KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Friday, April 17, 2009
BARUWA KWA MATAJIRI WOTE DUNIANI
BARUA KWA MATAJIRI WENYE IMANI YA KUWEPO MUNGU
TUNAONGONZWA NA NENO LA MUNGU NDANI YA QURAN NA BIBLIA
KILA BINAADAMU MWENYE AKILI TIMAMU, HANA BUDI YA KUKIRI KWAMBA KUNA MUUMBA WA MBINGU NA ARDHI NA VILIVYOMO. HAKUNA KIUMBE KISICHOSHUHUDIA MAZINGIRA YA AJABU NA YENYE KILA AINA YA UZURI . KILA KIUMBE MUNGU ALIKIUMBA NA AKAKITENGENEZEA UTARATIBU WA MAISHA YAKE HAPA ULIMWENGUNI NA NDIO MAANA TUNAANZA ( KUZALIWA ) TUNAISHI, KATIKA MIKAKATI NA KILA MTU AKIWA NA LENGO FULANI KATIKA MAISHA YAKE, LAKINI MWISHO WA MAMBO ( UHAI ) TUNAJIKUTA MDA WETU WA MAISHA UNAISHA BILA KUFIKIA LENGO AU KUFIKIA LENGO, NA KUANZISHA LENGO LINGINE. IKIWA BINAADAMU ANAAMINI KWAMBA ALIUMBWA NA MUNGU, AKAMPA UHAI NA MAISHA BORA, NI WAJIBU KWAKE KUMTANGULIZA KATIKA KILA JAMBO LILILOPITA, LILIOPO NA LIJALO. LAKINI UTAKUTA WATU MASIKINI NA MAFUKARA MARA NYINGI NDIO WENYE KUWA KARIBU NA MWENYEZI MUNGU. BAADHI YA MATAJIRI , HUJIKUTA KATIKA MAPAMBANO YA KUONGEZA KIPATO CHAO BILA KUWA NA HISIA ZA KUMTANGULIZA MWENYEZI MUNGU, MARA NYINGINE HUWEZA ( MATAJIRI ) KUTAMKA YA KWAMBA PESA NA MALI ZAO, WAMEZIPATA KUTOKANA NA UWEZO WAO WA KIAKILI. BAADHI YA MATAJIRI, ASILIMIA KUBWA YA MALI ZAO HUWA NI ZENYE KASORO YA UHALALI ( DHULMA ). DHULMA HIO HUWAKUMBA WATU MASIKINI, KWA KUDHULUMIWA MALI ZAO, HAKI YA MANENO AU VITENDO , HESHIMA , ELIMU……N.K. UDHAIFU WA MASIKINI MARA NYINGI UNATOKANA NA UPUNGUFU WA ELIMU JUU YA JAMBO HUSIKA AU KUKANDAMIZWA NA FEDHA AU NGUVU ZA TAJIRI HUSIKA. JAMBO HILI HALIJAANZA LEO AU JANA , BALI LILIANZA MIAKA MINGI ILIOPITA.
TUKIANGALIA MAANDIKO YA MUNGU ANAVYOSEMA JUU YA MATAJIRI HAWA, TUTAKUTA WANA MTIHANI MGUMU JUU YA MASIKINI,FUKARA ,YATIMA NA WAJANE.
BIBLIA
HAYA BASI, NINYI ( MATAJIRI ) MSEMAO, LEO AU KESHO TUTAINGIA MJI FULANI NA KUKAA HUMO MWAKA MZIMA, NA KUFANYA BIASHARA NA KUPATA FAIDA. WALAKINI HAMJUI YATAKAYOKUWAKO KESHO.
