA FAMILIA HUSIKA, NA KISHA WA KIONDOA UPENDO NA AMANI NA UTULIVU BAINA YA WATU HUSIKA KATIKA KOO HUSIKA.
KWA UPANDE WA WATOTO!!!!!!?
LICHA YA WATOTO, KUJIKUTA KATIKA JIA PANDA, KWA KUMPOTEZA BABA, KATIKA NJIA YA KIFO NA KUPOTEZA MAPENZI NA MALEZI YA MAMA KATIKA MAISHA YAO YA MAPITO, WATAJIKUTA WAKIWA NA UPUNGUFU WA AKILI(YAANI WATOTO WA YATIMA KATIKA HALI HII, HUJIKUTA WAKICHANGANYIKIWA KWA MZIGO WA MAWAZO NA VISHINDO VYA MAAMUZI KATIKA MSINGI WA MATENDO), KUTOKANA NA KUFIKIRI KIFO CHA BABA NA KUFIKIRI MTENGANO WAO NA MAMA MZAZI NA KUFIKIRI UPORAJI MALI ULIOTENDWA NA BABU, BIBI, BABA MKUBWA AU MDOGO, SHANGAZI……..KATIKA UKOO WAO.
KWA KWELI NJIA HII NI MBAYA NA NIJAMBO LA KUSIKITISHA KATIKA JAMII. WATU WENYE UPUNGUFU WA ELIMU JUU YA WATOTO YATIMA, WANAWEZA KUFIKIRI VIBAYA KUHUSU, UTENDAJI WAO WA KAZI NA MCHANGO WA MAONI YAO KATIKA JAMII. MTOTO YATIMA NA MTOTO MWENYE WAZAZI , KWANZA FIKIRA ZAO NI TOFAUTI. UTOFAUTI UNATOKANA NA MSAADA WA MAWAZO UNAOTOKANA NA BABA AU MAMA MAISHANI MWETU. UKOSEFU WA BABA AU MAMA, KIDOGO UNAWEZA KUTINGISHA KICHWA CHA YATIMA HUSIKA KWA MDA MFUPI KISHA AKAWEZA KURUDI KATIKA HALI YA KAWAIDA KIMATENDO NA KIFIKIRA. LAKINI UKOSEFU WA WAZAZI WOTE NI PIGO KUBWA, KAMA UGONJWA WA UKOMA KATIKA MOYO WA YATIMA HUSIKA. BABA NA MAMA, KILA MMOJA ANA UMUHIMU WAKE KATIKA MCHANGO WA MAWAZO NA MATENDO FULANI JUU YA WATOTO AU MTOTO WAO, BILA KUJALI JINSIA. MSAADA HUO, HUWA NI FARAJA KWA MTOTO HUSIKA, HATA KAMA BABA ATAKUWA NI MWEHU AU MLEVI, LAKINI KWENYE MOYO NA KATIKA JAMII UNAJULIKANA YA KWAMBA UNA MSINGI WA ULINZI, UMUHIMU, NA FAIDA YA KUWA NA BABA, NA KWA UPANDE WA MAMA NDIVYO ILIVYO.
JUU YA YULE MTOTO MWENYE UKOSEFU WA WAZAZI NA KUWA NA MSINGI WA DHULMA YA MALI YA BABA YAKE, HUWA KAMA MTU MWENYE UPUNGUFU AU UKOSEFU WA MAPENZI JUU YA KOO ZOTE MBILI(UPANDE WA BABA NA UPANDE WA MAMA) WOTE HUONEKANA KWAKE KAMA WATU WANAFIKI, WALIOSHINDWA KURUDISHA HAKI YA WAZAZI MKONONI MWAKE, NA MWISHOWE KUNDI FULANI LIKAJILIMBIKIZA MALI ZA WAZAZI WAKE, KATIKA JINA LA KUOKOA MALI ZA NDUGU YAO, BILA KUJALI MBEGU YENYE KUTOKANA NA MGONGO WA NDUGU YAO, HIYO ITAKUWA NI NJIA YA KUJENGWA VITA YA MAWAZO NA MATENDO NA KUONDOA RAHA YA UJOMBA, SHANGAZI, BABA MKUBWA AU MDOGO, MJOMBA, BIBI AU BABU.
MAMBO HAYA YAPO NA TUNAYASHUHUDIA KILA KUKICHA KATIA RUNINGA, MAGAZETI ……..N.K.
UKIMWONA MTOTO YATIMA AMEKAA MWENYEWE JUWA YA KWAMBA HANA RAHA MAISHANI MWAKE, WALA USIMKEMEE, ANACHOKIHITAJI NI MATIBABU YENYE MZINGO WA UPUNGUFU WA UPENDO NA KIZINGITI CHA KUPATA HAKI ZENYE UKUTA WA MALEZI BORA NA MLANGO WA ELIMU BORA KATIKA JAMII.
Ndugu kuchukuwa mali ya yatima au yatima katika jina la utunzaji bora
KUNA BAADHI YA NDUGU AMBAO WANAJIVIKA NGOZI YA KONDOO KUMBE NI MBWA MWITU NDANI YA NYOYO ZAO. WATU BHAWA HUTAMBULIKA KWA MANENO MAZURI NA MATENDO YENYE KWENDA KINYUME NA MISEMO YAO, KWA KIFUPI WATU HAO NI WANAFIKI.
UTAWAKUTA WAKICHUKUWA JUKUMU LA KUWALEA WA TOTO YA TIMA KATIKA JINA LA KUWAPA MALEZI BORA NA KUWALINDA KATIKA MSINGI WA HAKI, LAKINI MIOYONI MWAO WANA LENGO LINGINE KABISA.
