KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, July 10, 2009

Mawaziri wa MDC wamsusia Mugabe


Mawaziri wa MDC wamsusia Mugabe

Mawaziri kutoka chama cha Movement for Democratic Change (MDC) nchini Zimbabwe wamesusia kikao cha baraza hilo kilichoendeshwa chini ya uenyekiti wa rais Robert Mugabe.
Mkutano huo, ambao hufanyika kila siku ya Jumanne, ulifanyika mapema zaidi kumwezesha Bw Mugabe kwenda Libya kuhudhuria mkutano wa viongozi wa mataifa wa African Union.
Wakati Bw Mugabe akiwa nje ya nchi, kiongozi wa MDC, ambaye ni waziri mkuu Bw Morgan Tsvangirai huendesha vikao vya baraza la mawaziri.
Naibu kiongozi cha MDC amesema chama tawala kimeonyesha "dharau" kuhusu serikali ya muungano ya kugawana madaraka iliyoundwa Februari 2009.
Chama cha Zanu-PF "hakijaipokea MDC kama mshirika sawal", Makamu wa rais wa MDC, Thokozani Khupe alisema.
Alisema uamuzi wa kubadilisha ratiba ya kikao unaashiria " maamuzi ya upande mmoja, kukosa heshima, dharau na kukataa kutambua hali halisi na utaratibu wa makubaliano ya kisiasa", shirika la habari la AFP lilimnukuu akisema hivyo.

No comments:

Post a Comment