UZIMA WENU NI NINI? MAANA NINYI NI MVUKE UONEKANAO KWA KITAMBO, KISHA HUTOWEKA. BADALA YA KUSEMA BWANA ( MUNGU AKIPENDA ), TUTAKUWA HAI NA KUFANYA HIVI NA HIVI. LAKINI SASA MWAJISIFU KATIKA MAJIVUNO YENU ; KUJISIFU KOTE KWA NAMNA HII NI KUBAYA. BASI YEYE AJUAYE KUTENDA MEMA , WALA HAYATENDI , KWAKE HUYO NI DHAMBI. (WARAKA WA YAKOBO 4: 13……17)
* HAPO JUU, TUNAELEZWA KWAMBA MAISHANI LAZIMA MUNGU APEWE KIPAOMBELE. LAZIMA KILA MWANADAMU, ANAPOKUWA NA MPANGO WOWOTE, AOMBE MUNGU UZIMA KWANZA NA KISHA AMSHIRIKISHE KATIKA HARAKATI ZAKE ZA KUTAFUTA RIZIKI YA HALALI. LAZIMA KILA BINAADAMU ATAMBUWE KWAMBA MAISHA NI KAMA MVUKE LEO UPO KESHO HAUPO, NA JINA LAKO HUBADILIKA NA KUITWA MAREHEMU. MALI, MKE WATOTO,PESA,NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI HATA ADUI ZAKO WOTE HUBAKI DUNIANI WAKISIKITIKA NA WENGINE WAKIFURAHIA KIFO CHAKO.
IKIWA WEWE NI TAJIRI NA UNAAMINI KWAMBA KILE ULICHO NACHO UMEKIPATA KUTOKANA NA UWEZA WA MUNGU, BASI NIWAJIBU WAKO KUFUATA UTARATIBU WA MAELEKEZO YA KITABU CHAKO KUHUSU HAKI YA MASIKINI, YATIMA,WAJANE, WAFUNGWA , NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI KUHUSU MALI YAKO, NA UKIWA HUNA UWEZO HUO BASI MUNGU YUKO PAMOJA NAWE.
QURANI
KWA YAKINI WALE WANAOSOMA KITABU CHA MWENYEZI MUNGU, NA WAKASIMAMISHA SALA , NA KATIKA YALE TULIOWAPA WAKATOA KWA SIRI NA KWA DHAHIRI , HAO WATATUMAI BIASHARA ISIO DODA ( ISIYOBWAGA ) ( 35 : 29 )
NIWAJIBU JUU YA KILA BINAADAMU , KUSOMA KITABU CHA MWENYEZI MUNGU, ILI KUONGEZA UJUZI NA HEKIMA. MUNGU ALILETA VITABU, VINGI AMBAVYO NI TORATI, ZABURI, INJIRI NA QURAN. VITABU HIVYO VYOTE VINA MAFUNDISHO YANAYOONESHA UTUKUFU WA MUNGU , LICHA YA KUWA KUNA BAADHI YA BINAADAMU WANAO KIUKA AMRI NA SHERIA ZA VITABU HUSIKA NA MARA NYINGINE HUWA NA UBAGUZI WA VITABU KUTOKANA NA MASLAHI YA NAFSI ZAO. KILA KITABU CHA MUNGU KINAFUNDISHA MAADILI NA MFUMO WA MAISHA. KUMBUKA YA KWAMBA KILA KITABU KINA MSAADA JUU YA KINGINE, NA MAFUNDISHO YAKE YOTE YANAHUSU HAKI NA UTUKUFU WA MUNGU.