MALENGO KATIKA MALEZI YAKO AINA KUU TATU
1. LENGO LA KUTUMIA (KUDHULUMU) MALI YA YATIMA HUSIKA.
WATU HAO, HUCHUKUWA JUKUMU LA KUWALEA WATOTO HUSIKA, KATIKA MSINGI BORA WA MALEZI NA KUMBE LENGO LAO KUU NI KUTUMIA MALI ZAO KATIKA MAHITAJI YAO BINAFSI. MLEZI HUTUMIA MALI YA MTOTO YA TIMA BILA RIDHA YAKE WA LA MTOTO KUJUWA. KINACHOFANYIKA, NI KUTUMIA ILE MALI KWA JINA LA KULA WOTE (KUTUMIA MALI YA YATIMA KATIKA MATUMIZI YA FAMILIA HUSIKA AU UKOO HUSIKA, BILA RIDHA YA YATIMA (MMILIKI) HUSIKA KUJUWA, HATA KAMA ATAJUWA ATAJIKUTA HANA UWEZO WA KUZUIA MALI HUSIKA KUTUMIWA. WATU HAWA NI WATU WENYE UPUNGUFU AU UKOSEFU WA HURUMA JUU YA YATIMA. NDIO MAANA UKITAKA KUCHUKUWA YATIMA NA KUMLEA UWE NA UHAKIKA, KUTOKA MOYONI MWAKO KWAMBA UTAKUWA NA ULINZI WA KUMLINDA NA KULINDA MALI YAKE KATIKA JINA LA KWELI. MATOKEO YAKE YULE MTOTO ATAJIKUTA, KATIKJA NJIA PANDA NA KUTESWA PINDI MALI YAKE ITAKAPO KWISHA. MALI YA YATIMA ITAKAPOKWISHA, FAMILIA HUSIKA ITAANZA KUMWONA YULE MTOTO KAMA MTU MWENYE KUFIRISI FAMILIA HUSIKA, NA KITAKACHOTOKEA JUU YA MTOTO HUYO NI KUMTENGENEZEA MBINU ZA KUMWANGAMIZA KIFIKIRA AU KUMFUKUZA BILA JAMII KUTAMBUWA SIRI ILIOKO BAINA YAO(MTOTO YATIMA NA WALEZI).
MBINU ZIKO NYINGI ATAITWA MWIZI, MALAYA, MKOSA ADABU, MTU MNAFIKI, KAMPENDA MMEWANGU, ALITAKA KUMBAKA MKEWANGU AU MWANANGU AU KANIIBIA KIASI FULANI CHA PESA……N.K.
KITAKACHOTOKEA JAMII ITAMWONA MTOTO HUSIKA, HANA ADABU NA ITAOGOPA KUMKARIBISHA MAJUMBANI MWAO. NJIA HII NI NJIA IPO NA INATUMIWA NA KOO NA FAMILIA NYINGI MAISHANI MWETU.
2) LENGO LA KUMCHUKUWA MTOTO YATIMA ILI KUMFANYA MFANYAKAZI AU MTUMWA
KUNA BAADHI YA FAMILIA ZINAZOCHUKUWA WATOTO YATIMA, KWA LENGO LAKUWATUMIA, KAMA WAFANYAKAZI WA NYUMBANI. WATU HAWA HUWA NI WENYE MANENO MAZURI MBELE ZA WATU LAKINI MIOYO YAO INA KUTU KATIKA NJIA YA MALEZI YA WATOTO YATIMA.
KWANZA ANAPOCHUKULIWA MTOTO HUYO, HUWA NI MWENYE KUHISI FURAHA NA FARAJA MOYONI MWAKE(MTOTO YATIMA), LAKINI MATOKEO YAKE HUJIKUTA KATIKA DIMBI LA KINYUMBE CHA FIKIRA. MWANZO HUDHANI KWAMBA MANENO YA MUONGEAJI NIYA KWELI KATIKA UTENDAJI, MARA HUONA MABADILIKO KATIKA MSINGI WA MAUMIVU NA CHUKI JUU YAKE. KILA KAZI NGUMU HUPEWA YEYE, HUWA NI MWENYE KUAMKA WA KWANZA NA KULA NA KULALA HUWA NIWA MWISHO. MAUMIVU HAYA, KWA KWELI NI MAUMIVU YENYE KUMFANYA MTOTO YATIMA AKOSE RAHA YA UTULIVU NA AMANI MAISHANI MWAKE. SI KAZI NGUMU TU HUYO MTOTO ATAPEWA, LA! BALI HUJIKUTA KATIKA KIPIGO NA MATUSI NA MAARANYINGINE MANENO YA KEJERI. HALI HIYO HUMFANYA MTOTO HUSIKA AANZE KUWAZA UMUHIMU, FAIDA NA HASARA YA KUWA NA WAZAZI NA MARANYINGINE HUJIKUTA KATIKA KUPOOZA AU KUKOSEKANA KWA MAPENZI JUU YA WALEZI WAKE.
MLEZI MWENYE ROHO MBAYA KAMA HII, HAWEZI KUMPA MTOTO YATIMA HATA FURSA YA KUPELEKWA SHULENI AU KUJISOMEA. NA ATAKAPO MPELEKA MTOTO HUYO SHULE, BASI ATAMPANGI YA RATIBA YA KAZI ZA NYUMBANI BILA KUJALI MDA WAKE WA KUPUMZIKA AU KUJISOMEA. MWISHO WAKE MTOTO HUYO ATAKUWA NI MWENYE MAWAZO AU MZIGO MKUBWA WA MAWAZO NA ATAJIKUTA AKISHINDWA KUSOMA VIZURI NA MARANYINGINE KUFAULU.
UKIANGALIA WATOTO WENGI WA YATIMA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA KAMA HAYA, WENGI WA MEMALIZA DARASA LA SABA NA WENGINE WAMESHINDWA KUMALIZA ELIMU YA JUU. SIKUSEMA KWAMBA WATOTO HAO WAMEKOSA ADA L! BALI WALICHO KIKOSA NI UHURI AU UKOSEFU WA UTULVU NA AMANI NDANI YA NAFSI ZAO. NA MWISHO WAKE WALEZI HAO WABAYA HUPANDISHA BENDERA NA KUTAMKA KATIKA JAMII, KWAMBA MTOTO AMESHINDIKANA, HATAKI SHULE, NI RAHISI SANA KWA JAMII KUKUBALI MANENO YA MLEZI HUYO MBAYA , KUTOKANA NA KUWA NA MANENO MAZURI NA KUCHUKUWA MAAMUZI YA MATENDO YENYE SIRI YA NDANI YA NAFSI YAKE. MTOTO HUSIKA ATAONEKANA KAMA MTU MWENYE BAHATI LAKINI ANAICHEZEA NA MARANYINGINE ATALAUMIWA NA JAMII KWA KUTOTUMIA NAFASI YAKE YA BAHATI VIZURI. KAMA TUNAVYO JUWA SIRI YA MTUNGI AIJUWAE VIZURI NI KATA YAKE AU SIRI YA NDOA AIJUWAE VIZURI NI BABA NA MAMA AU WENYE NDOA. NDIO MAANA MLEZI HUYO HUTUMIA NGUVU YAKE YA MANENO KUANGAMIZA UTU NA NAFASI YA MALEZI NA ELIMU BORA YA MTOTO HUSIKA, KATIKA JINA LA WEMA. HAKUNA WEMA WENYE MATESO, WEMA WENYE MATESO MWISHO WAKE NI KISASI. NA TUNAJUWA YA KWAMBA KISASI NI MALIPO YA UBAYA WA NAFSI. IKIWA UMEAMUWA KUTENDA WEMA, BASI KUWA MFANO MZURI WA KUTENDA ULICHO KINENA NA UWE MVUMILIVU KATIKA UENDESHAJI, KWASABABU HAKUNA BINADAMU MWENYE UKOSEFU WA KASORO, HATA WEWE UNAKOSEA.
