Waasi wa Sudanese Liberation Movement, SLM, wamepongeza uamuzi wa majaji wa mahakama ya kimataifa ICC, wa kuchunguza upya ikiwa, rais wa Sudan, Omar Al Bashir anastahili kufunguliwa mashtaka ya mauaji ya halaiki, katika eneo la Darfur.
Majaji hao, walitupilia mbali uamauzi uliokuwa umetolewa awali, kuwa upande wa mashtaka haukuwa umewasilisha ushahidi wa kutosha, ili Bwana Al Bashir, afunguliwe mashtaka hayo.
Msemaji wa SLM, Yahya Bashir, amesema kuna ushahidi wa kutosha mashinani kuthibitisha kulikuwepo mauaji ya halaiki katika eneo la Darfur.
Amesema makundi ya waasi yanapaswa kufunguliwa mashtaka ikiwa yatapatikana na hatia
No comments:
Post a Comment