KUSIMAMISHA SALA ( IBAADA ), NI JAMBO MUHIMU NA NILAZIMA KWA KILA MWANADAMU MWENYE AKILI TIMAMU ,NAKUAMINI YA KWAMBA YEYE NI KIUMBE WA MUNGU NA HANA BUDI YA KUMSHUKURU MUUMBA WAKE. IBAADA NI MAWASILIANO BAINA YA MWENYEZI MUNGU NA VIUMBE WAKE. IBAADA INAMFANYA MTU AEPUKANE NA MAMBO MENGI YA ANASA NA KUWA KARIBU YA MUNGU. IBAADA INAMWEZESHA MTU ,KUMTANGULIZA MUUMBA WAKE KATIKA KILA JAMBO.IBAADA INAMFANYA MTU AWEZE KUWA JASIRI JUU YA MAISHA MAGUMU YANAYO MKABIRI, KUTOKANA NA IMANI YA MFANYA IBAADA, YAKUAMINI KWAMBA MTOA RIZIKI NI MUNGU PEKE YAKE. IBAADA INAMFANYA MTU AWE NA HURUMA JUU YA VIUMBE WENZAKE NA KUWA NA MOYO WA KUWA SAIDIA. IBAADA INAMFANYA MTU AWEZE KUWA NA AIBU, SIFA YA IMANI JUU YA MWANADAMU NI AIBU. UKOSEFU WA AIBU KATIKA MAISHA NDIO CHANZO CHA MAAFA YOTE ULIMWENGUNI.
BAADHI YA MATAJIRI WANAAMINI KWAMBA KUSALI KUNAWAPOTEZEA MDA WA KUSAKA MAPESA. NA MARA NYINGINE MATAJIRI WANAWAZUIA WAJIRIWA WAO, KUSALI AU KUWAPA SEHEMU YA IBAADA KATIKA OFISI ZAO. MATAJIRI WALIO WENGI WANAAMINI YA KWAMBA MDA WA IBAADA NI PUNGUZO LA MAPATO YAO.
UKIAJIRIWA NA TAJIRI KAMA HUYO, LAZIMA UKUBALIANE NA KUKAIDI AMRI YA MUNGU KUHUSU IBAADA YA SALA.
HUU NI MTIHANI WA MATAJIRI JUU YETU MASIKINI!
KUBALI MSHAHARA AU KUMWASI MWENYEZI MUNGU!
KUTOKANA NA MATAJIRI WENGI KUONA KWAMBA SALA , INACHUKUWA MDA WAO WA KIUCHUMI, NDIO MAANA OFISI NYINGI DUNIANI ZIMEPUNGUZA MDA WA MAPUMZIKO WA CHAKULA CHA MCHANA NA KAMPUNI NYINGINE KULA UTAJIJUA NA UKIZUBAA UTAIBIWA NA UTAWAJIBISHWA NA SHERIA KWA KUTOKA SEHEMU YAKO YA KAZI. HUU NI MTINDO WA ULINZI WA MATAJIRI JUU YA MALI ZAO. UTU UNAONDOKA BINAADAMU TUNAINGIZWA KATIKA MFUMO WA MAGEUZI , AMBAO NI VUNJA AMRI YA MUNGU UPATE MKATE AU UNASEMAJE ?
* MWENYEZI MUNGU ANAWAHIMIZA WATU WENYE UWEZO, KUWASAIDIA BINAADAMU WENZAO BILA KUTUMAINI FADHILA YA SHUKURANI KUTOKA KWA WASAIDIWA. MUNGU ANATUHAMASISHA KUHUSU HURUMA NA KUSAIDIANA KATIKA HALI NA MALI. USIMSAIDIE BINAADAMU MWENZAKO ILI UONEKANE KAMA NI MTOAJI AU UNA HURUMA MACHONI MWA WATU, KUMBE MOYONI HUNA HURUMA NA MOYO WA KUSAIDIA MASIKINI,YATIMA,WAJANE NA ……….N.K. UKITOA UNAWEKA AKIBA YA BAADA YA UHAI WAKO.UNAPOTOA MALI YAKO KUMPA MHITAJI, TAYARI MWENYEZI MUNGU ANAKUPA MALIPO YANAOITWA THAWABU. THAWABU NI MALIPO YENYE THAMANI KUBWA , KUMBUKA KWAMBA WINGI WA THAWABU NDIO KUJISHINDIA NAFASI YA KWENDA
PEPONI.