USITOWE VISINGIZIO VYA UONGO KWASABABU, MWENYE MPINI NI WEWE LEO KWAKO KESHO KWAKE, SIJUI ITAKUWAJE MKIKUMBANA NA ULIEMTESA KATIKA MSINGI WA KUHITAJI MSAADA WAKE. TENDA WEMA NENDA ZAKO NA IKIWA HUWEZI, USIJIPE JUKUMU HILO KWASABABU HULIWEZI. IKIWA NI MFANYAKAZI MTAFUTE KWA JINA LA AJIRA SIO KWAJINA LA MALEZI BORA.
3) KUANGAMIZA ELIMU NA UWEZO WA YATIMA.
KUNA BAADHI YA WATU KATIKA UKOO AU KOO, WAO HUWA NA ROHO ZENYE MSINGI WA CHUKI, WIVU, FITINA, LAWAMA, LAANA…… JUU YAKILA MTU AU FAMILIA YENYE MAFANIKIO KATIKA MFUMO WA MALI, PESA, ELIMU, CHEO, HESHIMA…………N.K.
WATU HAO NI WABAYA, WALA SIOWATU WAKUPEWA MTOTO WA YATIMA KWALENGO LA KUMLEA, KWASABABU HAWANA, MOYO WA MSAADA, BALI WANAHITAJI KILA JAMBO ZURI LIWE LA KWAO, BILA KUJALI UMUHIMU, FAIDA NA HASARA VYA JAMBO HUSIKA.
MTU HUYO, HUWA NA KAULI NZURI KATIKA UKOO AU FAMILIA HUSIKA. HUWA NI MTU MWENYE MAZUNGUMZO MAZURI YA ULIMI NA MSINGI WENYE TOFAUTI, KATIKA MATENDO YAKE.
KUNA BAADHI YA FAMILIA AMBAZO HUAMINI KWAMBA, NDIZO ZENYE KUSTAHIKI HESHIMA YA MALI, PESA, ELIMU, CHEO……N.K, WATU HAO, HUWA NI MARACHACHE KUWA NA MOYO WAKUWEZA KUSAIDIA, BAADHI YA WANACHAMA WA UKOO WAO, ILI WAWEZE KUPATA, ELIMU, MALI, PESA, CHEO, HESHIMA…….N.K, KUTOKANA NA NYOYO ZAO KUJAWA NA WIVU, FITINA, LAWAMA, HUSUDA, LAANA, CHUKI……..N.K.
WATU HAWA WATAKAPOMCHGUKUWA MTOTO WA YATIMA, ATAKUWA NI MWENYE KUFURAHI NA MWENYE KUHISI KUPATA NAFUU MAISHANI MWAKE. LAKINI MATOKEO YAKE MTOTO HUYO WA YATIMA ATAJIKUTA KATIKA, ULINZI WA MALI NA MARANYINGINE KUPEWA MAJUKUMU YA KIBIASHARA. MTOTO WA YATIMA ANAPOPEWA BIASHARA, HUJIHISI KUWA NA NAFUU KUBWA MAISHANI MWAKE, KWASABABU ATAHISI KWAMBA TAYARI ANA UHAKIKA WA KUISHI BILA TAABU, LICHA YA WAZAZI WAKE KUFARIKI. ITAKUWA NGUMU JUU YA MTOTO HUYO YATIMA, KUGUNDUWA KWAMBA NI MCHEZO WA KUMWANGAMIZA KIELIMU NA KIMAFANIKIO ZAIDI, BALI ATAONA HAKUNA FAMILIA YENYE MAPENZI YA MAANA KAMA HIYO, AMBAYO IMEWEZA KUMPA AJIRA NA KUMPA NAFASI YA TWISHENI.
BINAADAMU WANA MBINU NYINGI ZA KUANGAMIZA ELIMU NA HESHIMA YA MTU, NA HUJUWA VIZURI YA KWAMBA UKIMWANZISHIA BINAADAMU MAISHA MAZURI NA YENYE KIPATO, ATAKUWA RADHI KUACHA HATA SHULE, KUMBUKA YA KWAMBA HUYO MTOTO HANA WAZAZI WA KUMSHAURI, NA WALE NDUGU WALIOBAKI HAWAWEZI KUMKEMEA AU KUMKEMEA MLEZI WAKE, KWASABABU ASILIMIA KUBWA YA UKOO, HUPELEKA PALE(KWA MLEZI MWENYE MALI, PESA, CHEO……N.K) MALALAMIKO YAO YA NJAA NA SHIDA NYINGINE NDOGO NDOGO, HUMUONA HUYO MLEZI NI MKOMBOZI WA UKOO HUSIKA, NA WENGI KATIKA UKOO HUSIKA , WANATAJA TABIA ZAKE MBAYA KWA KUJIFICHA (KWA SIRI) NA YULE MWENYE KUTHUBUTU, KUULIZA KUHUSU HAKI YENYE MSINGI BORA WA FAHAMU (HAKI YA ELIMU) NA KUHOJI KUFANYA BIASHARA VYA YULE MTOTO WA YATIMA, KABLA HAJAFIKIA UMRI AU KUWA NA UWEZO THABITI WA KUKABILIANA NA AJIRA HUSIKA.
ATAKUMBANA NA UPINZANI WA CHUKI, VITISHO VYA KUSITISHA MISASADA(CHAKULA,CHUMVI, 5000 AU 2000 ELF, NGUO, MCHANGO WA HARUSI YA MWANAE, SALAMU YA TAJIRI…..N.K).
