KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, August 26, 2010
Umoja wa mataifa kujadili ubakaji-Congo
Mabalozi katika Umoja wa Mataifa wanasema baraza la usalama la umoja huo litafanya kikao cha dharura kujadili kubakwa kwa zaidi ya kina mama 150 katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanaoishi karibu na kituo cha wanajeshi wa kutunza amani wa umoja wa mataifa.
Wanajeshi hao wanasema walisikia habari za kubakwa kwa kina mama hao na waasi, siku kumi baada ya tukio hilo, licha ya kuwa wanajeshi hao walikuwa wakishika doria kijiji hicho.
Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa Mashariki mwa Congo, Roger Meece anasema wanakijiji hao waliamua kutosema lolote kuhusu tukio hilo kutokana na hofu ya kushabuliwa tena na pia aibu.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema, anajukumu la kuuliza ikiwa jambo fulani lingefanyika ili kuzuia tukio hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment