KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, April 30, 2009

HOFU YA TANDA KATIKA NYOYO ZETU LEO NA MATUMAINI YETU YA MAISHA TUMEMWACHIA MUNGU






Dar yawaka Moto leo!
Kwa wakazi wa jiji la Bongo leo ilikuwa ni siku ya hofu tele! Kwani mitaa ya mbagala kulikuwa na Mabalaa ya hatari sana! Kwa habari tulizopata ni kuwa mabomu kibao yamelipuka na kusababisha matatizo na vifo kwa wakazi waishio karibu na maeneo ya karibu. Kwa watu wafanyao kazi pale mjini mitikisiko ya mabomu hayo yalitosha kuwafanya waachie ofisi zao na kukimbia ovyo bila mpango, redio nazo hazikuwa nyuma katika kutoa taarifa kinzani kuhusu tukio zima!
Kwa kifupi unaweza pata picha kuwa jiji letu halina mpango maalumu kuhusu majanga mbalimbali yanayoweza kutokea katika jamii! Hatajajitayarisha ya kutosha kwa maafa ya aina mbalimbali kama vile moto, umeme, mafuriko, na majanga mengineyo mengi! Tukiola leo ni somo tosha kwa wakuu wetu ni jinsi gani twaweza kujipanga kwa athari zozote zinazoweza kutokea kwetu wakati wowote ule. Mfano ni jinsi gani sehemu hatari kama maghala ya silaha kali za jeshi zinavyoweza kuweka katika mazingira yasiyo salama kama ilivyotokea leo! Nadhani hili ni fundisho tosha wakuu wetu kupanga jinsi gani twaweza kuepuka na majanga kama haya.
Pia kwa watoa huduma za mtandao, kwani kwa muda mrefu wamekuwa hodari kwa kututumia meseji kuhusu promosheni zao ila leo kwa ajabu mitandao yao ilikwenda off! Sasa waweza kujiuliza ikiwa mitandao iko off na una ndugu ama jamaa yako huko itakuwaje!

No comments:

Post a Comment