NJIA HII, YAKUMPA MTOTO YATIMA NAFASI YA KIBIASHARA, KABLA HAJAFUDHU(KUMALIZA) MASOMO YENYE MSINGI WA ELIMU YA CHINI, KATI NA YA JUU KABISA, NI NJIA YA KUANGAMIZA ELIMU YA UTAMBUZI WA MENGI MAISHANI, UTAJIRI WA AJIRA BORA KATIKA MASHIRIKA MBALIMBALI, HESHIMA YA CHEO CHENYE KUHITAJI ELIMU FULANI……………………….N.K.
• FAMILIA YENYE TABIA HII, MARANYINGI UNAKUTA NIYENYE WAPENZI WACHACHE KATIKA UKOO HUSIKA. VILEVILE FAMILIA HII, HUWA NIYENYE UBAGUZI BAINA YA MATAJIRI NA MASIKINI, NA BAINA YA WATU WENYE ELIMU KUBWA NA MASIKINI WA ELIMU.
• FAMILIA HII HUWA NIYENYE KUHAKIKISHA KWAMBA INAANGAMIZA, KILA MTU MWENYE KUTAKA KUCHIPUWA NDANI YA UKOO, AKIWA NA MSINGI WA UTUKUFU WA ELKIMU NA MSINGI WA KUTENGENEZA MAZINGIRA YA AJIRA BORA, KATIKA JAMII.
MTAZAMO WA JAMII JUU YA YATIMA UKOJE?
KWANZA JAMII, IMEJIKUTA KATIKA MTIHANI MGUMU, WA MATUMIZI YA DARUBINI YAKE JUU YA WATOTO YATIMA.
HAKUNA MTU MWENYE UWEZO WA KUEPUKA UYATIMA AU KUKOSA YATIMA KATIKA UKOO WAKE. JAMBO HILI LAZIMA LIWE ALAMA YENYE KUBEBA ELIMU YA MSAADA JUU YA
WATOTO WA YATIMA.
LAKINI JAMBO LA KUSHANGAZA KATIKA JAMII, NI KUWA MSINGI WA MATUNZO BORA YA WATOTO WA YATIMA, UMEACHIWA WAFADHILI WA KIGENI NA MARANYINGINE, JUKUMU HILO LIMEELEKEZWA KATIKA VITUO VYA MALEZI.
BAADHI YA WATU KATIKA JAMII WANAJITOLEA MALI, PESA, ELIMU NA MDA, KATIKA HARAKATI YA KUWASAIDIA WATOTO HAO WA YATIMA.
KUNA WATU WENGINE AMBAO, HUCHUKUWA MTOTO AU WATOTO WA YATIMA NA KUCHUKUWA JUKUMU LENYE MSINGI WA MALEZI BORA NA UKUTA WA AMANI NA UTULIVU.
NA KUNA BAADHI YA WATU, AMBAO HUONA JUKUMU LA KUMLEA MTOTO WA NDUGU, JAMAA NA RAFIKI KUWA NI KERO. NA MARANYINGINE NDUGU (BABA MDOGOAU MKUBWA, SHANGAZI, WAJOMBA, WAKE ZAO AU WAUME WAO………N.K) HUCHUKUWA KASORO YA MAREHEMU(BABA AU MAMA) NA KUZIFANYA SABABU YA KUCHUKIA WATOTO HUSIKA.
NA MARANYINGINE WATOTO YATIMA HUJIKUTA KATIKA NJIA PANDA, PALE WANAPOKABILIWA NA WAKATI MGUMU WA KIFO CHA MAMA. MAMA MZAZI NI KIUNGO CHENYE MSINGI WA MALEZI BORA NA UKUTA WA HURUMA JUU YA MWANAE. NDIO MAANA MARANYINGI, KIFO CHA MAMA MZAZI KINAUMIZA SANA ZAIDI YA KIFO CHA BABA MZAZI.
ASILIMIA KUBWA SANA YA WATOTO WA MTAANI, AMBAO NI YATIMA, WAMEFIWA NA MAMAZAO. SABABU KUBWA INAJITOKEZA ,KUTOKA KWA UPANDE WA BABA.
MAMA MZAZI ANAPOKUFA(KUONDOKWA NA ROHO), ASILIMIA KUBWA YA MAISHA YA MTOTO AU WATOTO WAKE, INATETEMEKA KWA KISHINDO KIKUBWA. MTOTO HUWA NI MWENYE KUPOTEZA MSINGI WA HURUMA NA UKUTA WA MWONGOZO KUTOKA KWA MZAZI WAKE WA KIKE(MAMA). NA NDIO MAANA MARANYINGI UTAMKUTA AU UTAWAKUTA WATOTO YATIMA, WAKIPENDA KUKAA,SEHEMU TULIVU NA MARANYINGINE WAKILIA.
MACHOZI YA MTOTO YATIMA YANATOKANA NA MACHUNGU YA NAFSI YAKE. MACHUNGU YA NAFSI YANATOKANA NA UPUNGUFU AU UKOSEFU WA MSINGI BORA WA MALEZI NA NGUZO YA HURUMA JUU YAO (WATOTO YATIMA).
KIFO CHA MAMA NIMSIBA MKUBWA JUU YA YATIMA HUSIKA, KWASABABU, MAMA ANAPOKUFA NIRAHISI SANA MWANAUME, KUOA MWANAMKE MWINGINE NA KUMSAHAU YULE ALIYETANGULIA MBELE YA HAKI
(KILA NAFSI LAZIMA ITAKUFA).
BAADHI YA WANAUME HUJIKUTA WA KIKUMBWA NA MAJUKUMU MENGI YA KUTAFUTA RIZIKI, NA MARANYINGINE WAKIJIKUTA WA KITOA MAJUKUMU YAO YA NYUMBANI, KAFARA KWA WAKE ZAO AU WALEZI.
KWANINI TUNASEMA MWANAUME ANATOA MAJUKUMU YAKE YA NYUMBANI KAFARA ?
KWASABABU NI MDA MFUPI SANA, MWANAUME
(BABA MWENYE FAMILIA), ANAOWEZA KUUTUMIA NYUMBANI MWAKE NA AKAUTUMIA KATIKA MSINGI WA KUONGOZA NA KUPATANISHA FAMILIA YAKE, KATIKA UKUTA WA HAKI. UTAMKUTA MTOTO ANA MATATIZO NA MAMA YAKE WA KAMBO, LAKINI NJIA INAYOTUMIKA KUTENGENEZA, KUENDESHA NA KUTATUWA TATIZO HUSIKA, HALIMUHUSU BABA MWENYE FAMILIA. UTAKUTA WATU WENYE MATATIZO, NDIO BABA ANAWAACHIA JUKUMU LA KUMALIZA TATIZO HUSIKA.