* MWENYEZI MUNGU ANAWAPA TAARIFA NJEMA NA FARAJA KWA MATAJIRI, YA KWAMBA WASIWE NA KHOFU YA KUWASAIDIA WATU, MUNGU ANAWAPA OFA MATAJIRI YA KWAMBA ATALINDA BIASHARA ZAO NA WATAKUWA NA FURSA NZURI YA KUPATA THAWABU NYINGI. NA KUMBUKA WINGI WA DHAWABU NDIO TIKETI YA PEPONI.
KIFO CHA MATAJIRI BAHIRI NA HATIMA YA MALI ZAO
BIBLIA
HAYA BASI, ENYI MATAJIRI! LIENI, MKAPIGE YOWE KWASABABU YA MASHAKA YENU YANAYOWAJIA. MALI ZENU ZIMEOZA, NA MAVAZI YENU YAMELIWA NA NONDO. DHAHABU YENU NA FEDHA YENU ZIMEINGIA KUTU , NA KUTU YAKE ITAWASHUHUDIA , NAYO ITAKULA MIILI YENU KAMA MOTO. MMEJIWEKEA AKIBA KATIKA SIKU ZA MWISHO. ANGALIENI, UJIRA WA WAKULIMA WALIOVUNA MASHAMBA YENU, NINYI MLIOUZUIA KWA HILA, UNAPIGA KELELE , VILIO VYAO WALIOVUNA VIMEINGIA MASIKIONI MWA BWANA ( MUNGU ) WA MAJESHI. MMEFANYA ANASA KATIKA DUNIA , NA KUJIFURAHISHA KWA TAMAA,MMEJILISHA MIOYO YENU KAMA SIKU YA MACHINJO. MMEHUKUMU MWENYE HAKI MKAMWUA; WALA HASHINDANI NANYI. (WARAKA WA YAKOBO 5: 1……6)
QURAN
ADHABU KALI ITAMTHUBUTIKIA KILA MWENYE KURAMBA KISOGO, MSENGENYAJI. AMBAYE AMEKUSANYA MALI NA KUYAHISABU ( TU BILA YA KUYATUMIA KATIKA NJIA YA KHERI ).
ANADHANI YA KUWA MALI YAKE YATAMBAKISHA MILELE.
HASHA! BILA SHAKA ATAVURUMIZWA KATIKA (MOTO UNAOITWA) HUTAMA.
NA NI JAMBO GANI LITAKALO KUJULISHA (HATA UKAJUA) NI NINI (HUO MOTO UNAOITWA) HUTAMA?
NI MOTO WA MWENYEZI MUNGU ULIOWASHWA (KWA UKALI BARABARA).
AMBAO UNAPANDA NYOYONI.
HAKIKA HUO (MOTO) WATAFUNGIWA (WAWEMO NDANI YAKE).
KWA MAGOGO MAREFU MAREFU.
(SURATUL HUMAZAH)
QURAN
JE! HAWAJUI YA KWAMBA MWENYEZI MUNGU ANAPOKEA TOBA YAWAJA WAKE NA KUZIPOKEA SADAKA , NA YA KWAMBA MWENYEZI MUNGU NI MWENYE KUKUBALI TOBA SANA ( NA ) MWENYE REHEMA ?
(9: 104)
HAYA HAYA MATAJIRI ,HUU NI WAKATI WENU WA KULA MBIVU AU MBICHI. TAYARI VITABU VYA MWENYEZI MUNGU VINATOA AU VINAONYESHA NJIA ZA KUPITA NA NI RAHISI KWA WAMCHAO MUNGU.
KUNA MSEMO, USEMAO KAMA IFUATAVYO:
MMEPEWA MACHO HAMUONI!
NI NINI MAANA YA MACHO? MACHO NI CHOMBO AMBACHO,MWENYEZI MUNGU AMEMPA MWANADAMU ILI AWEZE KUONA KITU KIBAYA NA KIZURI PAMOJA NA KUANGALIA NEEMA AU UWEZO WA MUNGU KATIKA KUUMBA NA KUSHUKURU NEEMA ZAKE JUU YAKE ( BINAADAMU ). MACHO YANA UWEZO WA KUONA MAHITAJI,MATESO,MAUAJI,WIZI,UZIZI,UGOMVI,FITNA LAWAMA,HUSUDA,CHAKULA,UPENDO……N.K.
