KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, April 30, 2009
HOFU YA TANDA KATIKA NYOYO ZETU LEO NA MATUMAINI YETU YA MAISHA TUMEMWACHIA MUNGU
Dar yawaka Moto leo!
Kwa wakazi wa jiji la Bongo leo ilikuwa ni siku ya hofu tele! Kwani mitaa ya mbagala kulikuwa na Mabalaa ya hatari sana! Kwa habari tulizopata ni kuwa mabomu kibao yamelipuka na kusababisha matatizo na vifo kwa wakazi waishio karibu na maeneo ya karibu. Kwa watu wafanyao kazi pale mjini mitikisiko ya mabomu hayo yalitosha kuwafanya waachie ofisi zao na kukimbia ovyo bila mpango, redio nazo hazikuwa nyuma katika kutoa taarifa kinzani kuhusu tukio zima!
Kwa kifupi unaweza pata picha kuwa jiji letu halina mpango maalumu kuhusu majanga mbalimbali yanayoweza kutokea katika jamii! Hatajajitayarisha ya kutosha kwa maafa ya aina mbalimbali kama vile moto, umeme, mafuriko, na majanga mengineyo mengi! Tukiola leo ni somo tosha kwa wakuu wetu ni jinsi gani twaweza kujipanga kwa athari zozote zinazoweza kutokea kwetu wakati wowote ule. Mfano ni jinsi gani sehemu hatari kama maghala ya silaha kali za jeshi zinavyoweza kuweka katika mazingira yasiyo salama kama ilivyotokea leo! Nadhani hili ni fundisho tosha wakuu wetu kupanga jinsi gani twaweza kuepuka na majanga kama haya.
Pia kwa watoa huduma za mtandao, kwani kwa muda mrefu wamekuwa hodari kwa kututumia meseji kuhusu promosheni zao ila leo kwa ajabu mitandao yao ilikwenda off! Sasa waweza kujiuliza ikiwa mitandao iko off na una ndugu ama jamaa yako huko itakuwaje!
MATESO YA WATER BOARDING JUU YA WATUHUMIWA WA KIGAIDI RAIS BARAK HUSEIN OBAMA AFICHUWA SIRI ZA MR. BUSH
Water Boarding
Kutana na staili ya kinyama inayomlazimisha mateka/mfungwa au mtuhumiwa yoyote yule kutoa habari ambazo mtesaji anazihitaji. Mchezo huu wa hatari umekuwa ukifanywa na wanajeshi wa Kimarekani kwa wafungwa wa jela ya Guantanamo Bay huko Kuba (Cuba). Mheshimiwa Obama akaona isiwe tabu akatoa mafaili ya dondoo zote jinsi watu walivyoteswa kwa staili hii ya water boarding.
Yaani ni hivi: Unafungwa mikono na miguu kisha unafunikwa kichwa na kitambaa kisha unamwagiwa maji ili udhani kama unazama, zoezi hili laweza kufanywa kwa mda wowote ule ambao mtesaji anataka . Kisha chochote usemacho kinaweza tumika kama ushahidi wakati wa kesi! Ajabu!
Ila la ajabu na kweli ni jeshi la Marekani linapiga marufuku kumtesa mwanajeshi yoyote wa kimarekani anapokamatwa kivita! Je hii ni sawa?
Nadhani sasa ni sawia kuwa tunaishi kwa sheria za porini! Mwenye Nguvu ndie aliye sahihi! Kwani kibinadamu inajulikana kuwa usimtendee mwenzio usichotaka kutendewa wewe! Kwa ufupi waweza pata picha ya vita dhidi ya ugaidi ilivyo ya kidhalimu! Na tukiwa wapenda amani duniani tunapenda kuombea amani kwa dunia yote kwa ujumla!
Tuesday, April 28, 2009
Swine Flu
Wakati ulimwengu ukiwa unapambana na tishio jipya la mafua ya kitimoto, hapa Bongo land mambo bado politiki. hakuna idara yoyote ya kiserekari au isiyo ya kiserekari iliyotoa onyo ama tangulizi kuhusu janga hili. kisha tunasema tupo kwenye utandawazi?
Ni jukumu letu sasa sisi wazee wa maishani kuwataadharisha watanzania kuwa mzee kitimoto ni soo! habari ndio hiyo waungwana!watu kibao wameshakata roho huko mexico na usa! Tunasubiri nini? Why!
Friday, April 24, 2009
Ubaguzi Mashariki ya Kati
Katika khali ya kustajabisha hivi karibuni kulifanyika mkutano nchini Uswizi ili kuzungumzia kuhusu Ubaguzi kidunia! La ajabu ni kwamba mataifa makubwa yenye ushawishi wa khali ya juu yalijitoa kaitika mkutano huo kisa? Raisi wa Irani atakuwa mmoja wa wasemaji katika mkutano huo! Na hoja ya raisi huyo ilikuwa inahusu taifa la Israeli kukalia kwa mabavu ardhi ya wapalestina! Je kuongelea jambo hili ni ubaguzi? je kukwepa na kujitoa katikati ya mazangumzo ni ubaguzi? Je ni kweli dunia imefika mahali imekuwa na upofu wa kutoona nini ni haki na nini si haki? Je nani anabaguliwa huko Mashariki ya mbali? Israeli au Palestina? nani anapata tabu? nani amekataa tamaa? nani anaishi katika hofu?nani anakosa huduma zote muhimu kama shule, maji,umeme,miundombinu,hospitali?
Alafu kwenye mkutano mkubwa kama huu kwanini Afrika haikuzungumziwa?je sisi hatuna khali ya kubaguliwa? je utumwa ule wa zamani wa mwili na utumwa huu wa sasa wa kiakili si ubaguzi? ikiwa wanaisraeliwalilipwa kwa maovu waliyotendewa na wajerumani sisi waafrika mbona kimya? nani atatulipa? nani atadai haki yetu toka kwa hawa mabwana wakubwa? je afrika tutaendelea kutothaminiwa mpaka lini? na sisi tunamtazamo gani kwa mateso ya wenzetu wapalestina? je tunajitahidi vipi kuona haki zao na zetu zinapatikana! kisha ebu sema , Jeshi la mrusi lilipo vamia na kuipiga georgia dunia nzima ilihamaki je mbona huko kongo,somalia,sudani,uganda.madagaska,chadi nani anasema juu yao?Au ubaguzi una maana tisizozijua? mfano ugaidi,ugaidi unamaana gani!
Ubaguzi ni kitu kibaya sana iwe wa kifikra au kimwili.
tafadhali jamani kwa pamoja tupige vita ubaguzi wa aina yoyote ile hapa katika uso wa dunia yetu!
Tuombee haki kwa kila kiumbe cha Mola
Waafriaka Amkeni Kifikra!
Mapambano bado yanaendelea na ndio twaweza kufanya na kufanikiwa tukiwa na umoja na kuondowa husda na fitna na chuki na uroho wa madaraka katika nafsi zetu.
Mungu Bariki Afrika
Mungu ibariki Dunia Nzima!
Raisi Mpya Mtarajiwa wa Afrika ya Kusini
Raisi mtarajiwa wa hapo Bondeni ndio huyo hapo, anaitwa Jacob zuma na kwa kweli hana mfano katika viongozi wa sasa, kwani jamaa kwa mila na kwa mambo ya kigeni vyote vyake. Ana wake lukuki na watoto kibao pia haijulikani nani atakuwa first lady wake. yaani vurugu tupu ila ukipendwa umependwa kwani nyota yake kwa wapiga kura wa Afrika ya kusini ni njema.Licha ya kuwa hana ya kutosha pia ana kashfa za kila aina kuanzia ngono mpaka kashfa za rushwa watu hawajaona mwengine zaidi yake.