KUMBUKA KWAMBA MTOTO SIKU ZOTE NI MTOTO, LAKINI MKE ANA NAFASI YAKE NZURI NA YENYE CHEO CHAKUMWEZESHA KUFICHA, KUANGAMIZA NA KUMFUTA MTOTO YATIMA NDANI YA NYUMBA HUSIKA, BILA KUJALI YA KWAMBA NYUMBA HIYO ILIJENGWA KWA USHIRIKIANO WA MAREHEMU MAMA YAKE NA BABA YAKE.
KWA MTAZAMO WA HARAKA, LAZIMA TUJIULIZE KUHUSU CHANZO CHA MAPAMBANO BAINA YA WATOTO YATIMA NA MAMA WA KAMBO !!!!?
KWANZA KIFO CHA MWANAMKE, KINAMSTUWA MME WAKE, KUTOKANA NA MAZINGIRA YA MAISHA. LAKINI KIFO CHA CHA MAMA (MAMA WA FAMILIA) HUWA NI ALAMA YA MSIBA NA YENYE KUATHIRI KWA KIASI FULANI FIKRA(MTAZAMO) YA YATIMA HUSIKA KWA MDA FULANI.
SASA UHARAKA WA BABA KUOA, UNAWEZA UKAATHIRI WATOTO WAKE, IKIWA HAJAWAWEKA, KATIKA HALI YA MAANDALIZI YA KUISHI NA MAMA WA KAMBO. BABA ANATAKIWA KWANZA KUWAFARIJI WATOTO WAKE KATIKA MSINGI WA HURUMA NA MALEZI BORA NA PILI KUWAPA MAANDALIZI KATIKA MSINGI WA FURSA YA UHURU WA KUTOA MAONI NA KUPEWA MAJIBU, BILA UKUTA WA KHOFU NA UBABE.
TATU BABA LAZIMA ANAPOMUOA MWANAMKE WA PILI NA AKIWA NA WATOTO YATIMA(YATIMA KWA UPANDE WA MAMA), LAZIMA AWE MUAZI BAINA YA MKE MPYA NA WATOTO WAKE.
NA LINAPOTOKEA TATIZO BAINA YAO, BASI AWE NIMWENYE KUSIKILIZA KILA UPANDE NA KUJENGA MSINGI WA UTULIVU NA UKUTA WA HAKI BAINA YA NYOYO ZOTE ZENYE CHUKI AU KUTAFAUTIANA KIMANENO NA MATENDO.
KUMBUKA YA KWAMBA HAKUNA MTU ALIYEKAMILIKA MAISHANI MWAKE, WATU TUNACHUKIA NA KUPENDA. NA KILA UPENDO AU CHUKI, NI LAZIMA KILA KIMOJA KIWE NA SABABU.
NYOYO ZIMEUMBWA KWA KUCHUKIA WALE WENYE KUZICHUKIA NA KUWAPENDA WALE WENYE KUZIPENDA.
NDIO MAANA TATIZO LA NDANI YA NYUMBA, BAINA YA MAMA WA KAMBO NA WATOTO YA TIMA, LINAWEZA KUTOKANA NA MATENDO NA MANENO YENYE UKOSEFU AU UPUNGUFU WA MSINGI WA UPOLE NA UPENDO.
SIKU ZOTE VURU HUANZISHWA NA UPUNGUFU AU UKOSEFU WA HAKI, BAINA YA NAFSI (UKOO, FAMILIA,NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI) HUSIKA, KATIKA MZOZO HUSIKA.
NA UTAKUTA MAMA WAKAMBO, MARANYINGINE HAJALI, MAUMIVU (HISIA ZA WALE WATOTO WA YATIMA) YA WALE WATOTO, NA KUTUMIA MANENO NA AMRI ZA KIBABE NA MARANYINGINE AKIWAPA ADHABU YA KIPIGO CHA MAANA NA MARANYINGINE AKIWAPIGA KIPIGO CHENYE MSINGI WA NJAA NA KIU NA MAVAZI DUNI NA MARANYINGINE WAKINYIMWA HAKI YA ELIMU. HII INAWEZA KUWA NJIA MOJA WAPO YA KUJENGA MAZINGIRA YA CHUKI NA VITA NDANI YA NYUMBA AU FAMILIA HUSIKA.
BABA SIRAHISI KUJUWA HISIA NA MAUMIVU YA MTOTO AU WATOTO WAKE, KUTOKANA NA KUWA NA MDA MFUPI SANA WA KUKAA NYUMBANI, MARANYINGINE MWANAMKE ANAWEZA KUFICHA SIRI YA MAPAMBANO BAINA YAKE NA WATOTO NDANI YA NYUMBA, KWA KUPITIA NJIA YA KUMDHIBITI MME WAKE KATIKA MDA WA KUWEPO NYUMBANI. MWANAMKE ANAWEZA KUMSHAWISHI MME WAKE KUANGALIA MUVI(PICHA) FULANI AU KWENDA KUMTEMBELEA FULANI AU KUMDHIBITIA MUME WAKE CHUMBANI, ILIMRADI ASIMPE NAFASI YA KUKAA NA KUANZA KUJADILIANA NA WATOTO WAKE, KUHUSU HISIA NA MTAZAMO WA MAISHA YAO.
HIZO NI BAADHI YA NJIA AMBAZO BAADHI YA WANAWAKE WANAZITUMIA, KATIKA KUFICHA MAKUCHA YAO.SIKU ZOTE MWANAMKE ANAPOTAKA KUANGAMIZA AU KUTENGENEZA CHUKI BAINA YA MUME NA BABA, MAMA, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI, LAZIMA KWANZA AJUWE UDHAIFU WA MUME, ILI AWEZE KUPATA NAFASI NZURI YA KUMDHIBITI BILA KUFURUKUTA. KWA UPNDE WA MIKAKATI YA MWANAMKE MWENYE MOYO WA UPUNGUFU WA UPENDO JUU YA UKOO WA MWANAUME, ANAPOKUWA NAMPANGO WAKE, WAKULIPUWA (KUWAFANYIA UBAYA AU KUWAFUTA KATIKA DAFTARI LA UPENDO LA MME WAKE NA KULIANDIKA KATIKA DAFTARI LA CHUKI LA FAMILIA NZIMA NA KUPIGA MUHURI WA VURUGU KATIKA UKOO AU KOO HUSIKA. KIUNGANISHI CHA KOO HUSIKA NI NDOA, NA KASORO YA NDOA NDIO KASORO YA FAMILIA HUSIKA. KASORO YA FAMILIA INAKUWA NI KASORO YA MUUNGANO WOTE WA KOO HUSIKA.
