KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, May 26, 2010

Malema asisitiza hakutenda kosa lolote


Kiongozi wa vijana katika chama tawala cha African National Congress ANC, nchini Afrika Kusini ametetea mienendo alilazimika kuomba msamaha hadharani kwa kukikosea heshima chama hicho cha ANC, kufuatia matamshi yake kuhusu masuala yanayohusu ubaguzi wa rangi, serikali ya Zimbabwe na rais wa nchi hiyo Jacob Zuma.

Katika mahojiano ya kipekee na BBC, Malema amekataa kukubali kuwa alitenda makosa na kusema kwamba anahisi kutelekezwa na watu ambao alikuwa akiwategemea ndani ya chama hicho.

Amesema uchumi wa taifa hilo umegawanyika kwa misingi ya kikabila na kwamba ataendelea kupigania haki za Waafrika weusi ambao wamekandamizwa.

Malema ameongeza kusema kuwa huenda asikome kuimba wimbo ulioimbwa wakati wa harakati za ukombozi wa taifa hilo ambao una maneno yanayosema ''ua wazungu''. Mahakama moja nchini Afrika Kusini ilimzuia Malema kuimba wimbo huo hadharani.
yake baada ya kuadhibiwa na chama chake.

No comments:

Post a Comment