Pongezi zetu ziende kwa watu wa kusini ya afrika na tunatumai atafanya mabadiliko ya maana kuondoa umaskini, kumpambana na maradhi ya ukimwi kupunguza uharifu uliokithiri maana kombe la dunia laja hapo mwakani wasije tutia aibu bure! pia kuondoa matabaka ya matajiri na maskini yaliokithiri. Mungu ibariki Afrika ya Kusini, Mungu ibariki Tanzania na Mungu ibariki Afrika nzima!
Tuesday, April 21, 2009
UHARAMU WA RIBA KATIKA DINI
(QURAN AND BIBLIA)
NENO RIBA KWA UPANA KWA SASA LINATUMIKA SANA KIPESA! ILA NENO HILI LIMETOKA MBALI TANGU ENZI HIZO ZA MITUME NA WATAKATIFU WETU. JE! MWENYEZI MUNGU ANASEMAJE KUHUSU RIBA?
QURAN
WALE WANAOKULA RIBA ,HAWASIMAMI ( KUENDESHA YAO ) ILA KAMA ANAVYOSIMAMA YULE AMBAYE SHETANI KAMZUGA KWA KUMSAWAA; ( WAKO MBIONI TU, HAWANA KITUO ). (NA) HAYA NI KWA SABABU WAMESEMA, “ BIASHARA NI KAMA RIBA”, HALI MWENYEZI MUNGU AMEIHALALISHA BIASHARA NA KAIHARAMISHA RIBA. NA ALIYEFIKIWA NA MAUIDHA KUTOKA KWA MOLA WAKE
(YA HUKU KUKATAZWA RIBA), KISHA AKAJIZUIA, BASI YAMEKWISHA MTHIBITIKIA YALE (MALI) YALIOPITA (ALIOKWISHA YA PATA); NA HUKUMU YAKE IKO KWA MWENYEZI MUNGU. LAKINI WANAOREJEA (KULA RIBA) BASI HAO NDIO WATU WA MOTONI, HUMO WATAKAA MILELE. (2: 275)
BIBLIA
YESU “NA MKIWAKOPESHA WATU, HUKU MKITUMAINI KUPATA KITU KWAO, MWAONYESHA FADHILA GANI? HATA WENYE DHAMBI HUWAKOPESHA WENYE DHAMBI, ILI WAWARUDISHIE VILEVILE. BALI WAPENDENI ADUI ZENU,TENDENI MEMA, NA KUKOPESHA MSITUMAINI KUPATA MALIPO,NA THAWABU YENU ITAKUWA NYINGI, NANYI MTAKUWA WANA WA ALIYE JUU, KWA KUWA YEYE NI MWEMA KWA WASIOMSHUKURU, NA WAOVU. BASI IWENI NA HURUMA , KAMA BABA YENU ALIVYO NA HURUMA.MSIMUHUKUMU, NANYI HAMTAHUKUMIWA, KIPIMO CHA KUJAA NA KUSHINDILIWA, NA KUSUKWA SUKWA HATA KUMWAGIKA, NDICHO WATU WATAKACHO WAPA VIFUANI MWENU. KWA KUWA KIPIMO KILEKILE NDICHO MTAKACHOPIMIWA.
(LUKA 6: 34….38)
KWA KUSOMA MAANDIKO MATAKATIFU HAPO JUU WAWEZA PATA PICHA HALISI KUHUSU MTAZAMO WA KIDINI KATIKA SWALA ZIMA LINALOHUSU RIBA! RIBA NI TAMAA YA YULE MWENYE MALI ANAYOTUMIA MALI YAKE KUMUDHULUMU YULE ASIYE NA MALI KWA LENGO LA KUMFANYA AFIKIRI KAMA ANAMSAIDIA SHIDA ZAKE! PINDI RIBA INAPOSHINDWA LIPWA NDIPO UNAPOWEZA KUONA UDHALIMU WA YULE MTOAJI WA RIBA DHIDI YA YULE MDAIWA RIBA! KIPINDI KINGINE TUKIWA TUMEBANWA NA SHIDA ZETU HATUTAMBUI HATARI YA MTEGO HUU WA RIBA NA KUDHANI NI JAMBO LINALOWEZA KUWEZEKANA HII INASABABISHWA NA UPOFU WA SHIDA ZETU NA UPOFU WA FIKRA ZETU TUWAPO NA SHIDA! UPOFU HUU UTUSABABISHIA KUTOKUONA UHARAMU WA RIBA KAMA MAANDIKO YANAVYOTUELEZA. RIBA IMEKUWA MTIHANI BAINAYA MATAJIRI NA MASIKINI. MATAJIRI WANAONA KAMA SEHEMU YAO YA MRADI NA MASIKINI ANAONA KAMA UKOMBOZI WA MATATIZO NA SHIDA ZAKE. WOTE KWA PAMOJA HUSAHAU MAAGIZO YA MWENYEZI MUNGU LICHA YA KWAMBA WOTE WANADAI KUWA NI WACHA MUNGU NA KUFUATA MIONGOZO YA DINI ZAO. LICHA NA UHARAMU WAKE, RIBA IMEGEUZWA BIASHARA KATI YA MWENYE NACHO NA ASIYE NACHO WOTE KWA PAMOJA WAKIKUBALIANA KAMA NI BIASHARA YA USAWA ILA PINDI RIBA HIYO ISHINDWAPO KUPATIKANA NDIPO YALE ALIYOKATAZA MWENYEZI MUNGU HUONEKANA HADHARANI. KWANI CHUKU, UBABE, UONEVU HUFUATWA NA YULE MASIKINI ALIYEDHANI RIBA NI UKOMBOZI WAKE HUPATA DHAHAMA YA KHALI YA JUU. KWANI HUWEZA KUUTUMBUKIZA KATIKA UMASIKINI ULIOKITHIRI ZAIDI YA HAPO MWANZO!
JAMBO LA KUFUATA HAPA NI KUSOMA MAANDIKO MATAKATIFU NA KUYAFUATA KAMA MAAGIZO YA MANENO HAYO YANAVYOSEMA. TUPUNGUZE DHULUMA NA UONEVU. KWANI KUASIDIA KWA MAPENZI MEMA NDIO MWENYEZI MOLA ALIVYOTUAGIZA!
ALAAMSIKI!
Friday, April 17, 2009
TAFADHALI AFRICA TUNAKUHITAJI UTUSAIDIE TUTAKUBALI HATA KUMWASI MUNGU ILIMLADI TUJENGE MAJUMBA YAKIFAHARI
WATOTO YATIMA HAWATUHUSU WALA WAJANE WALA MASIKINI.
SI UNAJUA MABIBI, POMBE ,DISCO ,MAGARI MAKALI, UFISADI , RUSHWA YOTE HUWEZI KUYAFANYA BILA HELA. CHUKUWA MALI ASILI WENYE AKILI TUNUFAIKE NA WAJINGA WATAJIJU.
MUNGU KAMA YUPO ATATUHUKUMU SIKU HIYOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO.
KWA KWELI MATAJIRI WANA MACHO HAWAONI NA MASIKIO HAWASIKII. WATOTO YATIMA, WALEMAVU , WAJANE VUMILIENI MUNGU YUKO NANYI. MKIDHULUMIWA DUNIA NA MKAWA WAVUMILIVU NA KUONGEZA IBAADA MTARITHI PEPO.
