KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 31, 2009

TAWHIID

NENO TAWHIID NI UNGANISHO (KUFANYA KITU KIMOJA) NA LINATOKANA NA NENO LA KIARABU ‘WAHHADA’, LENYE MAANA YA KUUNGANISHA KUFANYA KITU KIMOJA. LAKINI NENO TAWHIID LINAPOTUMIKA KUMUELEZEA MWENYEZI MUNGU (YAANI TAWHIIDULLAH) LINA MAANA YA “KUMPWEKESHA MWENYEZI MUNGU” KATIKA KILA KITU, KWAMBA YEYE NI MMOJA NA UMOJA WAKE UNATOSHA KWA KILA KITU NA KILA JAMBO NA HANA MSHIRIKA.
KWA MUKTADHA HUO TAWHIID BASI NI IMANI KUWA MWENYEZI MUNGU NI MMOJA, HANA MSHIRIKA KATIKA UTAWALA NA MATENDO YAKE; HANA MFANO KATIKA ASILI YAKE WALA SIFA ZAKE; WALA HANA MPINZANI KATIKA UUNGU WAKE NA KUABUDIWA KWAKE. KWA HAKIKA TAWHIID NI DHANA YA KIMAPINDUZI INAYOLENGA KUMKOMBOA MWANADAMU KUTOKA KATIKA GIZA LA UJAHILI NA UKAFIRI KUMPELEKA KWENYE MWANGA. KUTOKANA NA MAELEZO HAYA NDIO TUNAPATA MAFUNGU MAKUU MATATU YA TAWHIID AMBAYO NI:
1. TAWHIIDIR – RUBUUBIYYA ( YAANI, KUMPWEKESHA MWENYEZI MUNGU KATIKA UTAWALA WAKE)
2. TWHIIDIL – ASMAA WASIFAAT ( YAANI, KUMPWEKESHA MWENYEZI MUNGU KATIKA MAJINA NA SIFA ZAKE)
3. TAWHIIDIL – IBAADAH ( YAANI, KUMPWEKESHA MWENYEZI MUNGU KATIKA KUABUDIWA)
VIPENGELE HIVI VITATU NDIVYO VINAVYOFANYA MSINGI WA SAYANSI YA TAWHIID.
VYOTE VITATU VINATEGEMEANA, NA KUCHA KIMOJAWAPO KUNAITIA DOSARI IMANI NZIMA YA TAWHIID. KIPENGEE KIMOJA TU KATIKA HIVYO KIKIKIUKWA BASI MTU HUZAMA KWENYE

No comments:

Post a Comment