KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Wednesday, May 26, 2010
Wanajinsia moja wakamatwa Zimbabwe
Mawakili wamesema, wanachama wawili wa shirika la kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja Zimbabwe wamewekwa rumande.
Mawakili hao wamesema wanakabiliwa na makosa ya kumiliki picha za uasherati na kumtukana Rais Robert Mugabe.
Ellen Chadian- afisa mtawala wa kundi hilo la wapenzi wa jinsia moja Zimbabwe- na Ignatius Muhambi ambaye ni mhasibu- ndio waliokamatwa.
Mapenzi ya jinsia moja ni kinyume na sheria Zimbabwe, lakini shirika hilo limeruhusiwa kufanya shughuli zake nchini humo.
Dzimbabwe Chimbga, wakili anayewawakilisha watu hao wawili, amesema walikamatwa siku ya Ijumaa.
Bw Chimbga amesema, " Mashtaka ya awali ni kwamba wamekutwa na picha za uasherati."
Amesema, " Sasa polisi wanataka kuongeza shtaka la kumtukana Rais."
Waandishi wanasema Bw Mugabe amekuwa akiwaelezea wapenzi wa jinsia moja, "wenye thamani ya chini hata kumfikia mbwa na nguruwe", lakini kukamatwa kwa watu wa namna hiyo ni nadra sana Zimbabwe.
Mapenzi ya jinsia moja ni kinyume na sheria katika nchi nyingi za Afrika.
Wiki iliyopita jaji mmoja nchini Malawi alitoa hukumu ya miaka 14 gerezani pamoja na kazi ngumu kwa wapenzi wa jinsia moja baada ya kufanya sherehe za uchumba za kiutamaduni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment