KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, June 27, 2009

HASHEEM THABEET NI NANI NA KWA NINI ACHAGULIWE KATIKA NAMBA 2 BORA ?



CHAMA CHA MPIRA WA KIKAPU TANZANIA PAMOJA NA UBALOZI WA WATU WA MAREKANI KIMEMPONGEZA MTANZANIA HASHEEM THABEET KWA KUFUZU KUCHAGULIWA KUCHEZA LIGI MASHUHURI DUNIANI YA MPIRA WA KIKAPU ‘NBA’.
AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI JANA MWAKILISHI WA UBALOZI HUO, AFISA DIPLOMASIA, KEREN GRISSETTE ALISEMA NI JAMBO LA KUJIVUNIA KWA TANZANIA PAMOJA NA NCHI YA MAREKANI KUTANGAZWA MCHEZAJI HUYO KUWEKA REKODI HIYO.



“NIJAMBO LA KUPONGEZWA KWA MCHEZAJI HUYO KUTANGAZWA JANA ( JUZI ) KATIKA JIJI LA NEW YORK AKIWA MCHEZAJI NAMBA MBILI KWENYE KINYANG’ANYIRO HICHO NA KUCHAGULIWA KUJIUNGA NA TIMU KUBWA KAMA MEMPHIS GRIZZLIES KATI YA MAMIA YA WACHEZAJI WALIOWANIA NAFASI HIYO,”




“HIVI SASA MICHEZO IMEKUWA LUGHA YA KIMATAIFA BILA KUJALI TOFAUTI ZETU ZA UTAIFA ,RANGI AU HATA DINI SOTE TUNAVUTIWA NA MICHEZO, TUNAMTAKIA MAFANIKIO MAKUBWA YA USHIRIKI WAKE KWENYE LIGI YA NBA, HONGERA SANA .” ALISEMA GRISSETTE.

NAYE KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MPIRA WA KIKAPU NCHINI TBF, LAWRENCE CHEYO ALISEMA NI HISTORIA KWA HASHEEM THABEET KUCHAGULIWA KUWA NDIO CHAGUO LA PILI AKITANGULIWA BLAKE GRIFFIN AMBAYE AMEENDA LA CLIPPERS.



HASHEEM ANAJIUNGA NA WACHEZAJI WENGINE TAKRIBANI 70 KUTOKA NCHI MBALI MBALI KWENYE LIGI YA NBA.

HASHEEM THABEET ALIKUWA AKICHEZA KIKAPU KWENYE TIMU MBALIMBALI ZA MITAANI JIJINI DAR ES SALAAM NA ALIENDA NCHINI MAREKANI KUJIUNGA NA CHUO KIKUU NA KUCHEZA MPIRA WA KIKAPU KATIKA CHUO CHA CONNECTICUT BAADA YA KUPATA UFADHILI WA KULIPIWA GHARAMA ZA MASOMO (SCHOLARSHIP).


HASHEEM AINGIA NBA










KAULI YA HASHEEM THABEET NI

“ KWANGU MIMI NI BARAKA KUBWA KUTOKANA NA KUPATA FURSA YA KUJA HAPA KUPATA ELIMU………….NAPENDA KUSEMA KWENU ASANTENI SANA.

KILA JAMBO MAISHANI LINAWEZEKANA LA KINI JAMBO MUHIBU NI KUWA NA JITIHADA NA KUWA MWEPESI WA KUSAIDIA AU KUSAIDIWA KATIKA MAENDELEO.

HASHEEM ALIPATA MDAMINI NA AMEWEZA KUFIKA MBALI NA KULETA HESHIMA NCHINI MWETU.
KWA SASA TANZANIA NI NCHI YENYE KUFAHAMIKA KATIKA KUMBUKUMBU ZAMANENO NA VITENDO ENDELEVU.


MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA NA VIONGOZI WAKE AMIN.

No comments:

Post a Comment