KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, August 18, 2009

Homa ya nguruwe yaenea Kenya


Taarifa kutoka Kenya na Jamhuri ya kidemocrasia ya Congo zinathibitisha kuwepo na kuenea kwa homa ya nguruwe katika nchi hizo mbili .
Taarifa hizi zimethibishwa na mawaziri wa afya wa nchi hizo Bi Beth Mugo na Bw. Augustin Mopipi. Nchini Kenya, Bi Mugo aliiambia BBC kwamba wizara yake imethibitisha kwamba maambukizi ya homa ya H1N1 yamekuwa yakitokea katika maeneo mbali mbali. Kufikia sasa watu wapatao 71 wamethibitishwa kuugua homa hiyo.

Kati ya hao, amesema watu 40 wameambukizwa homa hiyo katika mji mkuu wa Kenya Nairobi na watu wengine 10 huko Keiyo magharibi mwa nchi hiyo, ambako watu 300 wanaendelea kuchunguzwa baada ya kupatikana na dalili za homa hiyo.

Kati ya maeneo mengine yalioathrika nipamoja na mji wa Kisumu ambako watu 18 wameambukizwa, mjini Garissa watu wawili na Mjini Nyeri mtu moja.

Licha ya maambukizi hayo, waziri Mugo amewashauri wakenya wasiwe na hofu, huku akisisitiza kwamba Homa hiyo inadhibitiwa na haina makali kama ilivyo hofiwa hapo awali.

Wanaoambukizwa hata hivyo wamelalamika kwamba hawapati dawa.

DR Congo

Huko Congo serikali pia imethibitisha kwamba mtu moja ameambukizwa homa hiyo kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Hii ni mara ya kwanza homa hiyo kuthibitishwa nchini humo kwani ripoti za hapo awali zilizodai kuwepo homa hiyo zilikanushwa baadaye.

Bwana Mopipi akizungumza na BBC, alithibitisha kwamba mtu anayeugua ni mchimba madini kutoka mji wa Lumbubashi, katika jimbo la Katanga, aliyekuwa amesafiri Afrika Kusini.

Mchimba madini huyo waziri alisema ametengwa pamoja na wote waliosafiri naye licha ya kwamba hawajaonesha dalili zozote za kuugua homa hiyo.

Bwana Mopipi amesema kwamba, serikali ya Jamhuri ya kidemocrasia ya Congo ilikuwa tayari kupambana na homa hiyo na imeweka hifadhi ya madawa ya kutosha.

No comments:

Post a Comment