KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, April 24, 2009

Ubaguzi Mashariki ya Kati




Katika khali ya kustajabisha hivi karibuni kulifanyika mkutano nchini Uswizi ili kuzungumzia kuhusu Ubaguzi kidunia! La ajabu ni kwamba mataifa makubwa yenye ushawishi wa khali ya juu yalijitoa kaitika mkutano huo kisa? Raisi wa Irani atakuwa mmoja wa wasemaji katika mkutano huo! Na hoja ya raisi huyo ilikuwa inahusu taifa la Israeli kukalia kwa mabavu ardhi ya wapalestina! Je kuongelea jambo hili ni ubaguzi? je kukwepa na kujitoa katikati ya mazangumzo ni ubaguzi? Je ni kweli dunia imefika mahali imekuwa na upofu wa kutoona nini ni haki na nini si haki? Je nani anabaguliwa huko Mashariki ya mbali? Israeli au Palestina? nani anapata tabu? nani amekataa tamaa? nani anaishi katika hofu?nani anakosa huduma zote muhimu kama shule, maji,umeme,miundombinu,hospitali?
Alafu kwenye mkutano mkubwa kama huu kwanini Afrika haikuzungumziwa?je sisi hatuna khali ya kubaguliwa? je utumwa ule wa zamani wa mwili na utumwa huu wa sasa wa kiakili si ubaguzi? ikiwa wanaisraeliwalilipwa kwa maovu waliyotendewa na wajerumani sisi waafrika mbona kimya? nani atatulipa? nani atadai haki yetu toka kwa hawa mabwana wakubwa? je afrika tutaendelea kutothaminiwa mpaka lini? na sisi tunamtazamo gani kwa mateso ya wenzetu wapalestina? je tunajitahidi vipi kuona haki zao na zetu zinapatikana! kisha ebu sema , Jeshi la mrusi lilipo vamia na kuipiga georgia dunia nzima ilihamaki je mbona huko kongo,somalia,sudani,uganda.madagaska,chadi nani anasema juu yao?Au ubaguzi una maana tisizozijua? mfano ugaidi,ugaidi unamaana gani!
Ubaguzi ni kitu kibaya sana iwe wa kifikra au kimwili.
tafadhali jamani kwa pamoja tupige vita ubaguzi wa aina yoyote ile hapa katika uso wa dunia yetu!
Tuombee haki kwa kila kiumbe cha Mola
Waafriaka Amkeni Kifikra!
Mapambano bado yanaendelea na ndio twaweza kufanya na kufanikiwa tukiwa na umoja na kuondowa husda na fitna na chuki na uroho wa madaraka katika nafsi zetu.
Mungu Bariki Afrika
Mungu ibariki Dunia Nzima!

No comments:

Post a Comment