KWA KIFUPI WANA WAKE, NI VIUMBE WENYE HURUMA SANA. LAKINI LINAPOFIKIA SWALA LA KUMLEA MTOTO WA MWENZIWE, PANATOKEA MSHIKEMSHIKE YA AJABU NA KUANZA KUJIJENGEA MAZINGIRA YA CHUKI JUU YA WATOTO WA MME WAKE NA MARANYINGINE AKITENGENEZA SUMU, YA KUWAFUNDISHA WANAE( WATOTO WAKE MAMA WA KAMBO), JINSI YA KUWAKANDAMIZA NA KUWADHARAU WATOTO WA MMEWE.
HUO SIO UNGWANA KWA MWANAMKE MWENYE AKILI NA KUAMINI KWAMBA NA YEYE ANAWEZA KUACHA YATIMA, NA WAKAKABILIANA (WATOTO WAKE BAADA YA KIFO CHAKE) NA MATESO AMBAYO AMEWAPA WATOTO WA MKE MWENZA.
QURAN:
NABII MUHAMMAD (S.A.W)ALIKUWA YATIMA
MWNYEZI MUNGU ANASEMA
“NAAPA KWA MCHANA.
NA KWA USIKU UNAPOTANDA.
HAKUKUKUACHA MOLA WAKO WALA HAKUKASIRIKA
(NAWE EWE NABII MUHAMMAD).
NA BILA SHAKA (KILA) WAKATIA UJAO (UTAKUWA) NI BORA KWAKO KULIKO ULIOTANGULIA.
NA MOLA WAKO ATAKUPA MPAKA URIDHIKE.
JE! HAKUKUKUTA YATIMA AKAKUPA MAKAZI (MAZURI YA KUKAA)?
NA AKAKUKUTA FAKIRI AKAKUTAJIRISHA?
BASI USIMUONEE YATIMA.
WALA USIMKARIPIE AULIZAYE.
NA NEEME YA MOLA WAKO ISIMULIE (KWA KUMSHUKURU NA KWA KUFANYA AMALI NJEMA)”.
(SURATUDH DHUHAA)
NDIO MAANA ASILIMIA KUBWA DUNIANI YA WATOTO WA MTAANI, IMETOKANA NA VIFO VYA UPANDE WA WAKINA MAMA. NA ASILIMIA KUBWA DUNIANI YA WATOTO WA VITUONI NA MARABARANI, NA WENGINE KAMA MAKAHABA, MAISHA MABAYA NA MAGUMU YA WATOTO WA KIKE DUNIANI, ASILIMIA KUBWA YA MAMBO HAYO YAMETENGENEZWA NA KIWANDA CHA MAMA WA KAMBO KATIKA MSINGI WA UPUNGUFU AU UKOSEFU WA HURUMA MAJUMBANI MWAO.
HATUMAANISHI KWAMBA HAKUNA MAMA WA KAMBO WENYE MSINGI WA MALEZI BORA NA UKUTA WA HURUMA NA NGUZO YA ELIMU !! LA !! BALI NI WACHACHE NA WAWE NI WACHA MUNGU WA KWELI. MWANAMKE MCHA MUNGU HUWA NA MOYO WA HURUMA NA MSINGI WA MAISHA YAKE NI UVUMILIVU. MWANAMKE MCHA MUNGU HUWA NI MWENYE KUVUMILIA KATIKA MSINGI WA MANENO NA MATENDO NA HUWA MWEPESI KUSAMEHE NA KUOMBA MSAMAHA BILA KUJALI UMRI AU CHEO.
UTULIVU WA MAPENZI WA MAMA WA KAMBO NDIO MSINGI WA UTULIVU NA AMANI JUU YA MTOTO AU WATOTO YATIMA NDANI YA NYUMBA HUSIKA.
***MCHANGO WA UKOO KATIKA MALEZI YA WATOTO AMBAO WAMEACHWA NA NDUGU ZAO, KATIKA MAZINGIRA YA UYATIMA.************************** NI NINI ?
LAZIMA KWANZA TUJUWE NI NINI MAANA YA UKOO ?
UKOO NI MUUNGANO WA NAFSI NYINGI ZENYE UHUSIANO WA DAMU. BABA NA MAMA NDIO MSINGI WA KUANZISHA UKOO BORA AU UKOO MBAYA. KWA UPANDE MWINGINE UKOO NI MUUNGANO WA FAMILIA NYINGI. KUNA WATALAMU WENYE KUJUWA MAMBO HAYO YA KOO, SISI SIO WATALAMU WA NASABA.
SIKUZOTE, KILA BINADAMU ANAPENDA KUISHI KATIKA MAZINGIRA MAZURI NA KUISHI KATIKA JENGO LA AMANI NA UTULIVU MAISHANI MWAKE.
NI VYEMA NA NI MUHIMU, JUU YA KILA MZAZI KUAMINI KWAMBA YEYE NI MSINGI WA ULINZI NA UKUTA WA AMANI NA NGUZO YA UTULIVU JUU YA FAMILIA YAKE.
MALEZI NA MAELEKEZO BORA YA WAZAZI YANATOA FURSA YA UPENDO BAINA YA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI, KUWAPENDA WATOTO HUSIKA NA WATOTO KUWAPENDA NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI.
UBOVU WA FAMILIA UNATOKANA NA NGUZO ZA FAMILIA. NGUZO ZA FAMILIA NI MME NA MKE. IKWA MWANAUME AMEMUOA MWANAMKE KWA KUTUMIA VIGEZO VYA KIMAHABA, BASI MKEWE ATAMUENDESHA KATIKA NJIA YA KIMAHABA. NA IKIWA MWANAUME ALIMUOA MWANAMKE KWA LENGO LA UBORA WA TABIA NJEMA KATIKA MATENDO NA MAONGEZI, BASI FAMILIA YAO ITAKUWA HODARI KATIKA KUONGEA NA KUKAMILISHA MAONGEZI KATIKA MSINGI WA MATENDO BORA.
KUMBUKA SIFA YA FAMILIA INATOKANA NA MATENDO NA MANENO YAKE, KATIKA JAMII.