BARUWA KWA MATAJIRI WOTE DUNIANI
BARUA KWA MATAJIRI WENYE IMANI YA KUWEPO MUNGU
TUNAONGONZWA NA NENO LA MUNGU NDANI YA QURAN NA BIBLIA
KILA BINAADAMU MWENYE AKILI TIMAMU, HANA BUDI YA KUKIRI KWAMBA KUNA MUUMBA WA MBINGU NA ARDHI NA VILIVYOMO. HAKUNA KIUMBE KISICHOSHUHUDIA MAZINGIRA YA AJABU NA YENYE KILA AINA YA UZURI . KILA KIUMBE MUNGU ALIKIUMBA NA AKAKITENGENEZEA UTARATIBU WA MAISHA YAKE HAPA ULIMWENGUNI NA NDIO MAANA TUNAANZA ( KUZALIWA ) TUNAISHI, KATIKA MIKAKATI NA KILA MTU AKIWA NA LENGO FULANI KATIKA MAISHA YAKE, LAKINI MWISHO WA MAMBO ( UHAI ) TUNAJIKUTA MDA WETU WA MAISHA UNAISHA BILA KUFIKIA LENGO AU KUFIKIA LENGO, NA KUANZISHA LENGO LINGINE. IKIWA BINAADAMU ANAAMINI KWAMBA ALIUMBWA NA MUNGU, AKAMPA UHAI NA MAISHA BORA, NI WAJIBU KWAKE KUMTANGULIZA KATIKA KILA JAMBO LILILOPITA, LILIOPO NA LIJALO. LAKINI UTAKUTA WATU MASIKINI NA MAFUKARA MARA NYINGI NDIO WENYE KUWA KARIBU NA MWENYEZI MUNGU. BAADHI YA MATAJIRI , HUJIKUTA KATIKA MAPAMBANO YA KUONGEZA KIPATO CHAO BILA KUWA NA HISIA ZA KUMTANGULIZA MWENYEZI MUNGU, MARA NYINGINE HUWEZA ( MATAJIRI ) KUTAMKA YA KWAMBA PESA NA MALI ZAO, WAMEZIPATA KUTOKANA NA UWEZO WAO WA KIAKILI. BAADHI YA MATAJIRI, ASILIMIA KUBWA YA MALI ZAO HUWA NI ZENYE KASORO YA UHALALI ( DHULMA ). DHULMA HIO HUWAKUMBA WATU MASIKINI, KWA KUDHULUMIWA MALI ZAO, HAKI YA MANENO AU VITENDO , HESHIMA , ELIMU……N.K. UDHAIFU WA MASIKINI MARA NYINGI UNATOKANA NA UPUNGUFU WA ELIMU JUU YA JAMBO HUSIKA AU KUKANDAMIZWA NA FEDHA AU NGUVU ZA TAJIRI HUSIKA. JAMBO HILI HALIJAANZA LEO AU JANA , BALI LILIANZA MIAKA MINGI ILIOPITA.
TUKIANGALIA MAANDIKO YA MUNGU ANAVYOSEMA JUU YA MATAJIRI HAWA, TUTAKUTA WANA MTIHANI MGUMU JUU YA MASIKINI,FUKARA ,YATIMA NA WAJANE.
BIBLIA
HAYA BASI, NINYI ( MATAJIRI ) MSEMAO, LEO AU KESHO TUTAINGIA MJI FULANI NA KUKAA HUMO MWAKA MZIMA, NA KUFANYA BIASHARA NA KUPATA FAIDA. WALAKINI HAMJUI YATAKAYOKUWAKO KESHO.
UZIMA WENU NI NINI? MAANA NINYI NI MVUKE UONEKANAO KWA KITAMBO, KISHA HUTOWEKA. BADALA YA KUSEMA BWANA ( MUNGU AKIPENDA ), TUTAKUWA HAI NA KUFANYA HIVI NA HIVI. LAKINI SASA MWAJISIFU KATIKA MAJIVUNO YENU ; KUJISIFU KOTE KWA NAMNA HII NI KUBAYA. BASI YEYE AJUAYE KUTENDA MEMA , WALA HAYATENDI , KWAKE HUYO NI DHAMBI. (WARAKA WA YAKOBO 4: 13……17)
* HAPO JUU, TUNAELEZWA KWAMBA MAISHANI LAZIMA MUNGU APEWE KIPAOMBELE. LAZIMA KILA MWANADAMU, ANAPOKUWA NA MPANGO WOWOTE, AOMBE MUNGU UZIMA KWANZA NA KISHA AMSHIRIKISHE KATIKA HARAKATI ZAKE ZA KUTAFUTA RIZIKI YA HALALI. LAZIMA KILA BINAADAMU ATAMBUWE KWAMBA MAISHA NI KAMA MVUKE LEO UPO KESHO HAUPO, NA JINA LAKO HUBADILIKA NA KUITWA MAREHEMU. MALI, MKE WATOTO,PESA,NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI HATA ADUI ZAKO WOTE HUBAKI DUNIANI WAKISIKITIKA NA WENGINE WAKIFURAHIA KIFO CHAKO.
IKIWA WEWE NI TAJIRI NA UNAAMINI KWAMBA KILE ULICHO NACHO UMEKIPATA KUTOKANA NA UWEZA WA MUNGU, BASI NIWAJIBU WAKO KUFUATA UTARATIBU WA MAELEKEZO YA KITABU CHAKO KUHUSU HAKI YA MASIKINI, YATIMA,WAJANE, WAFUNGWA , NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI KUHUSU MALI YAKO, NA UKIWA HUNA UWEZO HUO BASI MUNGU YUKO PAMOJA NAWE.
QURANI
KWA YAKINI WALE WANAOSOMA KITABU CHA MWENYEZI MUNGU, NA WAKASIMAMISHA SALA , NA KATIKA YALE TULIOWAPA WAKATOA KWA SIRI NA KWA DHAHIRI , HAO WATATUMAI BIASHARA ISIO DODA ( ISIYOBWAGA ) ( 35 : 29 )
NIWAJIBU JUU YA KILA BINAADAMU , KUSOMA KITABU CHA MWENYEZI MUNGU, ILI KUONGEZA UJUZI NA HEKIMA. MUNGU ALILETA VITABU, VINGI AMBAVYO NI TORATI, ZABURI, INJIRI NA QURAN. VITABU HIVYO VYOTE VINA MAFUNDISHO YANAYOONESHA UTUKUFU WA MUNGU , LICHA YA KUWA KUNA BAADHI YA BINAADAMU WANAO KIUKA AMRI NA SHERIA ZA VITABU HUSIKA NA MARA NYINGINE HUWA NA UBAGUZI WA VITABU KUTOKANA NA MASLAHI YA NAFSI ZAO. KILA KITABU CHA MUNGU KINAFUNDISHA MAADILI NA MFUMO WA MAISHA. KUMBUKA YA KWAMBA KILA KITABU KINA MSAADA JUU YA KINGINE, NA MAFUNDISHO YAKE YOTE YANAHUSU HAKI NA UTUKUFU WA MUNGU.
