KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, August 26, 2010

Nigeria kubinafsisha sekta ya umeme




Serikali ya Nigeria imezungumzia kuhusu mipango ya kubinafsisha sekta ya nishati nchini humo, kutokana na matatizo ya ukosefu na uhaba wa umeme mara kwa mara.
Kituo cha kutoa umeme

Vituo vya umeme kubinafsishwa

Serikali imesema kwamba imeamua kuacha kuhodhi biashara hiyo, na kuuza vituo 11 vya kusambaza umeme.

Habari za kuuzwa kwa kampuni ya serikali, PHCN, zimetangazwa na Rais Goodluck Jonathan.

"Tunahitaji mageuzi katika sekta ya nguvu za nishati", alielezea katika hotuba iliyofikiriwa kuwa muhimu sana.

Vile vile serikali itaruhusu makampuni ya watu binafsi kuanzisha vituo vyao wenyewe vya uzalishaji gesi, nguvu za umeme kwa kutumia maji na vile vile makaa ya mawe.

Nigeria imekuwa ikikabiliana na tatizo lal upungufu wa umeme mara kwa mara, na biashara nyingi zimekuwa zikitegemea jenereta.

Nchi ya Nigeria ni kati ya mataifa yanayouza kiwango kikubwa cha mafuta duniani, lakini huduma nyingi hazipatikani, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa umeme.

Raia wengi wa Nigeria wamekuwa wakifanya utani kwamba ufupisho wa jina la kampuni ya taifa ya nishati, PHCN, kirefu chake kwa Ki-ingereza ni 'Please Hold Candle Now', yaani, 'Tafadhali Shikilia Mshumaa Sasa'.

Ripoti iliyotolewa miaka miwili iliyopita, ilielezea kwamba Nigeria inahitaji dola bilioni 85 katika kuimarisha miundo mbinu inayohusiana na umeme, ili raia wake milioni 140 waweze kupata stima kwa saa 24 kwa siku.

No comments:

Post a Comment