NA KUMBUKA KWAMBA FAMILIA NDIO ALAMA YA KUONESHA HESHIMA YA KOO ZAKE. IKIWA MWANAMKE NI MBOVU TAYARI ANALETA DOA JUU YA FAMILIA YAKE NA UKOO WAKE, NA KWA UPANDE WA MWANAUME NDIVYO ILIVYO. FAMILIA BORA NI ILE YENYE KUSIFIWA NA KILA JIRANI YAKE NA KUPAMBWA AU KUSIFIWA NA WAGENI WANAOTEMBELEA NYUMBA HUSIKA.
IKIWA MSINGI WA UKOO HUSIKA, UNA BARABARA NJEMA YA AMANI, UPENDO, UTULIVU NA ELIMU YA KUTOSHA KUHUSU MAZINGIRA YA DUNIA, NIRAHISI SANA, KULINDA NA KUTETEA HAKI ZA WATOTO WAO WA YATIMA.
WATOTO YATIMA WANAWEZA KUSALIMIKA, NA KUISHI KATIKA MAZINGIRA MAZURI, PALE AMBAPO, KOO ZAO(UKOO WA UPANDE WA BABA NA UPANDE WA MAMA) ZINASHIRIKIANA KATIKA MSINGI WA UPENDO. KUMBUKA YA KWAMBA UPENDO HAUPATIKANI PASINA HURUMA. NA KUMBUKA HURUMA MSINGI WAKE NI UVUMILIVU NA UVUMILIVU UKUTA WAKE NI AMANI NA UWANJA WA AMANI NI UTULIVU.
UTULIVU UNAPOKUWEPO KATIKA KOO, LAZIMA KILA NAFSI ITAKUWA YA KWANZA KUSONONEKA, KWANZA KWA KUMPOTEZA NDUGU MPENDWA NA PILI KWA KUHURUMIA WATOTO AU MTOTO ALIYEBAKI KATIKA MAZINGIRA YENYE KUHITAJI MUONGOZO WA MAMA AU BABA MAISHANI.
UKOO WENYE UPENDO UTAFANYA KIKAO, NA KUCHUKUWA MAAMUZI YENYE MAZINGIRA MAZURI YA KUHAKIKISHA KWAMBA HUYO MTOTO YATIMA, ATAISHI KATIKA MAZINGIRA YA UPENDO, ULINZI, AMANI NA KUPATA HAKI YA ELIMU NA HAKI YA KUTOA MAONI NA KUPEWA MAJIBU YENYE MSINGI WA UFAHAMU BORA KATIKA UKOO AU KOO HUSIKA(YANI MTOTO WA YATIMA KUPEWA FURSA YA KUPANZA SAUTI KATIKA KOO ZOTE MBILI).
JE ! KOO ZOTE MBILI ZINAWAJIBIKA AU ZINAWEZA KUWAJIBIKA KATIKA MALEZI BORA YA YATIMA ?
NI NINI MAANA YA KOO ZOTE MBILI ?
MFUMO WA NDOA, MARANYINGI UNATOKANA NA KOO MBILI TOFAUTI. UTAMKUTA MAMA ANA UKOO WAKE NA BABA ANA UKOO WAKE. KUMBUKA YA KWAMBA KIUNGANISHI CHA KOO NI NDOA NA MUHURI (ALAMA) WA MUUNGANO WA KOO HUSIKA NI KIZAZI
(MTOTO AU WATOTO).
IKIWA KOO HUSIKA KATIKA MUUNGANO WENYE MSINGI WA NDOA, ZITAKUWA NA UPENDO, ULINZI, MALEZI BORA NA HURUMA JUU YA WATOTO WAO, AMBAO NI MUOAJI(MWANAMUME) NA MUOLEWA(MWANAMKE), BASI KITAKACHOFUATA, KOO ZOTE MBILI ZITASHIRIKIANA KATIKA KILA HALI, BILA KUJALI FURAHA, MAUMIVU, PESA, MALI,……….N.K, NA KUHAKIKISHA USALAMA WENYE MAZINGIRA YA UPENDO, AMANI NA UTULIVU, UNADUMU KATIKA MUUNGANO HUSIKA.
NA NDIOMAANA KILA UKOO UNAKUWA NA WATU WAZIMA NA WENYE AKILI TIMAMU, WENYE KUSIMAMIA, KUUNGANISHA, KUONDOA TOFAUTI ZA CHUKI NA KULINDA HAKI YA KILA UKOO NA KUSIMAMIA BENDERA
(KIUNGANISHI NI NDOA NA BENDERA KUU NI MTOTO AU WATOTO) YA MUUNGANO WA KOO ZOTE HUSIKA.
MWANAUME ANAPOFUNGA NDOA, NDUGU, JAMAA, NA MARAFIKI WANASHEHEREKEA MUUNGANO(NDOA) HUSIKA. LAKINI KINACHO BAKI NI SIRI YA KUWA KIZAZI KIPO?
MWANAMKE MWENYE KUOLEWA NA KUPATA MTOTO, HUWA NA UMUHIMU NA NGUVU KATIKA KOO ZOTE HUSIKA. NA MWANAMKE MWENYE UKOSEFU WA BENDERA(MTOTO), HUWA NI MWENYE KUJIHISI VIBAYA NA MARANYINGINE AKISIMANGWA NA WANACHAMA WA UKOO WA UPANDE WA MMEWE, NA MARANYINGINE HUJIKUTA AKIKUMBANA NA MAADUI KUTOKA UPANDE WA UKOO WAKE, WAKIMUONA YA KWAMBA NI TASA WALA HANA UWEZO WA KUPATA MTOTO. LAKINI KUMBUKA YA KWAMBA KUMPATA MTOTO NA KUMKOSA(KUKOSA KIZAZI) YOTE HAYO YANATOKANA NA UWEZA WA MWENYEZI MUNGU. KUNA BAADHI YA WANAWAKE WANAOKOSA KIZAZI, KUTOKANA NA NJIA YAO YA UTOWAJI WA MIMBA. MARANYINGI UTOAJI WA MIMBA UNAHARIBU KIZAZI.
IKIWA KOO ZOTE MBILI ZITAKUWA NA MAZINGIRA MAZURI YA KUONEANA HURUMA NA MSINGI WA KULINDA HESHIMA YAKE KATIKA JAMII, BASI HAKUNA UKOO AMBAO UTAKUBALI AU KURUHUSU WATOTO WAKE WA YATIMA, KUHANGAIKA KATIKA VITUO VYA YATIMA AU KUZURURA BARABARANI(WATOTO WA MTAANI) OVYO OVYO BARABARANI BILA KUWA NA DIRA YENYE MFUMO WA MALEZI NA MSINGI WA MAISHA BORA NA UKUTA WA ELIMU BORA KWA KILA MWANA CHAMA WA KOO HUSIKA.