KUSIMAMISHA SALA ( IBAADA ), NI JAMBO MUHIMU NA NILAZIMA KWA KILA MWANADAMU MWENYE AKILI TIMAMU ,NAKUAMINI YA KWAMBA YEYE NI KIUMBE WA MUNGU NA HANA BUDI YA KUMSHUKURU MUUMBA WAKE. IBAADA NI MAWASILIANO BAINA YA MWENYEZI MUNGU NA VIUMBE WAKE. IBAADA INAMFANYA MTU AEPUKANE NA MAMBO MENGI YA ANASA NA KUWA KARIBU YA MUNGU. IBAADA INAMWEZESHA MTU ,KUMTANGULIZA MUUMBA WAKE KATIKA KILA JAMBO.IBAADA INAMFANYA MTU AWEZE KUWA JASIRI JUU YA MAISHA MAGUMU YANAYO MKABIRI, KUTOKANA NA IMANI YA MFANYA IBAADA, YAKUAMINI KWAMBA MTOA RIZIKI NI MUNGU PEKE YAKE. IBAADA INAMFANYA MTU AWE NA HURUMA JUU YA VIUMBE WENZAKE NA KUWA NA MOYO WA KUWA SAIDIA. IBAADA INAMFANYA MTU AWEZE KUWA NA AIBU, SIFA YA IMANI JUU YA MWANADAMU NI AIBU. UKOSEFU WA AIBU KATIKA MAISHA NDIO CHANZO CHA MAAFA YOTE ULIMWENGUNI.
BAADHI YA MATAJIRI WANAAMINI KWAMBA KUSALI KUNAWAPOTEZEA MDA WA KUSAKA MAPESA. NA MARA NYINGINE MATAJIRI WANAWAZUIA WAJIRIWA WAO, KUSALI AU KUWAPA SEHEMU YA IBAADA KATIKA OFISI ZAO. MATAJIRI WALIO WENGI WANAAMINI YA KWAMBA MDA WA IBAADA NI PUNGUZO LA MAPATO YAO.
UKIAJIRIWA NA TAJIRI KAMA HUYO, LAZIMA UKUBALIANE NA KUKAIDI AMRI YA MUNGU KUHUSU IBAADA YA SALA.
HUU NI MTIHANI WA MATAJIRI JUU YETU MASIKINI!
KUBALI MSHAHARA AU KUMWASI MWENYEZI MUNGU!
KUTOKANA NA MATAJIRI WENGI KUONA KWAMBA SALA , INACHUKUWA MDA WAO WA KIUCHUMI, NDIO MAANA OFISI NYINGI DUNIANI ZIMEPUNGUZA MDA WA MAPUMZIKO WA CHAKULA CHA MCHANA NA KAMPUNI NYINGINE KULA UTAJIJUA NA UKIZUBAA UTAIBIWA NA UTAWAJIBISHWA NA SHERIA KWA KUTOKA SEHEMU YAKO YA KAZI. HUU NI MTINDO WA ULINZI WA MATAJIRI JUU YA MALI ZAO. UTU UNAONDOKA BINAADAMU TUNAINGIZWA KATIKA MFUMO WA MAGEUZI , AMBAO NI VUNJA AMRI YA MUNGU UPATE MKATE AU UNASEMAJE ?
* MWENYEZI MUNGU ANAWAHIMIZA WATU WENYE UWEZO, KUWASAIDIA BINAADAMU WENZAO BILA KUTUMAINI FADHILA YA SHUKURANI KUTOKA KWA WASAIDIWA. MUNGU ANATUHAMASISHA KUHUSU HURUMA NA KUSAIDIANA KATIKA HALI NA MALI. USIMSAIDIE BINAADAMU MWENZAKO ILI UONEKANE KAMA NI MTOAJI AU UNA HURUMA MACHONI MWA WATU, KUMBE MOYONI HUNA HURUMA NA MOYO WA KUSAIDIA MASIKINI,YATIMA,WAJANE NA ……….N.K. UKITOA UNAWEKA AKIBA YA BAADA YA UHAI WAKO.UNAPOTOA MALI YAKO KUMPA MHITAJI, TAYARI MWENYEZI MUNGU ANAKUPA MALIPO YANAOITWA THAWABU. THAWABU NI MALIPO YENYE THAMANI KUBWA , KUMBUKA KWAMBA WINGI WA THAWABU NDIO KUJISHINDIA NAFASI YA KWENDA
PEPONI.
* MWENYEZI MUNGU ANAWAPA TAARIFA NJEMA NA FARAJA KWA MATAJIRI, YA KWAMBA WASIWE NA KHOFU YA KUWASAIDIA WATU, MUNGU ANAWAPA OFA MATAJIRI YA KWAMBA ATALINDA BIASHARA ZAO NA WATAKUWA NA FURSA NZURI YA KUPATA THAWABU NYINGI. NA KUMBUKA WINGI WA DHAWABU NDIO TIKETI YA PEPONI.
KIFO CHA MATAJIRI BAHIRI NA HATIMA YA MALI ZAO
BIBLIA
HAYA BASI, ENYI MATAJIRI! LIENI, MKAPIGE YOWE KWASABABU YA MASHAKA YENU YANAYOWAJIA. MALI ZENU ZIMEOZA, NA MAVAZI YENU YAMELIWA NA NONDO. DHAHABU YENU NA FEDHA YENU ZIMEINGIA KUTU , NA KUTU YAKE ITAWASHUHUDIA , NAYO ITAKULA MIILI YENU KAMA MOTO. MMEJIWEKEA AKIBA KATIKA SIKU ZA MWISHO. ANGALIENI, UJIRA WA WAKULIMA WALIOVUNA MASHAMBA YENU, NINYI MLIOUZUIA KWA HILA, UNAPIGA KELELE , VILIO VYAO WALIOVUNA VIMEINGIA MASIKIONI MWA BWANA ( MUNGU ) WA MAJESHI. MMEFANYA ANASA KATIKA DUNIA , NA KUJIFURAHISHA KWA TAMAA,MMEJILISHA MIOYO YENU KAMA SIKU YA MACHINJO. MMEHUKUMU MWENYE HAKI MKAMWUA; WALA HASHINDANI NANYI. (WARAKA WA YAKOBO 5: 1……6)
QURAN
ADHABU KALI ITAMTHUBUTIKIA KILA MWENYE KURAMBA KISOGO, MSENGENYAJI. AMBAYE AMEKUSANYA MALI NA KUYAHISABU ( TU BILA YA KUYATUMIA KATIKA NJIA YA KHERI ).
ANADHANI YA KUWA MALI YAKE YATAMBAKISHA MILELE.
HASHA! BILA SHAKA ATAVURUMIZWA KATIKA (MOTO UNAOITWA) HUTAMA.
NA NI JAMBO GANI LITAKALO KUJULISHA (HATA UKAJUA) NI NINI (HUO MOTO UNAOITWA) HUTAMA?
NI MOTO WA MWENYEZI MUNGU ULIOWASHWA (KWA UKALI BARABARA).
AMBAO UNAPANDA NYOYONI.
HAKIKA HUO (MOTO) WATAFUNGIWA (WAWEMO NDANI YAKE).
KWA MAGOGO MAREFU MAREFU.
(SURATUL HUMAZAH)
QURAN
JE! HAWAJUI YA KWAMBA MWENYEZI MUNGU ANAPOKEA TOBA YAWAJA WAKE NA KUZIPOKEA SADAKA , NA YA KWAMBA MWENYEZI MUNGU NI MWENYE KUKUBALI TOBA SANA ( NA ) MWENYE REHEMA ?
(9: 104)
HAYA HAYA MATAJIRI ,HUU NI WAKATI WENU WA KULA MBIVU AU MBICHI. TAYARI VITABU VYA MWENYEZI MUNGU VINATOA AU VINAONYESHA NJIA ZA KUPITA NA NI RAHISI KWA WAMCHAO MUNGU.