NI WAJIBU JUU YA KILA MWENYE JICHO, KUSHUHUDIA NA KUKEMEA MABAYA NA KUSIFIA NA KUSHUKURU MAZURI AYAONAPO.
MNA MASIKIO HAMSKII!
NI NINI MAANA YA MASIKIO?
MASIKIO NI CHOMBO, AMBACHO BINAADAMU ANAKITUMIA KATIKA HARAKATI ZAKE ZA KUINGIZA SAUTI NA NENO KWENYE NAFSI AU NDANI YA NAFSI HUSIKA. KILA MTU MWENYE NAFSI YA KUNASA SAUTI, JAMBO HILI LINAMHUSU, NA NIMUHIMU KABISA KATIKA MAISHA YAKE.
BABA AKIAMBIWA KWAMBA NI MARUFUKU KUTOKA NJE USIKU. TAYARI UJUMBE UMEFIKA KATIKA KILA NAFSI ILIYOMO NDANI. IKIWA MZAZI (BABA) ATAMTUMA MWANAE NJE KUWASHA SIGARA JIKONI,AKIMPA MATUMAINI KWAMBA SIMBA HAYUPO KARIBU. MTOTO AKIKUMBWA NA KIFO CHA SIMBA BASI,TATIZO HILO LITAKUWA NI KUBWA NA LENYE KULETA MGAWANYIKO KATIKA FAMILIA. WATOTO WALIOBAKI WATAMCHUKIA BABA NA MKE WAKE ATAMCHUKIA MME WAKE NA MAJIRANI WATAMUONA HUYO MZAZI ( BABA MTU ) KAMA MTU MWENYE MATATIZO YA AKILI, NA ATAHUKUMIWA KISHERIA KWA KOSA LA KUMUUA MWANAE.
JE! TATIZO NI NINI HAPA?
TATIZO NI TAMAA YA MZAZI ILIOSABABISHA KIFO CHA MWANAE NA CHUKI NA HUKUMU JUU YAKE. KUSIKIA AMESIKIA LAKINI MOYO WAKE UMEMSHINDA ( UVUMILIVU UMEMSHINDA ) AKAAMUA KUBEBA MIZIGO ( CHUKI,LAWAMA,ADHABU……N.K )MIKUBWA. KWA BINAADAMU KUSAMEHE NI VIGUMU LAKINI KWA MUNGU NI RAHISI.
HII NDIO MAANA YA KUPEWA MASIKIO , NA KUYATUMIA VYEMA.KILA SIKU MAASI YANASIKIKA, KATIKA TV ,RADIO NA KATIKA MIDOMO YA BINAADAMU WENZAO.
IKIWA UMEPEWA MASIKIO NA MACHO NA UNA AKILI TIMAMU, UJUMBE HUO UNAKUHUSU, UKIUFUATA SAWA NA UKIUACHA SAWA HUKUMU IKO JUU YA NAFSI YAKO. KUMBUKA MALI ,MAGARI,MANDEGE,MAJUMBA,MKE AU WAKE ,WATOTO,NGUO ,FEDHA,CHEO,NGUVU ZA MWILI, VYOTE HIVYO VINABAKI NA SIO AKIBA YAKO TENA AKIBA YAKO, NI KILE ULICHOKITOA UKITEGEMEA FADHILA ZA MWENYEZI MUNGU.
EWE MWENYEZI MUNGU, TUNAKUOMBA UTUNUSURU, NA UBAHIRI NA MALI AU RIZIKI YA HARAMU NA UTUWEZESHE KUWA NA HURUMA NA KUWASAIDIA BINAADAMU WENZETU.
AMINA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment