KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, May 26, 2009

Al-Shabaab wakiri kufanya shambulio

Al-Shabaab wakiri kufanya shambulio

Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Al- Shabaab nchini Somalia limedai lilihusika na mashambulio ya mabomu ya kujitoa muhanga yaliyotokea katika mji mkuu Mogadishu.





























Wapiganaji wa Al Shabaab wamedai kuhusika na mashambulio
Kundi la wanamgambo wa Kiislamu nchini Somalia , Al- Shabaab , linaloaminika kuwa na ushirikiano na kundi la kigaidi la Al- Qaeda limedai kuhusika na mashambulio ya mabomu ya kujitoa muhanga mjini Mogadishu.
Kiongozi wa kisiasa wa kundi hilo Shaykh Husayn Ali Fiidow amesema walimtumia mvulana mmoja mdogo kufanya shambulio hilo ambalo liliwauwa wanajeshi sita na raia mmoja.

Mlipuaji huyo aliendesha gari aina ya Pick-up hadi kwenye chuo cha kutoa mafunzo kwa maafisa wa Polisi.

Ongezeko la mapigano mjini Mogadishu katika muda wa majuma mawili yaliyopita yamelazimisha karibu watu 60,000 kuutoroka mji huo.

Takriban watu mia mbili wanadhaniwa wameuwawa tangu mwanzoni mwa mwezi Mei , huku wanamgambo wa Kiislamu wakijaribu kuiangusha serikali ya mpito.

Wanataka kulazimisha kuzingatiwa kwa sheria kali za Kiislamu katika utawala na wanataka kikosi cha kulinda amani cha umoja wa Afrika kiondoke Somalia.

Mara ya mwisho shambulio la bomu la kujitoa muhanga kutokea mjini Mogadishu ilikuwa mwezi wa Februari kwenye kituo cha kikosi cha AU, ambapo wanajeshi 11 kutoka Burundi waliuwawa.

Wanajeshi 4,300 wa AU hawahusiki kwenye mapigano hayo kwa kuwa hawana idhini ya kuwashambulia wanamgambo.

Rais mwenye msimamo wa wastani kuhusu Uislamu Sheikh Sharif Sheikh Ahmed alichaguliwa na serikali ya mseto mwezi Januari chini ya mpango wa amani ulioungwa mkono na umoja wa mataifa.

Lakini hata baada ya kiongozi huyo kuanzisha utawala wa Sharia katika nchi hiyo yenye waislamu wengi , hatua hiyo haijawaridhisha wanamgambo wa kiislamu.
Al-Shabaab wakiri kufanya shambulio

Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Al- Shabaab nchini Somalia limedai lilihusika na mashambulio ya mabomu ya kujitoa muhanga yaliyotokea katika mji mkuu Mogadishu.

No comments:

Post a Comment