KUNA MSEMO, USEMAO KAMA IFUATAVYO:
MMEPEWA MACHO HAMUONI!
NI NINI MAANA YA MACHO? MACHO NI CHOMBO AMBACHO,MWENYEZI MUNGU AMEMPA MWANADAMU ILI AWEZE KUONA KITU KIBAYA NA KIZURI PAMOJA NA KUANGALIA NEEMA AU UWEZO WA MUNGU KATIKA KUUMBA NA KUSHUKURU NEEMA ZAKE JUU YAKE ( BINAADAMU ). MACHO YANA UWEZO WA KUONA MAHITAJI,MATESO,MAUAJI,WIZI,UZIZI,UGOMVI,FITNA LAWAMA,HUSUDA,CHAKULA,UPENDO……N.K.
NI WAJIBU JUU YA KILA MWENYE JICHO, KUSHUHUDIA NA KUKEMEA MABAYA NA KUSIFIA NA KUSHUKURU MAZURI AYAONAPO.
MNA MASIKIO HAMSKII!
NI NINI MAANA YA MASIKIO?
MASIKIO NI CHOMBO, AMBACHO BINAADAMU ANAKITUMIA KATIKA HARAKATI ZAKE ZA KUINGIZA SAUTI NA NENO KWENYE NAFSI AU NDANI YA NAFSI HUSIKA. KILA MTU MWENYE NAFSI YA KUNASA SAUTI, JAMBO HILI LINAMHUSU, NA NIMUHIMU KABISA KATIKA MAISHA YAKE.
BABA AKIAMBIWA KWAMBA NI MARUFUKU KUTOKA NJE USIKU. TAYARI UJUMBE UMEFIKA KATIKA KILA NAFSI ILIYOMO NDANI. IKIWA MZAZI (BABA) ATAMTUMA MWANAE NJE KUWASHA SIGARA JIKONI,AKIMPA MATUMAINI KWAMBA SIMBA HAYUPO KARIBU. MTOTO AKIKUMBWA NA KIFO CHA SIMBA BASI,TATIZO HILO LITAKUWA NI KUBWA NA LENYE KULETA MGAWANYIKO KATIKA FAMILIA. WATOTO WALIOBAKI WATAMCHUKIA BABA NA MKE WAKE ATAMCHUKIA MME WAKE NA MAJIRANI WATAMUONA HUYO MZAZI ( BABA MTU ) KAMA MTU MWENYE MATATIZO YA AKILI, NA ATAHUKUMIWA KISHERIA KWA KOSA LA KUMUUA MWANAE.
JE! TATIZO NI NINI HAPA?
TATIZO NI TAMAA YA MZAZI ILIOSABABISHA KIFO CHA MWANAE NA CHUKI NA HUKUMU JUU YAKE. KUSIKIA AMESIKIA LAKINI MOYO WAKE UMEMSHINDA ( UVUMILIVU UMEMSHINDA ) AKAAMUA KUBEBA MIZIGO ( CHUKI,LAWAMA,ADHABU……N.K )MIKUBWA. KWA BINAADAMU KUSAMEHE NI VIGUMU LAKINI KWA MUNGU NI RAHISI.
HII NDIO MAANA YA KUPEWA MASIKIO , NA KUYATUMIA VYEMA.KILA SIKU MAASI YANASIKIKA, KATIKA TV ,RADIO NA KATIKA MIDOMO YA BINAADAMU WENZAO.
IKIWA UMEPEWA MASIKIO NA MACHO NA UNA AKILI TIMAMU, UJUMBE HUO UNAKUHUSU, UKIUFUATA SAWA NA UKIUACHA SAWA HUKUMU IKO JUU YA NAFSI YAKO. KUMBUKA MALI ,MAGARI,MANDEGE,MAJUMBA,MKE AU WAKE ,WATOTO,NGUO ,FEDHA,CHEO,NGUVU ZA MWILI, VYOTE HIVYO VINABAKI NA SIO AKIBA YAKO TENA AKIBA YAKO, NI KILE ULICHOKITOA UKITEGEMEA FADHILA ZA MWENYEZI MUNGU.
EWE MWENYEZI MUNGU, TUNAKUOMBA UTUNUSURU, NA UBAHIRI NA MALI AU RIZIKI YA HARAMU NA UTUWEZESHE KUWA NA HURUMA NA KUWASAIDIA BINAADAMU WENZETU.
AMINA
Nchi ya Rwanda katika mkondo wa Damu wa Kikabila na Kisiasa MPAKA LINI ?
NCHI YA RWANDA KATIKA MKONDO WA DAMU!
KILA MTU ANAHITAJI AMANI KATIKA MWILI NA MAISHA YAKE YOTE.
KILA KUKICHA AFRIKA INAMWAGA DAMU NDANI YAKE, BILA UTETEZI WA WAFRIKA WENYEWE NA WAPENDA AMANI WENGINE DUNIANI. WATU WENGI WANAONGEA KUHUSU HATIMA YA AFRIKA KUWA KITU KIMOJA, LAKINI UTATA UNAJITOKEZA PALE AMBAPO AFRIKA INAJIKUTA KATIKA UTATA WA KIKABILA,MAPINDUZI,MAGONJWA YA KUPANDIKIZWA FITNA NA LAWAMA ZINAZOANDALIWA NA NCHI TAJIRI DUNIANI NA WAAFRIKA WENYEWE.
NCHI YA RWANDA UHASAMA WAKE ULIANZA TANGU ZAMANI KATIKA MIAKA YA 1959, BAINA YA WAHUTU NA WATUTSI. KUMBUKA KWAMBA RWANDA INA MAKABILA MATATU AMBAYO NI WAHUTU,WATUSTI NA WATWA. LAKINI JAMBO LA KUSHANGAZA UHASAMA HUO UPO BAINA YA WAHUTU NA WATUTSI,KIASI KWAMBA KILA KABILA HUJIPA NAFASI YA MBELE ZAIDI KULIKO KABILA JINGINE. MWAKA WA HAMSINI NA TISA VILITOKEA VITA BAINA YA WAHUTU NA WATUSI , NA MWISHO WAKE WATUSI WALIOKUWA WENGI WALIKIMBIA NCHI YAO NAKWENDA KUTANGATANGA KATIKA NCHI ZA JIRANI. KITENDO HICHO NI KITENDO AMBACHO SIO CHA BUSARA BAINA YA NDUGU WAWILI, KUMWAGA DAMU BILA KUFIKIRIA KITAKACHOTOKEA BAADAE KAMA VIFO VYA WATU,KUHARIBU MIUNDOMBINU,ONGEZEKO LA WATOTO YATIMA NA WAJANE,MACHUNGU MENGI NA ULEMAVU WA KILA AINA. HUU SIO UTU WA MAISHA YA BINAADAMU AMBAO TUNAAMBIWA BABA YETU NI MMOJA NA MAMA YETU HAWA. BAADAE WATU WA KABILA LA WATUTSI WALIHITAJI KURUDI NYUMBANI KWA NJIA YA KIVITA. VITA YA WATUTSI KURUDI NYUMBANI ILIANZA MWAKA WA 1990.VITA HIO ILICHUKUWA MUDA WA MIAKA MINNE NA MWISHO WAKE ILIANGUSHWA NDEGE ILIOKUWA IMEBEBA MARAISI WA WILI WA RWANDA NA BURUNDI NA KIKAWA CHANZO CHA VIFO VYA WATU ZAIDI YA MILIONI WENGIWAO WAKIWA NI KABILA LA KITUTSI NA WAHUTU WENYE MSIMAMO WA KATI. MOJA KWAMOJA TUTAONA KWAMBA HATA WATWA WALIKUFA KATIKA JANGWA HILO LA DAMU, LAKINI MAUWAJI YA RWANDA YANAPOTAJWA JAMBO LA KUSHANGAZA WATWA HAWATAJWI KAMA NI WAATHIRIKA WA VITA HIVYO. JAMBO LA MSINGI NI KUJIULIZA UNDUGU WA INCHI ZA AFRICA, KATIKA HARAKATI ZAO ZA KUHAKIKIASHA AFRICA INAKUWA KITU KIMOJA KATIKA MCHEZO WA DAMU ZA WATU WASIO NA HATIA. WAAFRICA WENGI TUMEZOEA UBINAFSI NA KUSTUKA PALE YANAPOTUKUTA , LAKINI KWA WENZETU LAA POA TU.
PINDI VITA VINAANZA RWANDA MWAKA WA 1959 AFRICA NA DUNIA VILISHUHUDIA , WATU WAKIFA NA KUPOTEZA MALIZAO NA KUHAMA NCHI ZAO BILA MSAADA WOWOTE .
KISHA VITA VYA 1994 AMBAVYO VIMEWAUA WATU ZAIDI YA MILIONI, AFRICA NA DUNIA ZILISHUHUDIA. CHAKUSHANGAZA JESHI LA UMOJA WA MATAIFA UN TROOPS WALIKUWEMO NDANI YA RWANDA WAKAWEZA KURUHUSU MAUAJI YA WATU ZAIDI YA MILIONI KUFA NDANI YA MIEZI MITATU.
MIEZI HII MITATU ILIKUWA MIEZI YA MACHUNGU,VIFO,NJA,KIU, ULEMAVU WA KILA AINA,KUBAKWA, KUDHALILIKA …….N.K. HALI HIO ILIKUWA NI NGUMU NA KILA MTU MWENYE TV ALIKUWA AKISHUHUDIA, NA WENGINE WAKIANGALIA KOMBE LA DUNIA KANA KWAMBA MAUAJI YA RWANDA HAYAMHUSU KILA MWAFRICA NA WAPENDA AMANI WENGINE DUNIANI.
JESHI LA UMOJA WA MATAIFA LILISHINDWA KUWAOKOA WANYARWANDA. NA KWASASA WALIOHUSIKA KATIKA MAUAJI HAYO, KESI ZAO ZINACHUKUWA MIAKA KIBAO NA HUKU WAKIISHI MAISHA MAZURI. NILAZIMA AFRICA IAMKE ITAMBUWE KWAMBA UKABILA,RANGI NA DINI SIO SABABU YA KUANGAMIZANA JAMBO LA MSINGI NI KUVUMILIANA NA KILA MTU KURIDHIKA NA UMBILE LA MWENZIE , ILI TUJENGE NCHI ZETU NA NAFIKIRI AMANI NA UTULIVU VITATAWALA NA KILA MWANACHI WA AFRICA ATAJIVUNIA UAFRICA WAKE. VIJANA WENGI WA KIAFRICA WAKO ULAYA, MAREKANI,ASIA WANAHANGAIKA KILA KUKICHA NAWENGINE WAKIOGOPA KURUDI KATIKA NCHI ZAO WAKIKHOFIA VIFO VYA UKABILA NA MAPINDUZI YA KIJESHI YASIOANGALIA UTU WA MASIKINI. HUU NI MDA WA KILA MSOMI WA AFRICA, KUTUMIA ELIMU YAKE,ILI AOKOE DAMU ZA WATOTO WA KIAFRICA, SIO KUWAINGIZA KWENYE SIASA ZA KUANGAMIZANA NA KUAMBUKIZA CHUKI BAINA YA MAKABILA,DINI NA KOO.
JE IKIWA DUNIA INAWATAKIA , AMANI WANACHI WA RWANDA MBONE WAKIMBIZI WENGI WAMECHUKULIWA NA KUPELEKWA MAREKANI,CANADA,………N.K. KWANINI WASIRUDISHWE KATIKA NCHI ZAO!
NJIA HII BADO WATU WA NCHI TAJIRI WANATUPA WASIWASI KUHUSU HATIMA YA AFRICA.
KUMBUKA KWAMBA KUNA WANAJESHI WA KIHUTU BADO WAKO NDANI YA MSITU WA KONGO ! JE KIPI KIFANYIKE ILI KUEPUSHA MZUNGUKO WA MWAKA 1959 NA 1994 ?
NI KUANGAMIZA JESHI LA ZAMANI LA WAHUTU LILILOKO KONGO PAMOJA NA NDERAHAMWE ? JE WAHUTU , WATWA NA WATUTSI WALIOKO RWANDA WANA IMANI JUU YA USALAMA WA NCHI YAO KWA SASA ? JE MTAZAMO WA WAKIMBIZI WA RWANDA WALIOKO NJE YA NCHI YAO UKOJE ?
JE! IKIWA CHANZO CHA MAUAJI YA RWANDA NI KIFO CHA RAISI WA RWANDA, NANI ALIE HUSIKA NA KIFO CHAKE ?
KILA MTU MWENYE ELIMU ANAJUA KWAMBA NDEGE INAPODODOKA , KUNA KIBOX KINACHITWA BLACK BOX, KINAHIFADHI SIRI NYINGI ZIKIWEMO SAUTI , JE ! SANDUKU HILO LIKO WAPI?
UFARANSA NA RWANDA HUTUPIANA MANENO KILA KUKICHA , KILA UPANDE UKIMSHUTU MWINGINE KWAMBA ALIHUSIKA NA VIFO VYA MARAISI WA RWANDA NA BURUNDI NA WATU WENGINE. JE! MHUSIKA NI NANI?
JE! IKIWA WAFRICA WANAPENDANA WAMEWEZAJE KUONYESHA USHIRIKIANO WAO NA WANACHI WA RWANDA KATIKA KUKEMEA MAUWAJI HAYO YASITOKEE TENA.
TANZANIA INAHITAJI PONGEZI KUBWA KWA KUONYESHA UJASIRI WAKUWAWEKA PAMOJA WATU HAWA ( WAHUTU NA WATUTSI ) ILI KUSURUHISHA TAFAUTI ZAO BILA KUMWAGA DAMU ZAIDI. KUMBUKA KWAMBA NDEGE YA MARAISI HAO,ILIANGUSHWA IKIWA IMETOKA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA AMANI BAINA YA WAHUTU NA WATUTSI.
KIPI KIFANYIKE ILI AMANI YA KUDUMU IWEPO NDANI YA NCHI YA RWANDA NA KILA MTU AKIISHI KWA AMANI SIO KUISHI KWA MASHAKA.
EWE MUNGU UWEZO WAKO NA NGUVU ZAKO NI MUHIMU KWETU SISI TUNAKUHITAJI KUUNGA NYOYO ZETU NA KUTUEPUSHA NA UBAGUZI WA DINI, KABILA NA RANGI. YOTE HAYO UMEAUMBA WEWE KWA LENGO LA KUFAHAMIANA LAKINI KUNA WANA SIASA NA NCHI TAJIRI ZINATUMIA NJIA HII KAMA MRIJA KUTUNYONYA DAMU MUNGU TUNAKUOMBA UTUWEKEE ULINZI WA DAMU YAKO SISI WANYONGE.
AMEN
mtazamo wa mavazi katika Quran na Biblia
MAVAZI
Vazi ni kifaa ambacho kinasitiri mwili wa binaadamu. Binaadamu mwenye akili timamu, lazima ajue jinsi ya kuhifadhi mwili wake Katika hali ya stara. Mavazi ni mojawapo wa msingi wa kusitiri mwili wa binaadamu. Binaadamu anapovaa nguo, anajihisi kama yuko huru nafsini mwake. Binaadamu anaweza kukosa uhuru kutokana na mavazi alioyavaa. Mara nyingine binaadamu anaweza kupata heshima au kukosa heshima kutokana na mavazi aliovaa.
Baadhi ya binaadamu wanaamini ya kwamba, thamani ya mtu inatokana na thamani ya mavazi yake, na mara nyingine mtu anakosa ukaribisho salama katika majumba ya watu, maduka, kundi la watu, ………..n.k.
Kama tunavyoelewa kila binaadamu anatabia ya kipeke. Tabia ya kipekee ya binaadamu inatokana na elimu, macho, moyo, masikio na pua vya nafsi husika.
MUNGU ALIMWEKEA BINAADAMU, MWONGOZO WA MAVAZI, NATARATIBU ZAKE KATIKA JAMII NA ULINZI WENYE HESHIMA YA MWILI WAKE.
QURAN :
NA WAMBIE WAISLAMU WANAWAKE WAINAMISHE MACHO YAO, NA WAZILINDE TUPU ZAO,WALA WASIZIHIRISHE VIUNGO VYAO ISIPOKUA VINAVYODHIHIRIKA ( NAO NI USO NA VITANGA VYA MIKONO ) NA WAANGUSHE SHUNGI ZAO MPAKA VIFUANI MWAO, NA WASIONYESHE MAPAMBO YAO ILA KWA WAUME ZAO, AU WATOTO WAO AU WATOTO WA WAUME ZAO AU WANA WA KAKA ZAO AU WANA WA DADA ZAO AU WANAWAKE WENZIWAO, AU WALE ILIYOWAMILIKI MIKONO YAO YA KUUME ( WATUMWA WAO ) AU WATOTO AMBAO HAWAJAJUA MAMBO YANAOHUSU UKE.
WALA WASIPIGE MIGUU YAO ILI YAJULIKANE WANAYOYAFICHA KATIKA MAPAMBO YAO. NA TUBIENI NYOTE KWA MWENYEZI MUNGU, ENYI WAISLAMU ILIMPATE KUFAULU”.
(24:34).
MWENYEZI MUNGU ANATUHIMIZA NA KUTUFUNDISHA JINSI YA KUHIFADHI MIILI YETU. BINAADAMU WAMEUMBWA KATIKA JINSIA MBILI (MWANAMUME NA MWANAMKE). MWANAMKE UMBILE LAKE NI LENYE KUVUTIA, HASA KWA WANAUME.
BAADHI YA WANAUME WASIO KUWA NA ELIMU YA KUJIHIFADHI, HUVUTIWA SANA NA VIUNGO VYA MWANAMKE, HASA VINAPOONEKANA.
NA KUNA BAADHI YA WANAWAKE WENYE KUVUTIWA NA VIUNGO FULANI VYA WANAUME, HALI HII HULETA UTATA KATIKA NAFSI YA MWANAMKE HUSIKA.
NI LAZIMA KILA MWANAMKE HAIFADHI TUPU ZAKE, AJIEPUSHE NA ZINAA. AWE MUAMINIFU KWA MME WAKE NA IKIWA HAJAOLEWA ABAKI NA UBIKIRA WAKE.UBIKIRA WA MWANAMKE NI ZAWADI KWA MUMEWE NA NI IBAADA KWA MUNGU. ASILIMIA KUBWA YA WANAWAKE WA KARNE YA SASA MTIHANI HUU ( WAZINAA ) UMEWASHINDA NA THAMANI YAO INASHUKA KILA KUKICHA. NDOA HALALI ZIMEPUNGUA NA WAZAZI WAMESHINDWA KUZIBITI HALI HII.
KAWAIDA YA ASILI YA MWANAMKE , ANA AIBU ASILIMIA TISINI ( 90 % ) NA MWANAUME ASILIMIA KUMI TU ( 10 % ) . NDIO MAANA MWANAMKE SIO RAHISI KUMTONGOZA MWANAMUME. LAKINI KWA KARNE YA SASA WANAWAKE WENGI WAMETOKWA NA AIBU. WANAWAKE WANAVAA NGUO ZENYE KUONYESHA MAUNGO YAO BILA KUJALI MATAMANIO YA WANAUME JUU YAO. WANAWAKE HAO WANAJIITA WANAWAKE WA KISASA, AMBAO WANAENDANA NA MITINDO YA MAVAZI. HUU NI UVUNJAJI WA SHERIA ZA MUNGU KWA WALE WANAWAKE AMBAO WANAAMINI KUWA WANA DINI.
MWANAMKE AMERUHUSIWA KUVAA MAPAMBO LAKINI KAWEKEWA MPAKA NA MUNGU, ILI ASIJE AKASABABISHA MATAMANIO KWA WANAUME.
KWAMUJIBU WA AYA HII, NI LAZIMA KILA MWANAMKE WA KIISLAMU AJISITIRI, KWA KUANGUSHA USHUNGI WAKE HADI MABEGANI. KUNA BAADHI YA WANAWAKE WACHAMUNGU, AMBAO WANAFUATA SHERIA ZA MWENYEZI MUNGU BILA KUJALI SIFA ZA BINAADAMU WENZAKE AU HOFU YA KUFUKUZWA KAZI, KUKOSA MCHUMBA, KUONYESHA WATU VIUNGO VYAKE ANAVYOHISI KWAMBA VINAVUTIA, KUONYESHA THAMANI YA MAPAMBO YAKE NJIANI AU KWA WALE WATU ANAO WAZIDI UWEZO………..N.K.
KILA MWANAMKE ANAPENDA AWE NA MWANAUME MZURI NA MWENYE TABIA NJEMA, LAKINI TATIZO LINAJITOKEZA PALE AMBAPO MALALAMIKO YA NDOA YAMEZIDI KUWA MENGI NA HUKU ZINAA NA UASHERATI UKIZIDI KILA KUKICHA.
IKIWA MWANAMKE ANAHITAJI MWANAMUME MZURI WA SURA NA TABIA ATAMPATA , PALE AMBAPO NA YEYE ATAKUWA NASIFA HIZO ( ZA UZURI WA SURA NA TABIA AU TABIA TU INAWEZA KUMPA MWANAMKE AU MWANAMUME SURA ZURI NA TABIA BILA KUTEGEMEA ).
TUNAENDELEA KUANGALIA MTAZAMO WA MAVAZI, KUTOKA KATIKA KITABU CHA BIBLIA.
BIBLIA
BASI NATAKA WANAUME WASALISHE KILA MAHALA HUKU WAKIINUA MIKONO ILIOTAKATA, PASIPO HASIRA WALA MAJADILIANO. VIVYO HIVYO WANAWAKE NA WAJIPAMBE KWA MAVAZI YA KUJISITIRI, PAMOJA NA ADABU NZURI , NA MOYO WA KIASI , SI KWA KUSUKA NYWELE WALA KWA DHAHABU NA LULU , WALA KWA NGUO ZA THAMANI. BALI KWA MATENDO MEMA, KAMA IWAPASAVYO WANAWAKE WAOUKIRIO UCHAJI WA MUNGU. MWANAMKE NA AJIFUNZE KATIKA UTULIVU, AKITII KWA KILA NAMNA. SIMPI MWANAMKE RUHUSA YA KUFUNDISHA, WALA KUMTAWALA MWANAMUME BALI AWE KATIKA UTULIVU KWA MAANA ADAMU NDIE ALIYEUMBWA KWANZA, NA HAWA BAADAE.