UPUNGUFU WA UPENDO KATIKA KOO, NDICHO CHANZO CHA MGAWANYIKO WA MAPENZI KATIKA NYOYO ZA WANACHAMA WA KOO HUSIKA.
MATUNDA YA UKOO BAADA YA MSAADA WA MALEZI JUU YA MTOTO AU WATOTO YA TIMA****NI NINI ?
KILA MTU ANAPENDA KUTOA SHUKURANI PALE ALIPOSAIDIWA NA KULAUMU PALE ALIPOUMIZWA. KWA MUJIBU WA MAISHANI, KILA JAMBO MAISHANI MWETU LINAHITAJI ELIMU YA KUTOSHA ILI KUKABILIANA NALO, BILA KUSABABISHA BADHARA YENYE JINA LA SIKUJUWA A.K NAJUTA KULIFANYA.
UKIWASAIDIA WATOTO AU MTOTO WA YATIMA. TAYARI UNAPATA THAWABU, NA UMETOA MCHANGO WA KUPUNGUZA WEZI, MAKAHABA, WAKABAJI, WABAKAJI, MATAPELI, WATOTO WA MTAANI, MARADHI KAMA UKIMWI, TIBI, HASIRA, CHUKI, LAWAMA, FITINA………N.K. YOTE HAYO UTAKUWA UMEAYASAIDIA KATIKA JAMII. KILA JAMBO AMBALO MWENYEZI MUNGU ANATUKATAZA LINAMAFUFA JUU YETU BINADAMU WOTE, NA LILE TUNALOKATAZWA NINA MADHARA JUU YETU SOTE.
MTOTO YATIMA ANAPOKOSA MSAADA NA AKADHULUMIWA NA WANACHAMA WA KOO ZOTE (UPANDE WA BABA NA MAMA), MARANYINGI ANABADILIKA KIAKILI NA KIVITENDO. IKIWA NI MTOTO WA KIKE, ATAAMUA KUTUMIA MWILI WAKE ANAVYO JUWA, ILIMRADI AKIDHI MAHITAJI YAKE, NA PALE ANAPOKUWA ANAISHI NA WADOGO ZAKE, JITIHADA ZITAKUWEPO ZA KUBADILI WANAUME NA KUFANYA KILA AINA YA KAZI ILIMRADI APATE KIPATO CHA KUWALISHA WADOGO ZAKE NA KUWASOMESHA. MATOKEO YAKE HUJIKUTA AKIKUMBANA NA MIMBA ZENYE MSINGI WA SIMJUI BABA YAKO, TAYARI AMEISHA TENGENEZA VITA NYINGINE BAINA YAKE NA MTOTO WA HARAMU. AKIJIZUIA AKITUMIA KINGA ATAJIKUTA AKIKOSA HESHIMA, NA AKIMUACHA MUNGU WAKE KATIKA MASAFA MAREFU. AKISEMA ASIFANYE UKAHABA HAKUNA MTU YEYOTE KATIKA JAMII MWENYE KUMSAIDIA KATIKA KATIKA MAZINGIRA HAYO MAGUMU. NA AKIANGALIA PEMBENI KANISANI AU MSIKITINI HAKUNA MFUKO WA MATIBABU, MAVAZI, KUWASOMESHA AU KUWALISHA WATOTO WA YATIMA. AKIGEUKA AMEKUMBANA NA MISTA UKIMWI KWENYE KONA. AKITAFAKARI, BINAADAMU KAMA KAWAIDA YAO, MUONE AMEATHIRIKA, KWANZA ALIKUWA AKILINGA…..AKIINAMA KWA MAUMIVU ANAKUMBANA NA RIPOTI YA CHAKU, ADA, KODI YA NYUMBA……N.K. HAYA NDIO MAISHA YA WATOTO YATIMA. HAYANA MWISHO KATIKA MAELEZO, KWASABABU KILA MTOTO WA YATIMA ANAUPEO WA KUJUWA MAPENZI YA WATU ZAIDI YA WATU WANAVYO JIJUWA.
WATOTO YATIMA NI RAHISI SANA KUKUMBUKA FADHILA JUU YAWALE WALIOWAPA AU KUWAONESHA NJIA YA WEMA NA NIRAHISI KUONDOA UPENDO JUU YA KILA MTU WANAOMFAHAMU KATIFA KOO ZAO, AMBAYE HAJAWASAIDI HATA KIKOMBE CHA MAJI AU MAWAZI YENYE MSINGI WA FARAJA. NDIO MAANA MWENYEZI MUNGU ANATUHIMIZA KUWA NA SUBIRA(UVUMILIVU) MAISHANI MWETU. BILA SUBIRA DUNIA HII INGEWAKA MOTO KWA KULIPIZA KISASI, NAFIKIRI HOSPITALI, MAGEREZA, VITUO VYA POLISI NA MAKABURINI KUNGEKUWA BIZE. LAKINI KUTOKANA NA NGUVU ZA MWENYEZI MUNGU, AMECHANGANYA WATU WENYE WIVU, CHUKI, LAWAMA, HUSUDA PAMOJA NA WANAWAKE NA WANAUME, WENYE MOYO WAKUWAONEA WATOTO YATIMA HURUMA NA KUWASAIDIA MAHITAJI YAO. UNAPOMSAIDIA MTOTO WA YATIMA MAISHANI MWAKE, TAYARI UMEMTANDIKIA LAMI KATIKA NJIA YAKE. NJIA PANDA YENYE LAMI HUWA NI BORA KULIKO NJIA PANDA YENYE MABONE YA CHUKI, FITINA, WIVU, LAWAMA, HASIRA, UADUI…………N.K.
MTUME MUHAMMAD(S.A.W) ALISEMA
“NYUMBA MBAYA YA KIISLAMU NI ILE AMBAYO INAMTESA MTOTO WA YATIMA. NA NYUMBA NZURI YA KIISLAMU NI ILE AMBAYO INAMLEA MTOTO YATIMA KATIKA MAZINGIRA MAZURI”
MTUME MUHAMMAD(S.A.W) ALISEMA
“UKIMLEA MTOTO WA YATIMA VIZURI UTAKUWA SAMBAMBA NA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) PEPONI”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment