KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, May 26, 2010

Meles Zenawi aelekea kushinda uchaguzi


Tume ya Uchaguzi nchini Ethiopia imesema kwamba matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu uliokamilika siku ya Jumapili, yameonyesha kuwa chama cha waziri mkuu wa nchi hiyo Meles Zenawi, kinaelekea kushinda.

Tume hiyo imesema chama hicho kimeshinda katika maeneo 9 kati ya maeneo 11. Shirika la kutetea haki za kibinadam lililo na makao yake nchini Marekani, la Human Rights Watch, limesema uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki.

Shirika hilo limedai wapiga kura wengi walidhulumiwa na kushurutishwa kuipigia kura chama tawala. Madai kama hayo pia yametolewa na viongozi wa upinzani. Waangalizi wa Muungano wa Ulaya EU, wamesema kwamba wanachunguza madai hayo ya wizi wa kura na udanganyifu kabla ya kutoa ripoti yake..

Waziri mkuu wa nchi hiyo Meles Zenawi ambaye ameongoza taifa hilo kwa karibu miaka 20 amekanusha madai hayo.

No comments:

Post a Comment