(TIMOTHEO 2: 7……..14)
HUO NDIO MTAZAMO WA BIBLIA JUU YA MAVAZI. KUMBUKA YA KWAMBA IKIWA UNAAMINI KWAMBA ULIUMBWA NA MWENYEZI MUNGU, HUNA BUDI YA KUFUATA SHERIA ZAKE. BINAADAMU WANATAFAUTIANA KIMAWAZO, KUNA BAADHI YA BINAADAMU WANAOPINGA UKWELI WA MAMBO AU SHERIA ZA MUNGU KUTOKANA NA KULINDA FAIDA ZA NAFSI ZAO. WATU HAO HATA UKIWAAMBIA YA KWAMBA VIUNGO FULANI VYA MWANAMKE AU MWANAUME VINA MCHANGO MKUBWA WA KUVUNJA NDOA NA KUONGEZA MARADHI YA UKIMWI, WAO HAWAPO TAYARI KUKUBALIANA NA WEWE LICHA YA KUWA WANA SHUHUDIA NA KUSIKIA KWENYE VYOMBO TOFAUTI VYA HAPA DUNIANI. KUMBUKA KWAMBA KILA MTU MZINIFU AU MKAA UCHI , HAYUKO TAYARI KUKUBALI KUONA VITU HIVYO VINAONDOKA DUNIANI , SABABU NDIVYO VITU ANAVYOVITEGEMEA KUMPA UMAARUFU, RIZIKI NA STAREHE KIDOGO ZA MAISHANI.
KUNA BINAADAMU WENGINE, AMBAO NI WACHA MUNGU, WATU HAO UNAPOWAKUMBUSHA KUHUSU UBAYA WAJAMBO HUSIKA , WAO HUA NI WEPESI WA KUACHANA NA FAIDA KIDOGO ZA JAMBO HUSIKA NA KUELEKEA KATIKA NJIA YA TOBA. MWENYEZI MUNGU NI MPOLE NA NI MWEPESI WA KUWASAMEHE WAJA WAKE WANAPOMRUDIA.
WACHA MUNGU WANAWAKE, ALAMA YAO NI AIBU NA MAVAZI YAO HUWA NI YENYE KUHIFADHI VIUNGO VYAO. KUMBUKA YA KWAMBA NYAMA ILIO WEKWA WAZI, HUJAWA NA NZI , NA NYAMA ILIOWEKWA NDANI YA MFUKO IMEHIFADHIKA. INZI HUZUNGUUKA ULE MFUKO WAKIPIGA KELELE ILI , MWENYE MFUKO AOGOPE AFUNGUWE,KISHA WASHAMBULIE ILE NYAMA WAONDOE THAMANI YAKE AU WAPUNGUZE THAMANI YAKE. HALI HII HATARI IMEANZA DUNIANI JUU YA WANAWAKE WA KIISLAMU, WANALAZIMISHWA AU KUHAMASISHWA NA WATU WENYE KUASI AMRI ZA MUNGU, ILI WASIVAE MAVAZI YAO YA HESHIMA ,WAANZE KUVAA VIMINI NA VITOPU VYA WANAWAKE WA KISASA.HUO SIO UNGWANA NA SIO HAKI JUU YA WANAWAKE WACHA MUNGU WA KIISLAMU.
HALI HII TUMEISHUHUDIA UTURUKI,UFARANSA NA KATIKA NCHI NYINGINE WANAWAKE HAO WAMEPEWA MAJINA YA BANDIA KAMA NINJA, SIASA KALI, FICHO LA MALAYA ……N.K.
HAYO NI MAMBO YA KAWAIDA JUU YA JAMBO LA KHERI. HAKUNA JAMBO ZURI LISILOKOSA UPINZANI, HATA MITUME WA MWENYEZI MUNGU WALIKUMBANA NA VIFO,KUNYANYASWA,KUFUNGWA, KUUWAWA…….N.K.
HABARI NJEMA KWA WANAWAKE WOTE WANAOFUATA MAANDIKO, KUWENI NGANGARI, NA MWENYEZI MUNGU ATAWASAIDIA.
IKIWA WEWE MWANAMKE UNA DINI YAKO , NA DINI YAKO INA MAVAZI YENYE HESHIMA, BASI NI VIZURI KWAKO UYAVAE NA KISHA UONYESHE WANAWAKE WENZIO ULIVYOPENDEZA NA KAZI ZAKO UNAZIFANYA KAMA KAWAIDA.USIJE UKASEMA YA KWAMBA WEWE NI MWENYE DINI NA UNAMWOGOPA MWENYEZI MUNGU LAKINI UNASHINDWA KUTII AMRI ZAKE ZA KIMAVAZI UKIWA UNAJUA.
KWA KUMALIZA MWENYEZI MUNGU ANASEMA HIVI, KATIKA QURANI:
QURANI
JE! ANAYEKWENDA AKISINUKIA KWA USO WAKE NI MUONGOFU, AU ANAYEKWENDA SAWASAWA KATIKA NJIA ILIONYOKA ?
(67: 22)
SEMA : “ YEYE NDIYE ALIYEKUUMBENI NA AKAKUPENI MASIKIO NA MACHO NA NYOYO.” NI KIDOGO KABISA SHUKURANI YENU.
(67: 23)
BIBLIA
KUSIKIA MTASIKIA, WALA HAMTAELEWA; KUTAZAMA MTATAZAMA, WALA HAMTAONA, MAANA MIOYO YA WATU HAWA IMEKUWA MIZITO, NA KWA MASIKIO YAO HAWASIKII VYEMA, NA MACHO YAO WAMEYAFUMBA; WASIJE WAKAONA KWA MACHO YAO, WALA KUSIKIA KWA MASIKIO YAO, WAKAONGOKA KWA MIOYO YAO , WAKAONGOKA NIKAWAPONYA.
(MATHAYO MTAKATIFU 13: 14…..15)
AMINA.
Friday, April 10, 2009
Mambo ya Ndala
Mambo ya Ndala
Jamani naomba niulize kuhusu ndala, je ndala inafaa kuvaliwa wapi? Inafaa kuvaliwa na vazi gani? Inafaa kuvaliwa na mtu wa hadhi gani? Inafaa kuvaliwa kwa kwenda wapi? Je ndala iligunduliwa na nani? Maana tujuavyo ndala utumika sana kwa wakati wa faragha ama mapumziko pia ndala ni kiatu cha mnyonge asie na kipato anaweza kutembea nacho kwa muda mrefu na kinadumu kwa muda mrefu pia! Kwetu sisi ndala ni mkombozi wa wanyonge! Na ndala ndio nembo ya time yetu Yanga bingwa wa ligi kuu ya Vodacom je kwanini Yanga walichagua alama ya ndala kama ujulisho wa timu yao? Je twaweza kuoga na viatu vya ngozi ama laba? Basi sina budi kuipa sifa ndala kwa jinsi ilivyo na umuhimu katika maisha yetu ya kila siku!
Subscribe to:
Posts (Atom)